NHIF tofautisheni Sayansi na Siasa, Serikali ingilieni kati hili jambo

Aramun

Senior Member
Nov 8, 2023
165
745
NHIF hizi mnazofanya ni siasa kwenye uhai wa watanzania. Imagine mtu unaamua kujikamua unalipa ki NHIF chako cha laki 7, lakini unapoenda hospitali unaanza kuambiwa hiki NHIF hawana coverage yake, tena vitu basic kama sindano?, this is totaly unacceptable.

Serikali ni vizuri mkaingilia hili suala haraka sana maana huko mahospitalini hali si shwari kabisa..

*****************************************************************

Asalaam alykum waganga
Leo nimekuja kurefill dawa zangu hapa MNH- Mloganzila
Cha kushangaza kitita kipya kinalipa insulin lakini hakilipii needles.
Needle moja ni Tsh 1531.2 so kwa mwezi ni Tsh 91872 kwa Public
Na kwa kuwa nina bima ni 158k billed kama IPPM.
Niko social hapa nahamisha deni kwa muajiri.
Siwezi kukatwa bima kila mwezi na kisha nilipie Laki na hamsini na nane (158,000) ya syringe kwa mwezi.
Kama hospitali za serikali ziliona kitita hiki hakiwahusu basi Muajiri ajipange kunicredit hii 158k kila mwezi.
Labda naye ataenda kwenye vikao vya maboresho.
Unatoaje insulin hutoi syringe?
Kwetu hizi ndizo zinazoleta tofauti kati ya kuishi na kufa, then unavaa kaunda suit unasema ondoa hii weka hii.
 
Back
Top Bottom