KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.
Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.
Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.
Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.
Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.
Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.
Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.
Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!
Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.
Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.
Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.