Nguvu ya "NENO" katika Dunia na Katika Maisha yako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
NGUVU YA "NENO' KATIKA DUNIA NA KATIKA MAISHA YAKO!

Anaandika, Robert Heriel.

Isomwe Kwa hekima Kwa walio na hekima, wapate ufahamu. Pia isomwe kipumbavu na hao waliowapumbavu, wazidi kuchanganyikiwa katika njia panda za fikra zao.
Andiko hili ni Kwa watu wote.

Neno ni sauti yenye maana. Kwa Wataalamu WA lugha, tunasema, Neno ni muunganiko wa mofimu zinazotoa sauti yenye maana.
Kiroho, Neno ni nguvu ya Sauti zenye maana, sauti hizo zinaweza kuwa zakutamkika Kwa sauti au bila ya sauti(kimyakimya)


Wataalamu WA isimu Wanasema kuna Aina ya Tungo Kwa kigezo muundo, ambazo ni; Neno, Kirai, kishazi, Sentensi. Hata hivyo leo hatupo kujadili suala la Lugha.

Taikon atajadili nguvu ya NENO katika Dunia na maisha yetu. Nitajitahidi kufupisha kadiri ya nitakavyoweza,

AINA ZA NENO.
1. NENO LA ROHONI
2. NENO LA KIMWILI.

NENO LA ROHONI.
Hizi ni sauti za kiroho ambazo hutokea Akilini, ubongoni, fikarani, na hujulikana Kama WAZO(IDEAS)
Wazo ni neno lililoko akilini, fikarani, moyoni ambalo mtu hujisemesha yeye mwenyewe au kusemeshwa na roho au Nafsi zingine.
Pale mtu anapofikiri anakuwa anazungumza Kwa sauti ya chini katika akili yake,

Baadhi ya viumbe wa rohoni huweza kusikia sauti ya akili yako pale inapojiongelesha(unapowaza) sio ajabu Majini, au Baadhi ya viumbe wa Sirini WA kiroho kuweza kuwatumia Waganga au Manabii kufanya Utambuzi wa kile unachowaza.
Hii ni kutokana na kuwa unapowaza unatumia Neno la kiroho.

Huku ndicho chimbuko la Aina ya pili ya Neno.

2. NENO LA KIMWILI!
Ni sauti zinazotamkika ambazo huunda kitu inaitwa Lugha ambacho ni chombo cha mawasiliano. Hii sina haja ya kuilezea Sana. Hata hivyo zingatia kila lugha inajitosheleza lakini zipo lugha zenye nguvu kutokana na Utajiri wa msamiati.

Lugha zenye Nguvu mfano Kingereza, Kiarabu au Kihispania, au Kireno huwezi kukifananisha na Kiswahili.

Mtu kujua Lugha yenye nguvu maana yake anaweza kuwa na nguvu ya maarifa zaidi ya mtu mwenye kujua Lugha isiyo na nguvu.
Mfano, mtu anayejua lugha ya Kijadi tuu labda lugha ya kipare au Kisukuma ataachwa mbali kimaarifa na mtu anayejua lugha ya kingereza kwani huyu ajuaye kingereza atakuwa anajua mambo mengi kuliko ajuaye lugha za kijadi tuu.

Watu wenye akili, Kwa kulifahamu hili mapema waliweza kuhakikisha wanazishibisha lugha zao Utajiri mkubwa wa maneno(NENO) Kwa kuzunguka huku na huko duniani, kukusanya utajiri(Merchantilise) sio tuu Utajiri WA Mali za kiuchumi Bali hata Utajiri WA Neno kipindi cha Mercantilism.

Hata hivyo leo hatujadili Sana suala la Lugha!

Kuna mambo lazima yafahamike kabla hatuenda mbali,

1. Uwezo wa kubadilisha Neno la roho(Wazo) kuwa Neno la kimwili.

2. Uwezo wa kubadilisha Neno(wazo) kuwa mwili(kitu) kinachoonekana.

Hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanyika pasipo kuwa NENO, Hiyo falsafa aliitoa Yohana,
Lakini maana yake ni kuwa Jambo lolote huanza Kama NENO( Likiwa fikarani huitwa Wazo, Idea,) likiwa nje huitwa Sauti au lugha.

Uwezo wa kugeuza Neno(wazo) kuwa kitu kinachoonekana Pasipo kutumia kitu kinachoonekana huitwa UUMBAJI na huu ndio anaommoja pekee ambaye ni MUNGU MUWEZA.

Uwezo wa kugeuza NENO(wazo) kuwa kitu kinachoonekana Kwa kutumia vitu vilivyopo ndio huitwa "TEKNOLOJIA na Ubunifu" hiyo wanayoviumbe.

Zingatia Kwa Mungu kila kitu kipo HAI kutokana na uweza wa NENO lake.

Wakati Kwa Binadamu au viumbe wenye utashi, nguvu ya neno, kuna viumbe hai na viumbe mfu kutokana na kuwa wao wanauwezo wa kulibadilisha neno kuwa kitu kichoonekana Kwa kutumia vitu vilivyopo. Hiyo Life Chain ndio humfanya mwanadamu kuwa na mipaka.

Kisaikolojia, kuna kitu inaitwa MTAZAMO,
Wakati Kiroho kuna kitu inaitwa IMANI.
Vyote vinafanana lakini utendaji kazi wake huwa tofauti.
Imani ni nguvu ya kutumia neno(wazo) kiroho litokee au lisitokee.
Wakati Mtazamo ni nguvu ya kutumia neno kimwili litokee au lisitokee.

Kushindwa au kufanikiwa Kwa mtu hakutegemei Jitihada zake au Mazingira aliyomo bàli kunategemea zaidi Mtazamo na Imani yake.

Mataifa Makubwa na watu wenye akili wanafahamu Jambo hili.
Kitu cha kwanza Ambacho mtu akitaka kukuharibu kwenye maisha yako, na kukushinda atatumia NENO, iwe la kimwili au kiroho.
Wazungu walitoa Propaganda kuwa wao ni Bora kuliko Sisi, walitumia maneno kila walipoweza mpaka wakafanikiwa kutengeneza MTAZAMO Kwa kizazi cha Waafrika wengi ambao mpaka Leo wanafikiri hivyo.

Huko Kwa Wazungu labda nimeenda mbali.
Mzazi au jamii inayouwezo wa kutumia maneno kukuharibu au Kukujenga.
Na ndipo hapo nguvu ya MEDIA inavyopatikana.

Hata hivyo sio kila mtu anaweza haribiwa MTAZAMO wake na maneno ya watu.
Lakini uhakika ni kuwa Kwa upande wa watoto maneno huweza kuwaathiri Kwa sehemu kubwa na kuyabadili maisha Yao na kuwa kitu chochote cha ajabuajabu au kitu kizuri chenye manufaa.

Inasemwa; Aliwazalo mtu moyoni mwake ndivyo alivyo,
Kuwaza ni kuongea moyoni mwako, Neno la rohoni.
Vile unavyopenda kujiona, kujiwaza ndivyo utakavyokuwa hapo baadaye.

Ndio maana inashauriwa usipende kuishi karibu na watu wanaongea maneno ya hovyohovyo, watu wanaokukatisha tamaa. Kwani maneno hayo yananguvu ya kubadilisha Mtazamo wako.

Hata unapoenda Kwenye baadhi ya taasisi kubwa kuomba kazi, au Unapoenda kuoa Kwa baadhi ya Familia kubwa zinazojitambua na zenye mizizi mirefu, zenye mipango ya mpaka Karne mbili au tatu maswali watakayokuuliza yatalenga zaidi kugundua Mtazamo wako kuliko kitu chochote.

Kwa mfano, mtu atakapokuuliza, Unazungumziaje kuhusu suala la Ndoa?
Hapo atataka ajue mtazamo wako juu ya ndoa, jibu lako litamfanya aone jinsi ulivyo mjinga au Mwerevu. Aone jinsi wewe utakavyokuwa miaka Mia moja ijayo, jibu lako litatoa picha vile watoto wako watakavyokubwa aidha wenye manufaa kwenye jamii au Wapuuzi na kizazi kilichoshindwa.

Neno ndilo lenye nguvu ya kumuumba mtu vile alivyo.
Mtu lazima ajue Hesabu ya watu uliopitia Kwao kuishi ili wajue walikulisha maneno gani, sio ajabu ukaulizwa unaishi wapi, ukoo wenu ni upi, kabila lako ni gani, umesoma wapi, hapo mtu atajua kuwa mtu huyu Hana future yoyote.

Kiroho, inaambiwa usingwe NIRA na wasioamini.
Kiuchumi, matajiri wanaambiwa Watoto wao waoane matajiri Kwa matajiri.
Wasomi, wanaona wachukuane wao Kwa wao.

Kwa sababu kila jamii ina NENO lake ambalo huunda Mtazamo.
Matajiri huwezi sikia mtazamo kuwa Duniani Tunapita,
Wasomi, huwezi sikia mtazamo wa Bahati,
Kiroho, wenye Imani hawana mtazamo wa kushindwa. Wao kila kitu wanaamini watashinda. Na hayo yote huletwa na NENO.

Vijana wa sasa lazima mjifunze kubadilisha Neno lililomo kichwani kuwa kitu kinachoonekana, ukiwa na Wazo usiache kulitekeleza Kwa kuogopa kuwa utashindwa.
Jiepushe na maneno yanayokatisha tamaa.
Jiepushe na watu wenye akili za wadudu.

Kumbuka kile neno linawakati wake.

Na Nipumzike sasa!

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Pishi jingine bora kabisa toka kwa Taikon

Yaani kudadeki naona attack zinakuja toka pande zote, kijamii, kimaisha, kisaikolojia, kidini, kifilosofia hadi kisayanzi na kimahesabu.

Ambaye hataelewa atakuwa kaamua tu maana injili inahubiriwa kila mahali. See more of NENO hapa👇
 
Pishi jingine bora kabisa toka kwa Taikon

Yaani kudadeki naona attack zinakuja toka pande zote, kijamii, kimaisha, kisaikolojia, kidini, kifilosofia hadi kisayanzi na kimahesabu.

Ambaye hataelewa atakuwa kaamua tu maana injili inahubiriwa kila mahali. See more of NENO hapa👇

Barikiwa Sana Mkuu.
 
Nilianza kwa kusoma comments kwa naona mada inasifiwa ngoja nitulie nisome vizuri.
 
Kwa kufupisha tu “ Tunapaswa kuwa na neno la kusimamia”
Mfano: Mimi ni Mshindi
Mimi Naweza, Mimi ni mbarikiwa, Nitafanikiwa.
Ukiwa unatembea huku akilini /Fikarani una mawazo au maneno hayo juu.

Katika Ulimwengu wa kimwili mambo yataanza kutokea na kufanikisha.
 
Alafu mnaachia uongozi watu wasio na akili wakakalie viti, Wenye akili mpo nyuma ya keyboard.
 
Back
Top Bottom