Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu

ngeleja anasema tatizo ni nini hadi leo mgao bado unaendelea na utaisha lini? leo nimevaa nguo hazijapigwa pasi kwa mara ya kwanza ofisini!
Tatizo siyo Ngeleja , taizo ni hakuna Techniciens au wataalam wa Umeme Tanzania, Tanzania has not yet even thinking of incubeting engineers and technicien for this matter. Hakuna wabunifu na wataalaam wa umeme Tanzania(practically hawapo, Theoretically na kifisadi wapo) sasa unataka Ngeleja awatoe wapi hao practically? hata kwenye ujenzi wa mabarara Tanzania inategemea Wachina, Wajapan, Wataliano, na hakuna aliyehitimu Chuo Kikuuu Cha Dar Mjenzi wa Barabara kwa sababu ni Watu wa theories. Maji nayo Dar Shida tu. Maji taka nayo shida tu. Naona ni vizuri kujipanga na kuweza ku incubet vijana wetu hata kupitia mabilion ya JK.. badala ya kuwanyima nafasi na kusababisha ugumu wa kupata ajira.
 
Tatizo siyo Ngeleja , taizo ni hakuna Techniciens au wataalam wa Umeme Tanzania, Tanzania has not yet even thinking of incubeting engineers and technicien for this matter. Hakuna wabunifu na wataalaam wa umeme Tanzania(practically hawapo, Theoretically na kifisadi wapo) sasa unataka Ngeleja awatoe wapi hao practically? hata kwenye ujenzi wa mabarara Tanzania inategemea Wachina, Wajapan, Wataliano, na hakuna aliyehitimu Chuo Kikuuu Cha Dar Mjenzi wa Barabara kwa sababu ni Watu wa theories. Maji nayo Dar Shida tu. Maji taka nayo shida tu. Naona ni vizuri kujipanga na kuweza ku incubet vijana wetu hata kupitia mabilion ya JK.. badala ya kuwanyima nafasi na kusababisha ugumu wa kupata ajira.

Hii kiboko.... hata wale maprof wa masuala ya Production, Electrical + Energy engineering kumbe nao vilaza tu!!?

Ila mimi nadhani pamoja na yote kuna mambo yanasahaulika taratibu....

Kwanza sio kweli kwamba hakuna watu competent na creative katika sekta ya nishati hapa nchini, tatizo kubwa ni kwamba once ukiingia kwenye huu unaoitwa utumishi wa umma, last say aliyenayo ni mwanasiasa na mara nyingi wanasiasa wenyewe ndo huwa kama akina Ngeleja! How do u expect mtu anayefanya kazi chini ya Ngeleja kutimiza kazi zake ipasavyo kama sio kuishia kujaza mafaili na ushauri usiotumika? Mwisho wa siku hawa wahandisi, wanasayansi na wabunifu wetu nao huona ni bora waingie katika ulingo wa siasa ili na wao wapate kufaidi hii keki inayoliwa na wachache wasio na hata uwezo wa kuelewa ushauri wa kitaalamu na kuuchukua.

Cha pili ni kwamba inaonekana wazi serikali yetu inafurahia kero kama hizi kuwepo kwa wananchi.
 
The electricity system is totally broken. It is not working, and it never will if not fixed.....NOW!
Need to fix this once and for all.

- Right now, Option ya extra capacity iliyopo Tanzania yetu hii, kupunguza makali ya mgao ni IPTL (100MW, heavy fuel oil) + DOWANS (70-100MW, natural gas); Zote mbili zina siasa chafu kabisa.
- IPTL iko chini ya mufilisi(serikali) na wameweza kuzalisha umeme hapa kwa muda mrefu kiasi, mara nyingi hutoa 10MW kila siku. Tatizo walilo nalo kwa sasa ni mafuta, hawana au ndo yanaishia. (Serikali imeshindwa kuleta mafuta mpaka leo. Kwanini? Scarcity of money, don't care attitude, sleeping at the switch, who knows). It doesn't take months for oil to travel from the Gulf to Tanzania - this we know.

- Pia in the near future watakua na tatizo la spare parts za engines - supplier problem - so don't expect full 100MW from IPTL any time soon.

- DOWANS ni politically sensitive issue. In short, no politician will push for this plant to be used, even though it can be fully operational in short order. Even if it is decided to finally run it there is one problem: there is not enough gas in that one and only one pipeline from Songo songo, to supply all the gas plants ( yaani ubungo, tegeta, songas + dowans). So you wont get 100% from DOWANS either.

So, now what:
We have to wait for the rains - that is if they show up!
as for right now, well, we are screwed.
it is going to be mgao like this for a while, You should put that in your expectations framework.

Lets forget about short-term relief solutions (hapa watakula tu, tena wenyewe). There needs to be a very loud debate for a long term solution. You don't hear any new ideas from our politicians/representatives. Any new ideas should include dismantling/restructuring the now crapy TANESCO. Anything else ni yale yale hakuna jipya!.
 
Ngeleja anaendelea na ahadi zake lukuki za kuboresha hali ya umeme nchini sasa hivi Bungeni. Sijui kama watamruhusu John Mnyika azichambue ahadi hizi. Pamoja na mengi anayoyasema kuna kukodi majenereta mengine tena!

Hawa jamaa either ni vihiyo au wana ajenda ya siri ya ku-criple uchumi wetu. Which I believe is the case.Mimi najiuliza, hivi ni busara kung'ang'ania Mtera kweli na hizi other very expensive sources kama IPTL? Kwa nini tusichukue umeme kutoka Zambia,Congo DRC au hata Uganda?Hata kama tunasema we want our own source, basi tunge-develop Stiegler's Gauge.Mm..., kazi kweli kweli.
 
Huyu jamaa hopeless sana. Alipojinasibu pale ikulu siku alipoapishwa nilidhani ana mabwawa yake ya kuzalisha umeme kwa sababu mtu mwenye akili yake na mwenye kujua uzito wa dhamana yake hawezi kutamka kwamba kuanzia sasa mgao wa umeme basi wakati ni yeye aliyekuwepo kabla ya kuapishwa kwake. Hawa watu ni sumu kwa maendeleo ya nchi na ndiyo wanaompa wakati mgumu mpendwa Rais wetu ambaye amewaamini akawa nafasi akidhani ni watu wenye upeo, uzalendo na uwajibikaji kumbe ni watu wa hovyo na vibaraka wa EL na RA na ambao hawana maadili. Kila kukicha ni ku-plot namna ya kuchukua rushwa na kuifilisi nchi hii. Ni huyu huyu aliyetoa orodha feki ya wamiliki wa dowans halafu baadae anaulizwa maswali anasema yeye siyo msemaji wa dowans. Enzi za mwalimu hawa wangesikia habari za kufukuzwa kazi kwenye taarifa ya habari ya saa saba au saa mbili usiku. Hata huko kwenye mafuta ya IPTL yeye akili yake iko kwenye kula kitu kidogo na hana aibu hata chembe maana rushwa yake sasa anaiombea kwenye sms.
 
Makinda lazima ajue ndani ya bunge yeye ni spika sio kada wa ccm na nje ya bunge yeye ni spika na kada. Ananisikitisha sana huyu mama kwa double standards zake -na hii yote ni tatizo la ombwe la uongozi ndani ya chama kinachoelekea kufa -makindaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tenda haki mama wewe ni spika ndani ya bunge acha kutuangamiza mama -basi tumia hekima za kuwa mama kulikomboa taifa acha kutumia ukada wako ndani ya bunge.
 
Huko Egypt Mubarak aliisuspend katiba kwa muda wote aliokuwa madarakani,sioni tofauti yoyote na bongo,huko nako katiba iko likizo!
Solution ni kuanza upya kama wamisri,tofauti na hapo ni kuendelea kuumizana tu....Too much conflicts of interest and this issue is almost unresolvable in the current situations....Kwa hali yoyote ile,bila mapinduzi wananchi wataendelea kuumizwa tu,labda watafikia level ya intolorence kwasababu ndo tunakoelekea,hata hivyo tolerence level ya wabongo ni extremelly high kwa maoni yangu.
 
anatakiwa atoe kauli ya kushtua wengi, aseme kama mramba alivosema katka ununuzi wa ndege ya raisi kipnd cha uongozi wa mkapa''hata watanzania wale nyasi pesa ya ndege itapatikana'' anachotakiwa kusema wazir ngeleja ni...."hata watanzania wale nyasi vinu vya kufua umeme vitajengwa" hapo kidogo tutaon[a kafanya la mana ila kukodisha majenereta ni mchezo wa kihuni hauna tofauti na dowans na richmond. Quote=wildcard;1624365]ngeleja anaendelea na ahadi zake lukuki za kuboresha hali ya umeme nchini sasa hivi bungeni. Sijui kama watamruhusu john mnyika azichambue ahadi hizi. Pamoja na mengi anayoyasema kuna kukodi majenereta mengine tena!
[/quote]
 
Ngeleja anaendelea na ahadi zake lukuki za kuboresha hali ya umeme nchini sasa hivi Bungeni. Sijui kama watamruhusu John Mnyika azichambue ahadi hizi. Pamoja na mengi anayoyasema kuna kukodi majenereta mengine tena!

Mkuu of course serikali imeshindwa kuongoza hivyo it has to stay aside wengine waongoze, 50 years ya Uhuru ni blah blah kila siku lakini at whose expense?
Tumeongea swala la Nuclear Energy mwaka wa kumi no development no nothing, wakibanwa bungeni na wapinzani wachache ndiyo wanaibua hoja ya uranium kwa ajili ya kuwapa watanzania matumaini, utafikiri wote wana upungufu wa kinga mwilini
 
Nchi hii hata tambwe hiza anaweza akawa rais akaongoza anavyopenda na watanzania tukaishia kulalamika pembeni tu. Tangu uhuru mpaka leo bado tunaongelea suala la umemeeeee!!! Ajabu na kweli!.
 



Na Deodatus Balile


NI KARIBU miezi miwili sasa tangu nimesitisha kuandika safu hii. Niliisitisha si kwa nia mbaya, bali kutokana na majukumu ya ghafla yaliyonifika, baada ya kuteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni hii ya New Habari (2006) Ltd, zamani ikijulikana kama Habari Corporation. Napenda kuwashukuru watangulizi wangu katika nafasi hii, wale waliofikiria na kuniteua kushika wadhifa huu na wasomaji ambao mara kwa mara mmekuwa mkinipigia simu za pongezi.

Sikutaka uteuzi wangu utangazwe haraka, bali nilitaka nichape kazi kwanza umma uniambie kwa kuangalia bidhaa zetu tangu nishike wadhifa huu zina mwelekeo upi, kisha wanihukumu kama nimezididimiza au kuna jinsi nilivyozibadili mwelekeo. Siku hizi kila nikipokea simu asilimia kubwa wananiambia neno utakalodhani wamepanga kabla ya kunipigia simu, nalo si jingine bali wanasema hivi: “Magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, The African na Bingwa yamebadilika na yamependeza.”
Sitanii, maneno haya hawayatamki kwa mpangilio huo huo, kwani hata kama ungekuwa wimbo ni vigumu kundi kutamka neno kwa neno, na nukta kwa nukta kwa wakati sawia, hivyo mshororo huo nimeuweka kuwasilisha mantiki ya wanayoyaeleza hao wanaonipigia simu. Wengine wanasema tumeamua ‘kujivua gamba’, mimi nasema hakuna la ajabu tulilofanya zaidi ya kuheshimu misingi ya taaluma. Ninachoomba na kushukuru ni ushirikiano wa sasa ninaopata kutoka kwa wafanyakazi wenzangu na wasomaji, nikiwaahidi kwa pamoja kuwa sasa kaeni mkao wa kula, mambo mazuri yanakuja.

Safu hii leo inaongozwa na kichwa cha habari kisemacho, ‘Ngeleja ameamua tufe kifo cha umeme’. Kifo ni jambo baya. Tukiwa na ndugu zetu, jirani zetu, mke, mume, mtoto, baba au mama, hakuna wakati unapata kufikiria kuwa yupo mmoja kati ya hao uwapendao atakutoka na usimuone tena milele. Mara nyingi, kama mmekaa sehemu yoyote, mtu akitumbukiza mazungumzo ya kifo, watu huzizima, furaha hutoaweka na wengi humsihi aliyeanzisha mazungumzo hayo kuyasitisha.

Leo kutokana na ukubwa wa tatizo la umeme katika nchi yetu, nimeona ni bora nitumie mfano huu mbaya wa kifo. Kama ni malaria ‘tumejitahidi’ kusambaza neti (ingawa mtu ana kitanda cha futi sita anapewa neti ya futi tatu) kampeni kemkem zimeendeshwa, lakini sasa tumekwepa kifo cha malaria tunaelekea kufa kifo cha umeme. Serikali kupitia Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), imetangaza mgawo wa mwezi mmoja kati ya Mei 19, hadi Juni 18. Mgawo huu unatangazwa kwa sababu tu ya kuondokewa na megawati 200 kwenye gridi ya taifa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhadisi William Mhando, umeme utakuwa unakatwa saa 2:00 asubuhi na kurejeshwa saa 5:00 usiku kila siku kwa muda huo wa siku 30. Hapa ndipo nasema tumechagua kifo chetu. Muda unaorudishwa umeme si wa kazi, bali ni wa usingizi (kwa utamaduni wetu). Wenye viwanda ni bora wajiandae kufunga viwanda kwa siku hizo 30. Na inawezekana si siku 30, bali zitakuwa hata siku 90.

Sitaki kutoa ahadi mbaya, maana ningependa kufanya hivyo ningesema ahadi ya Serikali kuwa mgawo wa umeme utapata ufumbuzi ifikapo Julai, mwaka huu, ni ndoto za mchana. Ningekuwa na uwezo wa kutoa ahadi ningesema hivi; umeme ukiwaka na mgawo ukakoma ifikapo Julai, basi kichwa changu halali yao. Nashindwa kutoa ahadi hii maana hata wenye kutoa ahadi ya ukomo wa mgawo wa umeme, wanajua kuwa hautawaka ifikapo Julai, ndiyo maana hawawezi kukubali tucheze wote kamali hii.

Sitanii, nimeyasema haya, kutokana na fikra finyu zilizoonyeshwa na viongozi wetu, ambazo zinalihakikishia taifa hili kifo cha taratibu. Kwamba mwaka 2006 mwekezaji ajulikanaye kama Alstom Power Rentals, alipeleka mtambo wa kuzalisha megawati 40 kwa mafuta mazito ya mitambo huko Mwanza, ikashindikana kuzalisha umeme. Mwekezaji huyu mitambo yake iliwashwa kwa saa 12 tu za majaribio, lakini alilipwa kila alichostahili kwa mujibu wa mkataba na akatia kibindoni mabilioni bila kuzalisha umeme hata uniti moja kwa muda wa miaka miwili. Tatizo ni nini? Alikosa mafuta, kwani hakuna miundombinu ya kupeleka mafuta Mwanza. Reli mbovu, hatuna bomba la mafura Dar es Salaam hadi Mwanza na malori hayatoshi.

Ukiacha mwekezaji huyu, leo tunao mtambo wa umeme wa Tanzania Independent Power Limited (IPTL). Mtambo huu una uwezo wa kuzalisha megawati 100, lakini kutokana na ukosefu au upungufu wa mafuta unazalisha kati ya megawati 50 na 80. Ikumbukwe mtambo huu uko Dar es Salaam, kilomita zisizofika tatu kutoka kwenye ukingo wa Bahari ya Hindi, bahari ambayo meli zinaitumia kusafirisha mafuta kutoka Uarabuni kuja Tanzania.

Namaanisha nini? Ninachosema ni kwamba Serikali na Tanesco wameshindwa kununua na kupeleka mafuta ya kutosha pale ITPL kuzalisha megawati 100 za umeme, leo wanakodisha mitambo ya mafuta hayo hayo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 260, wakisema megawati 60 zitazalishwa Mwanza na megawati 200 Dar es Salaam. Wakati wakiyasema hayo, hatujaona ukijengwa mfumo mpya wa kupakua mafuta katika Badari ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga au Mtwara wenye kutuhakikishia kuwa watu hawa wako ‘serious’ na wanachokisema.

Sitanii, nikizungumza na rafiki yangu William Mganga Ngeleja, mara zote ananipiga maneno ninayopata shaka kuyaamini. Huyu ndugu yangu ni msomi, mwanasheria mzuri na kijana anayejua kujenga hoja, ila katika hili nadhani amekwama. Kama alikuwa anatumia ‘4wheel’ alipofikia sasa, gari limekwama kwenye tope, ‘difu’ imegusa chini, hivyo anahitaji ‘kreni’ ya kulinyanyua au kulivuta kutoka kwenye tope hili. Nafahamu kuwa ndugu yangu huyu anajua kitu kinachoitwa ‘opportunity cost’ kiuchumi.

Fasiri sahihi ya uchumi ni matumizi ya rasilimali kidogo, dhidi ya mahitaji yasiyo na mipaka (economics is the use of limited resources against unlimited wants). Opportunity Cost hata kwenye Kiswahili chetu tunalo hili. Kupanga ni kuchagua. Utakuwa baba wa ajabu ikiwa mtoto wako ana homa ya malaria, una Sh 500 mfukoni na wewe ni mvutaji mzuri wa sigara, hivyo unapaswa kuchangua kati ya kutumia hiyo Sh 500 ukamnunulia mtoto dawa ya mseto akapona malaria au kununua sigara ukaivuta na ukakata kiu yako. Wapo wanaoweza kushindwa kufanya uamuzi sahihi katika hili. Eti katika mazingira hayo wewe msomaji ungenunua nini kati ya sigara na dawa ya mseto?
Kama nilivyotoa fasiri ya uchumi hapo juu, mahitaji ni mengi, tena kuna fasiri pana zaidi kuwa kuna mahitaji na matakwa (needs and wants). Unapofika katika kupanga matumizi nyumbani, huanzi na chumvi. Mshahara unapochelewa kutoka, kitu cha kwanza unawaza kiroba cha unga, kisha mchele, maharage, ndipo inakuja anasa ya chumvi, mafuta, kitunguu, na samaki au nyama. Katika shida ya kweli, kulumanga ugali ni suala la kawaida. Akina sie pangu pakavu tunayajua haya. Napata shida na mipango anayoitangaza ndugu yangu Ngeleja.

Nasikitika kuwa kila ukizungumza na Ngeleja atakutajia mipango ya muda mfupi, muda wa kati, muda mrefu na mingi ya mipango hii inakwenda hadi 2025. Kwa maneno matamu anayoyatoa sawa na mchora picha hewani, unavutika kumsikiliza. Hata hivyo, nimeanza kuapta wasiwasi. Naelekea kuamini tunafanya kazi ya kufukuza upepo. Mwanzo na mwisho wetu unaweza usifahamike.

Sijaona juhudi za makusudi na zenye mwelekeo chanya za kulikomboa taifa hili. Leo ni ukeli usiopingika kuwa sehemu yoyote yenye umeme katika nchi hii imechangamka. Shughuli za biashara kuanzia kwa mama ntilie, mafundi uwashi na mchundo, wenye viwanda na mashirika ya kati na makubwa, umeme ndiyo nguzo ya maendeleo. Hatuwezi kujitapa katika nchi yetu kuwa tutaendelea kwa kuendelea na matumizi ya umeme wa megawati 575.

Kwanza napata wasiwasi kama hata hizo megawati 575 tunazotangaziwa zinatimia. Kinachonipa wasiwasi ni kama tukio la sasa. Kwamba wakati wa matengenezo ya mitambo hiyo ya Songas zitakuwa zinaondoka megawati 200 kwenye gridi ya taifa nchi inapata mgawo wa umeme kwa saa 15, ni ishara kuwa matumizi halisi ya umeme tunaoutumia kabla ya kuchakachua takwimu ni megawati 300 kwa nchi nzima. Nasema tufike mahala tuone aibu. Afrika Kusini wanatumia megawati 72,000. China wanatumia megawati 280,000. Marekani wanatumia megawati 360,000. Sisi megawati 300. Aibu.

Sitanii, nilitarajia Ngeleja katika kipindi hiki cha uongozi wake, angeweka kando porojo, akachagua mradi mmoja tu akasema ‘Nakufa nao’. Miradi iko mingi yenye kutajwa. Miezi miwili iliyopita nilitembelea Mradi wa Ngaka. Hawa tayari wameonyesha uwezekano wa kuzalisha megawati 400 kutoka katika Wilaya ya Mbinga Songea, lakini uzalishaji unafanyika Kyela, na wakubwa hawa wanasafirisha makaa ya mawe kwa kutumia Ziwa Nyasa kisha wanafua umeme pale Kyela. Unajua tatizo lililopo? Ni aibu.

Umeme huu unaweza kuzalishwa ifikapo Juni, yaani wiki mbili zijazo, lakini hivi ninavyoandika makala hii, Ngeleja atanikosoa kama siko sahihi, umeme huu bado hata ukizalishwa utabaki kutazamwa kama tembo mweupe. Gridi ya Taifa inasafirisha umeme kwa msongo wa KV220, na umeme huu utazalishwa kwa msongo wa KV400 hadi KV420. Ukiingizwa kwenye gridi ya taifa kama ulivyo, italipuka. Japan wametusaidia wanaendelea na upanuzi wa miundombinu hii kwa kujenga msongo wa KV400 kutoka Shinyanga hadi Iringa Mjini, lakini Serikali yenyewe haijasema itafanya nini kuunga kipande cha Iringa hadi Kyela unapozalishwa umeme huu.

Acha hiyo. Shirika la Uwekezaji la Taifa (NDC) limepata mwekezaji kutoka China. Nilizungumza na Mwenyekiti wa NDC, ambaye ni Mbunge wa zamani wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya, akasema wamepata Wachina wanaotaka kutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma, kuzalisha umeme wastani wa megawati 600, ambapo sehemu ya umeme huo wataiingiza kwenye gridi ya taifa na sehemu ya nyingine wataitumia kuzalisha chuma kwenye eneo la Liganga, Ludewa.

Wachina hawa wamejitokeza pia kujenga hata gridi ya taifa yenye msongo wa KV400 ambayo ni ya kisasa kutoka Ludewa hadi Mufindi karibu na kiwanda cha Karatasi cha SPM Mgololo, lakini napo ni aibu tupu. Eti sasa kuna mgogoro mzito Mchina huyu anakataliwa kujenga transmission line, kwa maelezo kuwa hiyo ni kazi ya Tanesco kujenga line kama anataka awakabidhi Tanesco fedha wao ndiyo wajenge line. Thubutu! Uchukue mchwa ulaze majani yaliyokauka juu yake? Wachina, taifa ambalo ni la pili kwa utajiri kwa sasa, wanasema kama mpango ni kukabidhi fedha kwa Tanesco basi tusahau.

Sitanii, weka kando hiyo. Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), lenyewe limejitoa muhanga. Likaitaka Serikali ilikabidhi mgodi wa Kiwira. Kampuni ya Tan Power Resources iliyoununua ikashindwa kuuedesha ikadaiwa kuwa inadai ina mali zake hivyo Shirika la Consolidated Holding (CHC) likapewa jukumu la kukagua hesabu za Kiwira makabidhiano yaweza kufanyika. Hapa Kiwira ingeweza kuzalisha hadi megawati 600. Ukizungumza na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa NSSR, Yacoub Kidula, anasema hata wakiamshwa leo asubuhi wakaambiwa anzeni taratibu za kuzalisha umeme fedha wanazo si za kwenda kukopa. Wako tayari kulipa hata mikopo iliyochukuliwa na wakubwa ‘wakasafishia nyota’. Lakini roho mbaya ya wakubwa, wapi bwana, hawapewi mradi huu. Wapeni Kiwira mjiepushe na aibu iliyopo mbele yenu.

Nasema ndugu yetu Ngeleja sasa umefika wakati wa kufanya maamuzi magumu. Sisemi ujivue gamba, ila kuna kila sababu ya wewe kama Waziri mwenye dhamana na suala la Umeme (wala sitazungumzia mafuta na mchezo wa bulk importation katika safu hii leo) usimame utwambie Watanzania ni mradi upi utaanza kutoa angalau megawati 50 ndani ya muda gani, bila kukisia. Heshima yako itapanda kwa kiasi kikubwa brother, ukithibitika kuwa unataja mipango inayotekelezeka. Ukikaa kwenye kiti na kusubiri kuletewa makabrasha ya mipango iliyoachwa na wakoloni bila ‘akili ya kuambiwa kuchanganya na ya kwako’, mwisho wa siku utaondoka na kuacha historia pekee ya kuongeza orodha ya idadi ya mawaziri wa Nishati na Madini waliopata kushika wadhifa huo.

Ila napenda kuamini sisi Watanzania tumezichoka ahadi zisizotekelezeka. Hatutaki uitishe mikutano na waandishi wa habari kutueleza mipango ya Serikali yenye kulenga kutatua matatizo ya umeme yanayotukabili, bali tunataka mkutano ujao na waandishi wa habari, utuite sisi wanahabari kutushirikisha uzinduzi wa mradi angalau wa megawati 20 za umeme kuwa zimeingia kwenye gridi ya taifa, na si kwamba zitaingia. Tumezichoka porojo, sasa tunataka umeme si maneno matamu.
Suala la mafuta, bado nalifanyia uchunguzi kujiridhisha iwapo ndani yake kuna mchezo mchafu, nini kimekwamisha kanuni kutungwa kutoka mezani kwa Waziri mwenye dhamana na lini mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja utaanza kuepusha uchakachuaji wa bei unaua uchumi wetu pia. Nikikamilisha nondo zote, hii nayo nitaiweka bayana.
Mwisho, nasema mitambo ya mafuta ya kukodisha ni kitanzi na pengine ‘kanyabwoya’ kwa taifa hili, na wanasiasa wa nchi hii mjiepushe na mchezo wa kuifanya Tanesco kuwa gunia la mazoezi. Kila anyetaka umaarufu, anaona njia pekee ni kuwenda kuwakoromea Tanesco na kuwaelekeza upi ni mpango mzuri kwa maendeleo ya shirika hilo. Hapa ndipo kifo chetu kilipolala. Tunataka umeme, si maneno. Tukutane wiki ijayo. deobalile@yahoo.com au 0784404827/0713404827.
 
Bei ya umeme wenyewe hata kama upo: Bei ya nguzo moja Tzs.800,000 - 1,000,000/=( je kama nguzo tatu inakuwaje) , Service charge Tzs.400,000/=, Gharama ya kuhonga mafundi na meneja maana list ya wajeja ni ndefu Tzs.250,000/=, Gharama ya kumleta mpima njia ya umeme toka nguzo na Braket Tzs.50,000, Gharama ya vifaa vingine vya toka nguzo mpaka braket Tzs.500,000, Gharama ya kuweka wiring ndani ya nyumba yako Tzs.500,000/=

TANZANIA YENYE NEEMA?? TANZANIA YA CCM. Tutafika tumechoka sana!!
 
...Inawezekana kuna ugumu wa kufanya maamuzi magumu! Ugumu wa kuamua kuachia ngazi kwa kushindwa kunamfanya Mheshimiwa Ngeleja kung'ang'ania nafasi ya uwaziri wa nishati na madini ilhali ameshindwa kuleta ufanisi kwenye wizara hiyo inayoelemewa na mzigo wa kushindwa kutatua katizo na au upungufu wa umeme Tanzania. Kwa ujumla, Ngeleja ameshindwa kazi! Na hakika hakustahili kuwepo kwenye nafasi anayoishikilia hadi sasa...yapo mengi anayoweza kujivunia, kama waziri, lakini si hali ya nchi kuwa gizani huku yeye (kama waziri mwenye dhamana na nishati na umeme) akikodoa macho...! Nadhani kuna sababu zinazomfanya ang'ang'anie wizarani japokuwa HAWEZI KAZI! Nani anampa kiburi na jeuri ya kubaki hapo! Nadhani kuna watu wawili (majina yanahifadhiwa kwa sasa) waliyempa kazi hiyo katika kulinda na kusimamia maslahi ya kimkakati kwenye wizara nyeti na muhimu kwa uchumi wa nchi. Tusubiri na tuone ahadi za umeme wa uhakika....kama si ndoto ya mchana!
 
...hawa mawaziri kwa uzoefu wangu wanawajibika zaidi kwa CCM kuliko kwetu sisi wananchi. nenda kwenye nyumba nyingi za mawaziri na wabunge utakuta umeme full time ndo maana wao wanateteana saaana na si ajabu wanatushangaa tunavyotaka ajiuzuru. dawa ni kuiitoa tu CCM madarakani na kuweka wengine watakaowajibika kwetu wananchi
 
In Tanzania we dont fear crooks, we fear honest ministers who are wrong in their decisions. in good faith the Government has gone in public to wish Tanzanians well. yes Tanzanians have had confidence in the Government. unfortunatly your method of Governance NISHATI NA MADINI!!...your now failling dismally to to get out the good in Tanzanians.

Following what transpired in BUNGE last Friday + today Monday as cabinet ministers, have you asked yourself what constitutes a successful government? Yes, your right to govern, also entitles you a duty to develop Wananchi in TZ. the enlighted ruler is one who is incharge of a developmental dictatorship. Yes we have the noble duty to advise, assist, guide and correct your ministers into doing your jobs properly. the logic you should learn from us is that the better the ruller, the weathier the Wananchi. that dont judge your success by your ownwealth. that the rullers success has to be based on the wealth and happiness of his people PERIOD. now, who benefits from the Gold extracted from Tz? from mobile phones? from land grabbing? MPS have benovolently given you all necessary figures, where do you get the courage to ignore them? yes we have by design decided to forget about the colonial tratment and as a result cowardice na kulinda vyeo has began to take over a previous couraged us generation.

Mwl J.K.N shapped and dictate well both our economic + foreign policy. he used his skills to get parliament and well minded leaders and wananchi to alley with him, yes the untimelly death of J.K.N Rob bed TZ of the bright future. now the leadership has turned its back on all J.K.Ns policies and his allies the Chinese, Russians, Cubans etc, in the light of what your doing. as cabinet ministers, do you have courage to talk about principles and look at the people direct in their eyes?
PROVIDE UMEME
S.H. KASORI
 
Kazi aliyopewa ngumu sana.... ameendelea kuvurunda miaka yote hii, lakini bado hataki kujiuzulu!!!!
 
Back
Top Bottom