Nimefuatilia maelezo ya chadema kuhusu madai mbalimbali na kupata wasiwasi kuwa chama hakina nguvu ya maamuzi bali kinategemea nguvu ya umma. Watanzani wengi si wanasiasa bali ni washabiki wa siasa. Kwa mtazamo wa haraka nguvu ya umma ya chadema kudai matokeo yatangazwe haraka uliona kilitokea. Chama kuwatumia wananchi kabla ya kuwaelimisha ni kuleta maafa makubwa nchini. Uingereza waliunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kutumia tu busara za viongozi wa vyama si wananchi. Vyama ni wawakilishi wa wananchi hivyo unaposhindwa kutetea hoja na kurudi kushawishi umma ni hatari kwa taifa hili. Nasikitika kusema kuwa nguvu kubwa ya chadema ni vijana wa mjini. Wote tunajua maamuzi ya vijana wengi pale unapowashawishi jambo la kufanya. Nguvu ya umma kwa chadema ni kuleta fujo tu. Katiba yenyewa iliopo umma hauijui vizuri. Tusijetukampa mbu kutibu malaria.