Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.
 
Hiyo bodi ya pamba ilipata panya buku walipiga pesa balaa.

Licha ya zao la pamba, tangu global warming awareness ianze na watu kuacha kutumia bidhaa za plastic zao la mkonge sasa hivi ni mali sana katika kuzalisha vifungashio kuanzia magunia, mikoba ya kina mama na mifuko ya sokoni.
 
Lazima nikiri bila unafiki kuwa hakika Magufuli katuangusha sana wanaccm tumebaki kutumia nguvu kubwa katika propaganda na matumizi ya nguvu.

Awamu ya JK ilikuwa na mabovu mengi, lakini yalikuwepo mazuri ambayo ndiyo ilipaswa kuyaendeleza kwa nguvu, lakini tuliyapuuza yote na kumfanya Magu kuwa ni mteule wa Mungu huku tukidanganya hili au lile ili kumpamba.

Kilemba cha ukoka hakidumu maana kinanyauka, sasa tumebaki kutumia nguvu kubwa kwa wapinzani ili kuficha udhaifu wake na kulazimisha wananchi wamuelewe positively.

Ukweli lazima tukubali kuwa kwa hali ya sasa ikiundwa Tumehuru ya uchaguzi na wenzetu wakiweka mgombea imara kama yule tuliyetaka kumtoa kwenye mzunguko na amekimbilia nje basi kupata 30% ya kura za urais tutakuwa tumejitahidi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguvu ya Soda.... Ina uhusiano gani na hiki ulichoandika?? Huna kazi ya kufanya?
 
Ngoja waje wale waliopangwa zamu ya leo waje wakanushe kila kitu ulichokisema. Lakini waswahili wana msemo wao, mficha maradhi kifo humuumbua.

Kama kwenye viwanda tumerudi nyuma, kama kwenye kilimo cha mazao hasa ya biashara hatufanyi vizuri kuanzia uzalishaji, kuchakata na hata kuuza nje, kama uvuvi umeathirika na viwanda vya uchakataji samaki vimefungwa na orodha ni ndefu ni nini sasa kinaendelea kwenye uchumi wetu!!!?

Zisipochukuliwa hatua za haraka na za makusudi kabisa kuokoa hali, basi ni suala la muda tu tutakua na crisis ya kiuchumi. Biashara za ndani nazo bado hazijarudia hali yake ya miaka mitano iliyopita. Hata miundombinu inayojengwa kama kutakua hakuna marekebisho muhimu ya sera, sheria na nia ya dhati bado mchango wake hautaonekana sana kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
 
Hivi operesheni ya Jesh ya kuendesha biashara ya korosho iliishia wapi 😃 😃 😃 😃 😃 viwanda vya kijeshi vya kubangua korosho!

Inashangaza Sana Mambo yanaharibika Wazee wameufyata. Hata Taasisi ya Mwalimu Nyerere siku hizi ni inazidiwa hata na Mke wa Godbless Lema, hakika hizi Zama Ni Zama!
 
Kalamu1,

Ni kweli kabisa, nyie lieni na pamba sie tunalia na korosho! Serikali hii ikijiusisha tu na mazao jua wanaua, na kupora pesa zilizopo, tulikuwa tunapata miche ya mikorosho kila mwaka kupitia mfuko wa pembejeo,leo hamna kitu, walisha anza ujenzi wa ghala na kiwanda cha korosho maeneo matatu Nanyumbu, Tunduru na Tandaimba imebaki msingi tu.

Na hamna shughuli, mfuko wa pembejeo ulikuwa na mamia ya mabilioni wakaona ili wazile wavunje mfuko, baadhi ya wakulima na wasafirishaji hadi leo hawajalipwa fedha zao, ukimwona waziri wa kilimo huku akijuwa jinsi wanavyouwa zao eti anatamka tunawalinda wakulima, kuendeleza zao blabla kibao, wenye akili wameamua kumwangalia tu kama vile wabunge wa kusini.
 
Kalamu1,

Ajira pia ameshindwa. Tangu 2015 hakuna kinachoeleweka mpaka leo 2020. Kwa kushindwa kwake,aliwaaminisha watu eti uhakiki wa watumishi akasumbua weeee hadi leo mamtu yakarudishwa kimyakimya lakini vijana graduands wa vyuo hakuna ajira hata ya dawa. Tangu hapo ni ajira za kuungaunga tena kwa kutaka ujiko tu wala si vinginevyo.
Ndo ushafeli hivyo. Huendi Mbinguni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom