Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Mie binafsi nakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa hapa nchini hakuna njaa. Tanzania ni moja wapo za nchi ambazo mwenyezi Mungu ameipa kila aina ya neema lakini watu wake hawataki kuitumia ipasavyo kwa sababu ya kutotaka kufanya kazi haswa za kilimo.
Leo nchi kama Misri yenye idadi ya watu karibu Milioni 100 wanaishi kwa kutegemea kilimo cha umwagiliaji kutoka mto Nile inakuwaje hapa Tanzania tuna maziwa na mito mengi mbali mbali na mvua kunyesha mara kwa mara tunashindwa kuwa na chakula na kusingizia njaa?
Sasa hivi tuna kiongozi asiyekuwa mnafiki anachowaambia watanzania ni ukweli mtupu na inatakiwa mkubaliane na ushauri wake kwamba kuna wafanyabiashara na wanasiasa wanajaribu kutengeneza hili suala la njaa kwa manufaa ya kujipatia umaarufu wa kisiasa na faida ya kibiashara.
Mshabiki
 
Magufuli ana chakula amekitoa wapi?au ana kipi cha kumuingizia hela katika serikali yake.?zaidi ya kodi ya wananchi.
Kila mtu abebe msalaba wake Rais siye wakushughulika na mambo madogo km ya njaa wakati wataalam wamejaa kibao wamebweteka tu
 
Mnataka watu wafanye kazi gani?kwani hawajalima?.
8b4bdfa98b02389a7ade559ac85648e4.jpg
"Poor minded people will always blame politicians for their own problems "

Fanyeni kazi watanzania, acheni maneno ya wanasiasa, hata kama chakula kimepungua serikali haiwezi kuwalisha ninyi nyote, tuna uchumi gani wa kulisha nchi nzima hata kwa wiki mbili? Wanasiasa wanawadanganya oooh serikali haiwajali wananchi wake wakati wa njaa sasa hao wakiingia madarakani wataweza kuilisha nchi hii hata wiki mbili in case kuna njaa?
Ni kweli sisi bado ni maskini wa vipato, tusikubali kua maskini wa akili, kukaa tunalaumu laumu kila kitu, igeni mifano ya wachaga wao wanachakarika, wakati nyie wengine mnalialia wao magari yanaongozana kwenda Moshi kusheherekea Christmas sasa wao wako Tanzania gani? Au wote ni wapiga dili?
Fanyeni kazi bhana
 
Nawe nadhani inapaswa kuchange jinsi ya kushauri, why not sasa tusimpe rais hii changamoto kuwa serkali iboreshe miundo mbinu ya umawagiaji kwa kuwa kuna source za maji nyingi ili tulime? hii inaweza kumjulisha tu kuwa serkali ikiboresha kama walivyofanya maeneo mengi tunao uwezo na dhamira ya kufanya kazi,
Hatufai Basi kama hajui kuhusu hii changamoto na Hana mpango huo! Alituaminisha kuwa anayafahamu matatizo ya Watanzania na yeye ndiye suluhisho! Sasa badala yake ye mwenyewe Ni tatizo badala ya suluhisho!
 
"Poor minded people will always blame politicians for their own problems "

Fanyeni kazi watanzania, acheni maneno ya wanasiasa, hata kama chakula kimepungua serikali haiwezi kuwalisha ninyi nyote, tuna uchumi gani wa kulisha nchi nzima hata kwa wiki mbili? Wanasiasa wanawadanganya oooh serikali haiwajali wananchi wake wakati wa njaa sasa hao wakiingia madarakani wataweza kuilisha nchi hii hata wiki mbili in case kuna njaa?
Ni kweli sisi bado ni maskini wa vipato, tusikubali kua maskini wa akili, kukaa tunalaumu laumu kila kitu, igeni mifano ya wachaga wao wanachakarika, wakati nyie wengine mnalialia wao magari yanaongozana kwenda Moshi kusheherekea Christmas sasa wao wako Tanzania gani? Au wote ni wapiga dili?
Fanyeni kazi bhana
Tuwalaumu serikali kwa matatizo yetu?kwani sisi ndo tumeleta njaa?

Yale mahindi yamenunuliwa kwa hela za nani?
 
Hatufai Basi kama hajui kuhusu hii changamoto na Hana mpango huo! Alituaminisha kuwa anayafahamu matatizo ya Watanzania na yeye ndiye suluhisho! Sasa badala yake ye mwenyewe Ni tatizo badala ya suluhisho!
Nadhani anajua Chanzo cha matatizo yetu ndio maana anasema tufanye kazi na kucreate mazingira ya kufanya kazi ili Kuishi.
 
Nadhani anajua Chanzo cha matatizo yetu ndio maana anasema tufanye kazi na kucreate mazingira ya kufanya kazi ili Kuishi.
Watu wanafanya kazi, nae tumemwajiri afanye kazi sii mipasho! Pia aache uongo!
 
Acha kufikiri tofauti na maumbile ya asili. Tumia ubongo kufikiri. Aliyewambia wananchi ni wavivu ni nani? Mbivu wewe unayewaza na kaamua kununua ndege badala ya kutengeneza miundombinu ya kilio cha umwagiliaji. Hao unao wait a wavivu wataweza je kuharisha irrigation programmes wakati pesa yote mmelala akina jag dish Singh? Mere meta? Green finance? Iptl nk nk? Fikiri kwa ubongo mpendwa. Hao waziri walikaa barazani wakapanga Siyo wewe unayetoa matamko majukwaani . Budget kwenye jukwaa? Nina uhakika hata hao walikuwa hayo mamlaka wanakushangaa sana na huenda wanajua sana
 
Back
Top Bottom