Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Deal done..!
Mark my words!
Hizi za sasa ni purukushani za muda tu na kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji..!
Ngorongoro is no longer ours..and maybe be it will never be ours again ..! Nani anakumbuka ya Loliondo? Pamoja na kelele zote zile haikuwahi kurudi kwetu...!

Siku ile pm alipoenda Arusha na ile list ndefu ya Wamasai waliokubali kuhamia ugenini huko Handeni Tanga... Ndio ilikuwa hitimisho la kuiaga Ngorongoro..

Ule mkutano
Zile picha
Yale majina
Zile video
Vyote vimechukuliwa na kuhifadhiwa vizuri kwamba kila kitu kilifanyika kwa kuzingatia haki za binadamu, matakwa ya kisheria nknk..

Hawa waliopelekewa moto leo wanahesabika kama wavamizi na ndio maana jeshi la polisi lilienda kule.. Na trust me kile kilichifanyika asubuhi ya leo ni salam tuu.. Ile ni kifungua kinywa tuu.. Full menu ya bufee itawaendea usiku kukiwa kuna kiza kinene. Hapo ndio shetani atasimamia ukucha...

Kesho yaweza kuwa siku ya kuokota mizoga, majeruhi vituo vya afya, watuhumiwa kwenye selo za polisi, na matukio ya watu kupotea huko Ngorongoro national park.

Kwa wiki chache zijazo safisha safisha itaendelea kuondoa masalia yote ya kitu kinachoitwa Wamasai wa Ngorongoro wavamizi.. Tutawekwa busy na unit za umeme kupaa, kesi za sabaya na drama zingine zote..!

Itakapofika 30/6 ndio itakuwa mwisho wa kuiona Ngorongoro uliyozoea kuiona japo kwa picha tangu ukiwa mdogo.. Kama una picha zake ama ulibahatika kufika kule na kupata kumbukumbu kadhaa..ZIHIFADHI VEMA..Hiyo bahati haipo tena!

Hakuna picha zake zitapatikana tena huko kwa uhuru na kujiachia, hakuna selfies tena za mbuga yetu ile urithi wetu...picha zitapigwa na watu maalum..! Na kwa sababu maalum...!

Na wazawa watakaoruhusiwa kuingia kule ama ni mamluki ama ni wafanyakazi wasio huru,.. Itakuwa ni kama watumwa katika nchi yao wenyewe!

Tusitaharuki zaidi, tusilie, bali tuanue tanga.. Msiba ulishaisha kwasasa tusubiri kusomwa historia ya marehemu.. Tukipata wasaa tutawasimulia wana wetu picnic, na study tour za kishule wakati pale pakiwa kwetu..
Wapishe ndio kwani wao Wana haki Sana kuliko wenzao wa kwenye migodi au wale wa Ruaha?

So long as Wana pa kwenda ,watii sheria bila shuruti maana Uhifadhi na faida zake zina tija zaidi kwa Nchi kuliko individuals hao.
 
Majaliwa tangu atudanganye jiwe linatusalimu na ni lizima la afya kumbe limefia pale mzena BASI KUMUAMINI HAIWEZEKANI. Ccm imeuza nchi na kweli jiwe tunalikumbuka japo sasa ni fuvu pale chato. Ila jiwe liliua watu sana japo tunalikumbuka.
una ushaidi wa mtu alieuliwa na Jiwe ?kuna muda tunahukumu kwa hisia tu
 
Yapo mambo kwa akili ndogo tu ya kiuanadamu unaona kabisa hili silo, unaona kabisa watu wanachota mchanga kwenye kingo za daraja unangoja utafiti kwanza ufanyike badala ya kuwaondoa haraka"
Naona unakimbia hoja kiaina
 
Kwa kweli this is sad, Hivi ni lazima nchi iliyojaliwa Resources kibao kung'an'ania hio hifadhi? labda ni kweli hifadhi ina potential ya kugenerate income kwa Watanzania, but not kwa gharama ya Maisha ya watanzania wengine... ni busara tu ilitakiwa itumike hapo, Kama wamekataa kuhama tafuta sehemu nyingine unayoweza kuinvest kama serikali, mbona simple!
Mwanzoni mwa mwaka huu nilipata fursa ya kutembea Magharibi mwa Tanzania. Nilichokiona ni nchi kuuubwa yenye ardhi yenye rutuba,mabonde na mito ambavyo havijawahi kutumika tangu kuumbwa kwa Dunia. Hata tukizaliana kwa Kasi ya aina gani hatutoimaliza ardhi ya Tanzania. Tatizo liko Serikalini, viongozi tulionao hawana maono wala mbinu sahihi za kuongoza nchi. Hivi vyama ndio kabisa, kikongwe kimepoteza dira na vipya havina itikadi wala mrengo unaoeleweka zaidi ya maslahi binafsi.... Iko siku yataibuka machafuko na mtafutano.
 

Attachments

  • IMG_20211227_140938_917.jpg
    IMG_20211227_140938_917.jpg
    1.5 MB · Views: 16
  • IMG_20211227_140926_862.jpg
    IMG_20211227_140926_862.jpg
    1.6 MB · Views: 20
  • IMG_20211227_140904_869.jpg
    IMG_20211227_140904_869.jpg
    1.3 MB · Views: 18
  • IMG_20220102_160806_056.jpg
    IMG_20220102_160806_056.jpg
    1.7 MB · Views: 17
  • IMG_20220104_113701_656.jpg
    IMG_20220104_113701_656.jpg
    1.3 MB · Views: 19
Mwanzoni mwa mwaka huu nilipata fursa ya kutembea Magharibi mwa Tanzania. Nilichokiona ni nchi kuuubwa yenye ardhi yenye rutuba,mabonde na mito ambavyo havijawahi kutumika tangu kuumbwa kwa Dunia. Hata tukizaliana kwa Kasi ya aina gani hatutoimaliza ardhi ya Tanzania. Tatizo liko Serikalini, viongozi tulionao hawana maono wala mbinu sahihi za kuongoza nchi. Hivi vyama ndio kabisa, kikongwe kimepoteza dira na vipya havina itikadi wala mrengo unaoeleweka zaidi ya maslahi binafsi.... Iko siku yataibuka machafuko na mtafutano.
Beautiful Tanganyika..!
 
Back
Top Bottom