Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Ni aibu kusema Tanzania kuna njaa

Nikiangalia hekari zangu 4 mahindi yanakauka then ww unasema ni uvivu natamani hata nijitoe muhanga kwako. Najua upo town unapesa za kununua chakula sasa kisipofika sokoni utanunua nn
Sasa unamiini ccm ndo inasababisha mahindi yako kukauka?
 
Vifo ni matokeo ya njaa ambayo mnadai ipo lkn dalili za njaa sio kifo. Tanzania hakuna njaa wala dalili za njaa bali kuna upungufu wa chakula ulio sababishwa ukame uliozikumba baadhi ya wilaya lkn chakula kilichopo kwenye mikoa mingine ambayo haijakumbwa na ukame kinatosha kusustain nchi mpk mwakani halafu vile vile upungufu mkubwa upo kwenye mahindi pekee lkn nafaka zingine hazina upungufu kama mtama mchele uwele na mazao jamii ya kunde kwahiyo hakuna njaa na haitatokea besides mvua zimeanza kunyesha kwa mfano wilaya ya rufiji huwa wanapanda mpunga tar 20 mpk 25 ya kila dec ya mwaka lkn kutokana na kuchelewa kwa mvua wameanza kupanda tarehe 5 January baada ya kupata mvua kuanzia tar 1 jan sasa kuchelewa huko kutasababisha NJAAAA?
Uongo huwa unakuja kwa spidi Kali sana. Ukweli ndio mwisho wa yote.

Tusubiri.
 
Jamani tembeeni maeneo mbali mbali ndo mje na maneno yenu humu jf
 
Siku zote binadam hana shukurani yule mlikuwa mnamwita Dhaifu sasa wasasa anawasafishia nchi ni mbaya pia what kind of Presidential material you want?
Suala la first lady kila kiongozi ana hulka yake kama Mheshimiwa hataki kumhusisha mambo ya siasa ni dhambi?
Rais Magufuli kama mwanadamu hakosi mapungufu lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpe
1484227975693.jpg
 
Nilichogundua... WATU WATAMKOSOA JPM SIKU AKIWA NJE YA MADARAKA

Wengi hawawezagi kumkosoa raisi aliyeko madarakani
 
Mie binafsi nakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa hapa nchini hakuna njaa. Tanzania ni moja wapo za nchi ambazo mwenyezi Mungu ameipa kila aina ya neema lakini watu wake hawataki kuitumia ipasavyo kwa sababu ya kutotaka kufanya kazi haswa za kilimo.

Leo nchi kama Misri yenye idadi ya watu karibu Milioni 100 wanaishi kwa kutegemea kilimo cha umwagiliaji kutoka mto Nile inakuwaje hapa Tanzania tuna maziwa na mito mengi mbali mbali na mvua kunyesha mara kwa mara tunashindwa kuwa na chakula na kusingizia njaa?

Sasa hivi tuna kiongozi asiyekuwa mnafiki anachowaambia watanzania ni ukweli mtupu na inatakiwa mkubaliane na ushauri wake kwamba kuna wafanyabiashara na wanasiasa wanajaribu kutengeneza hili suala la njaa kwa manufaa ya kujipatia umaarufu wa kisiasa na faida ya kibiashara.
Umeandika kwa kujikomba sana. Tatizo LA nchi yetu ni Sera. nchi nyingi zinazofanya vzr katika kilimo ni za watu waliojitambua. kilimmo kinafanywa na watu au mashirika machache yenye mitaji mikubwa na kwa technolojia ya halo ya juu. Lkn kwa kilimo HK cha mkono na kuendelea kuwadhulumu haohao wanaozalisha kiduchu. Bado tutaendelea kuimba nyimbo zlzl. Tubadili Sera tuache roho mbaya njaa itapotea
 
I am not too extreme at all. I am telling the truth and nothing BUT THE WHOLE TRUTH. Do you want me to do standing ovation on your lies (on mediocre performance)!?

BAK cool down don't be too extreme.
 
Wakati wa kikwete bajeti ya kilimo (pembejeo) ilikuwa billion 70.sasa ni bilioni 10. +kiangazi unategemea nini? Kama sio bombadia?.

Lengo lilikuwa zuri ilitumikaje? (Huruma ya JK na kuwaamini kupita kiasi waliokuwa chini yake kulichangia wengi wetu kumtukana kama vile si kiongozi wetu.) Je ilifika kwa wakulima au iliishia kulima Ofisini? Kama ilifika kwa wakulima kilio cha njaa leo kinaanzia wapi? kwamba wakulima wanatakiwa kuwezeshwa kila kitu na kila siku kwa mazao yote au kwa mazao maalum? kama kwa mazao maalum ni yapi? na kwa nini?

Mtaalam mmoja makini Dr.Bagambi( anisamehe kama nimekosea namna ya kuandika jina lake aliandika Makala ndefu nini kifanyike kudhibiti njaa na kuhamasisha wakulima.Alipendekeza kanda maalum kwa mazao,sababu za mapendekezo yake na tija iliyotarajiwa.Sikumbuki kama tunaolalamika leo kuna kitu tulichangia au hatua tulizochukua kwa ngazi zilizo chini yetu.

Waweza kukosa mamlaka katika ngazi ya Taifa lakini ukawa na mamlaka katika ngazi ya Mkoa,Wilaya,Tarafa,Kata,Kijiji au familia yako.Huna nguvu ya kimaamuzi labda je hata kushauri huwezi,kushawishi huwezi kuonyesha kwa vitendo pia huwezi?

Kwa maoni yangu jukumu la kila kiongozi wa familia ni kuhakikisha kuwa kuna uhakika wa chakula kwa familia yake.Ukikuta familia ambayo baada ya miezi mitatu ya msimi mpya wa kilimo kuanza inalia njaa na familia hiyo ni ya wakulima na hali ya hewa ya msimu uliopita hapakuwa na tatizo la hali ya hewa wala janga lililoathiri familia nzima kwa msimu mzima wa kilimo hapo hayupo kiongozi makini.
 
Umeandika kwa kujikomba sana. Tatizo LA nchi yetu ni Sera. nchi nyingi zinazofanya vzr katika kilimo ni za watu waliojitambua. kilimmo kinafanywa na watu au mashirika machache yenye mitaji mikubwa na kwa technolojia ya halo ya juu. Lkn kwa kilimo HK cha mkono na kuendelea kuwadhulumu haohao wanaozalisha kiduchu. Bado tutaendelea kuimba nyimbo zlzl. Tubadili Sera tuache roho mbaya njaa itapotea

Mnalalamika bei ya chakula imepanda wakati huo huo mnalalamika wakulima wanadhulumiwa.Nakubaliana na hoja ya kutowapangia bei mazao yao wala kuwachagulia wakulima aina ya mazao ya kuzalisha ila siafikiani hata kidogo na upuuzi wa kulalamika kupanda bei ya mazao.
JPM tunayemwita dikteta ameona tatizo la vijana wenye nguvu kuwaachia wazee waliochoka kuwalisha wenye nguvu.Tunalalamika vijana hawajawezeshwa.

Natamani japo ninajua madhara yake vijana wa jirani zetu Kenya waazimwe ardhi yetu kwa miaka 5 halafu tujipime kama matumizi ya akili na nguvu zetu ni timilifu.
 
That's the fact l could not understand the reality
 
Nimekuja kugundua mbali na ukosefu wa chakula. Wananchi wa hali ya chini hawana hata pesa ya kununua chakula because of lack of employment.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Now you're talking Bro.

Nimekuja kugundua mbali na ukosefu wa chakula. Wananchi wa hali ya chini hawana hata pesa ya kununua chakula because of lack of employment.
 
Back
Top Bottom