Godoro la kioo
JF-Expert Member
- Aug 2, 2025
- 364
- 727
Wakuu kama kichwa kinavyojieleza
Naomba leo tujikumbushe kidogo adhabu tulizowahi kupewa mpaka ukatamani Bora akuchape tu yaishe
1) Binafsi nakumbuka kipindi tukiwa shuleni siku Moja tulichelewa kufika
Basi siku hiyo ilikuwa zamu ya mwalimu mmoja hivi
Yule mwalimu akatuambia Mimi sitoweza kuwapiga Cha kufanya chukueni hii ndoo
Akatupatia ndoo ya Lita ishirini, Kisha akasema, pangeni mstari mmoja akae kule bombani (Bomba la maji) na mwingine akae huku mwisho karibu na ndoo
Sasa zoezi lililokuwepo ni unakinga maji kwa mikono yote miwili Kisha unampatia mwenzako na yeye anampatia mwenzake yeye Tena anampatia mwenzake hivyo hivyo mpaka ndoo ijae
Changamoto iliyokuwepo ni kwamba unakinga maji kitendo Cha kumpatia mwenzako tayar mengine yamemwagika yamebakia machache
Nakumbuka hiyo siku wengi tulilia mpaka mwalimu akaja kutusamehe
2) Nilipewa swali nikakosea jibu basi yule mwalimu alivyokuwa katili akaniambia weka miguu juu kichwa chini halafu pale chini akaweka jiwe Ili kama nikichoka na nikadondoka basi kichwa kidondokee lile jiwe sitosahau
3)Nilipitiwa na usingizi wakati wa kipindi baada ya kuniona akaniita akaniambia chukua ndoo hii hapa
Zoezi lililopo hapo ni unaenda unachota maji unakunywa halafu unatoka unakimbia Yale maji unayatemea kwenye ndoo
Changamoto ni kwamba ndoo ilikuwa mbali kiasi kwamba ukija kuifikia Ile ndoo tayari Yale maji umeshayameza
Inabidi urudi Tena. Siyo Siri nilitamani kulia
Ila shule basi tu