BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
Katika hizo wiki mbili pia utwambie ni nani mmiliki wa mgodi wa Buhemba maana uliomba muda na ukapewa wa kutosha.
Posted Date: 5/26/2008
Na Jackson Odoyo
Mwananchi
SIKU moja baada ya kuagizwa aipitie ripoti ya madini na atoe ushauri ndani ya wiki mbili kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja amesema kazi hiyo ni nzito na inahitaji umakini wa hali ya juu kwa sababu hilo linagusa uchumi wa nchi na maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Akizungumza na Mwananchi jana alisema kuwa atafanya kazi aliyopewa na rais kwa umakini ndani ya wiki mbili kama alivyoagizwa.
Nimepewa maelekezo namna ya kufanya kazi hiyo na muda wa kutosha, hivyo sioni kitakachonifanya nisiikamilishe ndani ya muda huo,?alisema Waziri Ngeleja.
Aliongeza kuwa atalitekeleza suala hilo kama alivyoagiza na rais kwa kuzingatia kanuni na taratibu za nchi.
Alifafanua kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo atamshauri rais kinachotakiwa kifanyike ili utekelezaji wake uanze mara moja na kwamba, wananchi wanahitaji kunufaika na madini hayo na ndiyo maana hata rais alitoa muda wa wiki mbili ili wafanye kazi hiyo kwa haraka na umakini zaidi.
Waziri huyo alitoa kauli hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya Rais Kikwete kupokea ripoti ya kamati ya madini aliyoiunda Novemba 20 mwaka jana ikiwa chini ya Jaji Mstaafu Mark Bomani.
Kamati hiyo ilitoa mapendekezo mbalimbali yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa haraka ili utekelezaji wake uweze kuanza mara moja, likiwemo la kuanzishwa kwa mfumo mpya wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini nchini unaofanana na ulioanza kutumika Zambia, mwanzoni wa mwaka huu.
Akipokea taarifa ya Kamati ya Madini jana kutoka kwa Jaji mstaafu, Mark Bomani, Ikulu ya Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema hatua hiyo ni kuharakisha utekelezaji wa mapendekezo ya kamati hiyo, aliyoiteua Novemba 20, mwaka jana.
Alisema Serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa rasilimali ya madini nchini inalinufaisha taifa na wawekezaji.
Taarifa hiyo imekuja na pendekezo jipya la kutaka kuanzishwa mfumo mpya wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini nchini unaofanana na ule ulioanza kutumika Zambia mwanzoni mwa mwaka huu.
Katika mabadiliko ya Zambia, Serikali ya nchi hiyo ilisimamia mabadiliko ya sheria na taratibu za usimamizi wa sekta ya madini, pamoja na mfumo wa kodi katika sekta hiyo.
Aliongeza kuwa awali, pamoja na kuitwa mara kadhaa na kuombwa kukutana na kamati hiyo ya Jaji Bomani, hakutaka kufanya hivyo ili kuepuka kupandikiza mawazo na mtazamo wake kwa lengo la kuipa uhuru wa kufanya kazi zake na kutoa mapendekezo yenye manufaa kwa Watanzania.
Akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Kikwete, Jaji Bomani alisema kamati yake inaamini kuwa taarifa yao pamoja na mapendekezo yake vitafanyiwa kazi na uamuzi wa serikali utawekwa wazi ili kuondoa hisia kwamba taarifa za kamati mbalimbali huwa hazifanyiwi kazi.
Bomani alisema katika kufanya kazi na wadau mbalimbali, wananchi wa sehemu tofauti walionyesha shauku kubwa kuhusu kazi ya Kamati yake na matarajio yao makubwa wakielekeza imani yao kwa Rais Kikwete kuwa atasimamia vyema utatuzi wa matatizo yanayoikabili sekta hiyo.
Alisema mapendekezo ya mfumo huo mpya wa kodi yametolewa baada ya kutembelea nchi zinazosifika kuwa na usimamizi mzuri wa madini, zikiwemo Thailand, Ghana na Botswana na Zambia.
Kamati hiyo iliyokamilisha rasmi mapendekezo yake baada ya kazi ya miezi sita ilijumuisha wajumbe 12 ambao ni Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Mark Bomani, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Idd Simba, Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe (CCM).
Wengine ni Peter Machunde, David Tarimo, Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa katika Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha na Uchumi, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi msaidizi Idara ya Makazi, Edward Kihundwa.
Hadidu za rejea mara baada ya kuundwa kwa kamati hiyo zilionyesha ilitakiwa kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.
Pia kamati hiyo ilitakiwa kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na kukutana na wadau wengine wa sekta hiyo kisha kutoa mapendekezo kwa serikali.
Awali, Kamati hiyo ilipewa miezi mitatu kukamilisha kazi yake, lakini Jaji Bomani alisema ililazimika kuomba iongezewe muda zaidi kutokana na ukubwa na ugumu wa kazi hiyo.