Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Katika hizo wiki mbili pia utwambie ni nani mmiliki wa mgodi wa Buhemba maana uliomba muda na ukapewa wa kutosha.

  Posted Date: 5/26/2008
  Na Jackson Odoyo
  Mwananchi

  SIKU moja baada ya kuagizwa aipitie ripoti ya madini na atoe ushauri ndani ya wiki mbili kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja amesema kazi hiyo ni nzito na inahitaji umakini wa hali ya juu kwa sababu hilo linagusa uchumi wa nchi na maslahi ya wananchi kwa ujumla.

  Akizungumza na Mwananchi jana alisema kuwa atafanya kazi aliyopewa na rais kwa umakini ndani ya wiki mbili kama alivyoagizwa.

  Nimepewa maelekezo namna ya kufanya kazi hiyo na muda wa kutosha, hivyo sioni kitakachonifanya nisiikamilishe ndani ya muda huo,?alisema Waziri Ngeleja.

  Aliongeza kuwa atalitekeleza suala hilo kama alivyoagiza na rais kwa kuzingatia kanuni na taratibu za nchi.

  Alifafanua kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo atamshauri rais kinachotakiwa kifanyike ili utekelezaji wake uanze mara moja na kwamba, wananchi wanahitaji kunufaika na madini hayo na ndiyo maana hata rais alitoa muda wa wiki mbili ili wafanye kazi hiyo kwa haraka na umakini zaidi.

  Waziri huyo alitoa kauli hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya Rais Kikwete kupokea ripoti ya kamati ya madini aliyoiunda Novemba 20 mwaka jana ikiwa chini ya Jaji Mstaafu Mark Bomani.

  Kamati hiyo ilitoa mapendekezo mbalimbali yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa haraka ili utekelezaji wake uweze kuanza mara moja, likiwemo la kuanzishwa kwa mfumo mpya wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini nchini unaofanana na ulioanza kutumika Zambia, mwanzoni wa mwaka huu.

  Akipokea taarifa ya Kamati ya Madini jana kutoka kwa Jaji mstaafu, Mark Bomani, Ikulu ya Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema hatua hiyo ni kuharakisha utekelezaji wa mapendekezo ya kamati hiyo, aliyoiteua Novemba 20, mwaka jana.

  Alisema Serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa rasilimali ya madini nchini inalinufaisha taifa na wawekezaji.

  Taarifa hiyo imekuja na pendekezo jipya la kutaka kuanzishwa mfumo mpya wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini nchini unaofanana na ule ulioanza kutumika Zambia mwanzoni mwa mwaka huu.

  Katika mabadiliko ya Zambia, Serikali ya nchi hiyo ilisimamia mabadiliko ya sheria na taratibu za usimamizi wa sekta ya madini, pamoja na mfumo wa kodi katika sekta hiyo.

  Aliongeza kuwa awali, pamoja na kuitwa mara kadhaa na kuombwa kukutana na kamati hiyo ya Jaji Bomani, hakutaka kufanya hivyo ili kuepuka kupandikiza mawazo na mtazamo wake kwa lengo la kuipa uhuru wa kufanya kazi zake na kutoa mapendekezo yenye manufaa kwa Watanzania.

  Akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Kikwete, Jaji Bomani alisema kamati yake inaamini kuwa taarifa yao pamoja na mapendekezo yake vitafanyiwa kazi na uamuzi wa serikali utawekwa wazi ili kuondoa hisia kwamba taarifa za kamati mbalimbali huwa hazifanyiwi kazi.

  Bomani alisema katika kufanya kazi na wadau mbalimbali, wananchi wa sehemu tofauti walionyesha shauku kubwa kuhusu kazi ya Kamati yake na matarajio yao makubwa wakielekeza imani yao kwa Rais Kikwete kuwa atasimamia vyema utatuzi wa matatizo yanayoikabili sekta hiyo.

  Alisema mapendekezo ya mfumo huo mpya wa kodi yametolewa baada ya kutembelea nchi zinazosifika kuwa na usimamizi mzuri wa madini, zikiwemo Thailand, Ghana na Botswana na Zambia.

  Kamati hiyo iliyokamilisha rasmi mapendekezo yake baada ya kazi ya miezi sita ilijumuisha wajumbe 12 ambao ni Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Mark Bomani, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Idd Simba, Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe (CCM).

  Wengine ni Peter Machunde, David Tarimo, Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa katika Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha na Uchumi, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi msaidizi Idara ya Makazi, Edward Kihundwa.

  Hadidu za rejea mara baada ya kuundwa kwa kamati hiyo zilionyesha ilitakiwa kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

  Pia kamati hiyo ilitakiwa kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na kukutana na wadau wengine wa sekta hiyo kisha kutoa mapendekezo kwa serikali.

  Awali, Kamati hiyo ilipewa miezi mitatu kukamilisha kazi yake, lakini Jaji Bomani alisema ililazimika kuomba iongezewe muda zaidi kutokana na ukubwa na ugumu wa kazi hiyo.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Naye Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja alipotakiwa kutoa ufafanuzi wake jana na msimamo wa serikali katika utata uliogubika mgodi wa Buhemba alisema jambo hilo linahitaji takwimu zaidi.

  Jambo hili linahitaji takwimu zaidi halafu mimi sipo ofisini, tafadhali hebu wasilianeni na Kamishna wa Madini, atakuwa anafahamu zaidi, alisema waziri Ngeleja.

  Aliongeza kuwa suala hilo linahitaji kujiandaa zaidi na kwamba yeye atamuagiza kamishna huyo wa madini atoe ufafanuzi kwa gazeti hili.

  Suala la utata wa mgodi wa Buhemba limedumu kwa muda mrefu sasa, takribani miaka mitano, na kwamba mwishoni mwa mwaka jana wapinzani waliinyoshea kidole serikali kuhusu umiliki wake wa mgodi huo.

  Mgongano huo pia, ulisababisha Mbunge wa Musoma vijijini, Nimrod Mkono kukataa kupokea kiasi cha sh 200 milioni kama mrabaha kwa wilaya hiyo, kwa madai kuwa haikuwa inaendana na kile kinachovunwa katika ardhi hiyo. Juhudi za Kumtafuta Kamisha wa Madini jana hazikuzaa matunda.
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  wiki mbona nyingi sana ! kama kweli wana nia ya kutambua mgodi ni wa nani, wafuate waliotoa leseni wa kufanyia kazi huo mgodi na anadakwa ! lakini hii naona ni kama loop, itafika wiki 2, tutaambiwa mambo yanaendelea !
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Kada hawa ndiyo wenzio leo ndiyo unaamka? Huyu Ngeleja an kauli za kubabaisha sana .Nashangaa sijui ni mtu wa aina gani .Ni muongo hata chini ya kiapo huwa anasema uongo kisa wako madarakani .
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  ...alipewa muda wa wiki mbili na Muungwana wa kusoma ripoti ya madini na kisha atoe ushauri nini kifanywe kuhusiana na mapendekezo mbali mbali yaliyomo ndani ya ripoti hiyo. Wiki mbili zimeshapita hatujasikia ushauri wake. Je kulikoni?

  Kwa habari zaidi
  soma hapa
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jun 14, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Huyu waziri Ngeleja naye scandal kibao!... habari zake nzito sana huko alikotokea yaani hata nashindwa la kusema!...
  Hii ndio sababu kubwa inayonipa wasiwasi kubwa na uwezo wa JK kuongoza - hawa WATU WAKE!
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Mimi sina background story nzuri ya huyu mhusika, naona kama kazuka tu. Kama una data (hata zile general) naomba utupatie. Shukrani!
   
 8. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  huo ushauri ulikusudiwa uwe public amshauri rais na watendaje nn cha kufanya ?


  mbona mna kimuhe muhe nyie
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  mkuu tunaomba japo tetesi za scandal za huyu jamaa tuzifanyie kazi.
   
 10. T

  Tufu Member

  #10
  Jun 14, 2008
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kabla ya kuwa mbunge , Ngereja alikuwa mwanasheria wa makampuni ya rostam ambaye alifadhiri kampeni zake za ubunge. Kushinda ubunge na kuwa waziri wa madini ni mahususi eti.....Ngereja sio mwenzenu....
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jun 14, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ngeleja ni smart sana academically, sina wasi wasi kabisa na ukali wa kichwa chake. Ila nadhani kuwa jamaa huyu ni bogus sana politically, anafuata upepo unapokwenda
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mtandao wa kutupwa ni mmoja wa viongozi waliopigania sana ripoti ya Mwakyembe isisomwe bungeni!, wakiongozwa na Chenge, Makamba, na Almeir!

  Ukiangalia kauli zake nyingi toka ewa waziri kamili wa hii wizara, ni clear kuwa hata yey wmenyewe ana wasi wasi kama aniweza hiyo nafasi!
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ngeleja baada ya JF kumwaga mambo hadharani sasa kashikwa na kigugumizi maana wao wako kwa ajili ya Sinclair na sasa yeye kesha wamaliza .Hata hivuo ripoti haikuw akwa watanzania bali kwa akina Sinclair wamesha ipata sasa unadhani kuna uharaja tena?
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Baada ya Sinclair kupata ripoti ile ndiyo sasa tuna anza kujua kwa nini Ngeleje alisema kazi aliyo pewa ni ngumu .Haya sasa wacha tuone ushujaa wake na uzalendo kwa Nchi yake ambayo anaitumikia kama waziri .
   
 15. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ugumu wake ni nini hasa? kwamba mtandao hawajampa cha kusema au ugumu gani?Au zinalindwa siri za baraza la mawaziri zinazoendelea kuwafukarisha wananchi na kuwanyenyekea wakoloni kama Jim?
  Kamati ilitoa mapendekezo ambayo yeye ameyapitia ili yatekelezwe.
  Mwaka huu ana kazi kweli maana kila kukicha Madini na pia umeme ZENJ bado ni mazingaombwe
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Uungwana ni vitendo,kama kazi uliyopewa ni maji marefu iteme fasta kabla hujaboronga zaidi.
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Jun 14, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Sasa kama unajua hivyo,mbona unakaa hapa jamvini na kuwatetea mafisadi? Kuanzia leo basi ujadili kile chenye maslahikwa taifa.

  Afadhali kama umezinduka kidogo
   
 18. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mods hii iunganishwe,naona kuna nyingine kama hii hapa pembeni inaendelea
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jun 14, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Susuviri,

  Mkuu unajua tena sisi wengine hatuna ushahidi ndio maana nimeyaacha kama yalivyo na kubaki domo wazi. Labda nitakachosema ni kwamba kutoka kwa Karamagi na kuingia Ngeleja hakubadilisha kitu zaidi ya sura. Huyu ni mshirika mkubwa kama mwanasheria ktk kundi hilo la Chukua chako Mapema (mafisadi), isipokuwa uteuzi wake umetokana na kwamba hajulikani..
  Habari nilizozipata hazifai mkuu kuziweka hapa unless nipate uhakika zaidi, nimejifunza mengi JF hasa ktk ngazi hii na kusema kweli ni muhimu kuwa na uhakika kwanza...Unajua tena binadamu husema mengi sana mazito. Labda moja kubwa naloweza kulisema ni kwamba Ngeleja ni mshikaji, mshiriki mkuu ktk kundi la Boyz to Men..ambao macho yao yalikuwa ktk madini toka wakati wa Mkapa.
   
 20. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ....Kivipi?
   
Loading...