Ngeleja akiri kazi aliyopewa ngumu

Mimi nianvyojua maana ya kampeni ni kuwashawishi wapiga kura wakuchague na kuwaelezasera ya chama,
sasa huyu Ngeleja anavyowatishia kwa hiyo ina maana wakichagua CCM watakuwa wanafanya kazi bure bila kulipa mapato,
Hapoa anajaribu kuonyesha CCM ni chama cha aina gani (thats why sipendi siasa)
 
......
Katika hali inayoonekana kuwa vitisho, Ngeleja alisema kama CCM itashindwa kwenye uchaguzi huo, wachimbaji hao watashukiwa kwa nguvu zote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuona kama kweli wanalipa kodi ya serikali.

“Moja ya mkakati ambao tumeandaa ni kwamba kama CCM haitashinda, TRA itakuja hapa kwa ajili ya kuhakiki kama kweli mnalipa kodi ya mapato, ikiwa ni kinyume chake mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya serikali,” alisema Ngeleja.
..............

Jamani mmesikia hiyo? Kama jimbo lako lina mbuge wa CCM hakuna kulipa kodi. Kodi ni kwa majimbo yenye wabunge toka upinzani tu. Kaaaazi kwelikweli. Hao ndo askari wa mwavuli wa JK. Mhhhhh! kwa namna hii ili tupate maendeleo TZ tunahitaji kufanya mapinduzi. CCM has to go out, no way.
 
Amenukuliwa na vyombo mbalimbali, chombo gani, kasema nini? Weka maneno ya Ngeleja hapa tuyaone.

Maana si tunajadili kauli tata ya kiongozi. Niwekee kauli hiyo niione basi, halafu tutajadili. Press tunayo...
inaonekana wewe hupiti humu ndani mara kwa mara.
 
Jamani mmesikia hiyo? Kama jimbo lako lina mbuge wa CCM hakuna kulipa kodi. Kodi ni kwa majimbo yenye wabunge toka upinzani tu. Kaaaazi kwelikweli. Hao ndo askari wa mwavuli wa JK. Mhhhhh! kwa namna hii ili tupate maendeleo TZ tunahitaji kufanya mapinduzi. CCM has to go out, no way.

Mkuu Mashauri, hizo ni dalili za mfa maji, haishi......
 
Toka lini Waziri akatoa kibali, kama sio Kamishina wa Nishati au Kamishina wa Madini, inaelekea Mheshimiwa hajui mipaka ya kazi yake wala sheria anazo zisimamia (Sheria ya Madini na Sheria ya Madini).
 
Huyu jamaa hajawahi kuwa na sifa za kuwa waziri. Alipewa hicho cheo kwa kuwa ni mwanamtandao na pia kwa nguvu ya papa no.1. Kwani hata akiongea huwa haongei kama kiongozi atekelezi majukumu yake mfano mpaka sasa anasubiliwa atoe taarifa kuhusu Kiwira yuko kimya, Dowans mlisikia jinsi anavyotumiwa, Nchi inajitahidi kukusanya kodi wewe unawaambia wachimbaji kuwa wasipochagua CCM watashukiwa na TRA so it means CCM no kulipa kodi!

Hii ndiyo hasara ya kuweka vihiyo wa uongozi kwenye hizi serikali zetu. INABIDI WAPIGWE CHINI HAWA
 
Mugerezi!

Uko sahihi kabisa. Huyu Billy Ngeleja ni mtoto wa Kisukuma mwenye mapepe anatakiwa apepewe tumtoe majini! Kauli zake ni za kitoto na kusema kweli ni kibaraka wa Rostam Aziz alikuwa mwanasheria wa Vodacom. Hilo genge la watu ambao wanaharibu taaluma ya Sheria including the stupid Lawrence Kejo Masha!

Mashine za DOWANS bado ziko pale Ubungo sasa yakaribia mwaka mmoja tangu Jakaya Mrisho Kikwete aka Vasco da Gama atoe amri ya kuvunja mkataba na kuziondoa.. Badala ya kutoa maelezekezo na mwelekeo anakwenda kucheza chakulaga kule Busanda.

Do you know as a lawyer and Minister for Energy and Minerals hajaweka kwenye GVT gazzete uamuzi wa kuachana na Dowans kwa hiyo because we are all wapumbavu (INCLUDING myself) Sitoshangaa come September Dr. Idris akaja na hoja ya kutumia hizo mashine kuzalishia umeme kwa ajili ya uhaba KIZa alichotutangazia na Vasco akampa hongera.

Tuombe Mungu wamshitaki kwenye SCANDAL ya RADA othrewise habari ni mdundiko!

What goes around comes around ndaga fijo tumwombee Mwakyembe asife kwani the picture itaanza upya naapa!
 
ukweli mawaziri wote walio kuwa busanda mwezi huu wasilipwe mshahara wametuibia watanzania hawawezi kuacha ofisi zao nakukaa huko mwezi mzima huku wakiiba hati za wapiga kura
 
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na menejimenti ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), keshokutwa wanakabiliwa na mtihani mgumu baada ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuweka wazi kwamba wanatarajia kuwabana kutokana na makosa mbalimbali ya kiutendaji.

Kamati hiyo ya Nishati na Madini, tayari imeandaa hoja zenye lengo la kuwahoji mawaziri kadhaa ambao utendaji wao hasa utekelezaji wa maagizo ya Bunge umekuwa hauna tija.

Kubainika kwa hali hiyo, kunatokana na taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinazoeleza kuwa, Kamati ya Nishati na Madini, inajipanga kuibana serikali iipatie mkataba mpya wa Kampuni ya kuchimba madini ya Petra Diamond Limited ya nchini Afrika Kusini, inayotaka kumiliki mgodi wa almasi wa Mwadui uliopo mkoani Shinyanga, baada ya Kampuni ya Willcroft Diamond Limited (WDL) kunyang’anywa mgodi huo na serikali.

Taarifa za uhakika ambazo zimelifikia gazeti hili zinaeleza kwamba, Ngeleja atawekwa kitimoto na kamati ya Nishati na Madini katika vikao vya Kamati za Bunge vinavyoendelea jijini Dar es Salaam na baadaye Bungeni kutokana na kutowasilisha taarifa ya mgodi huo kama alivyotakiwa na kamati hiyo Aprili, mwaka huu.

Kadhalika, Ngeleja atalazimika kueleza sababu za Tanesco kutowasilisha taarifa ya mpango mkakati wake (master plan).

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Shellukindo, alikiri kuwa pamoja na kwamba kamati yake ilimwagiza Waziri Ngeleja kuwasilisha taarifa kamili na mkataba wa kuendesha mgodi huo kabla ya mkutano wa Bunge uliopita, hajafanya hivyo.

"Hadi sasa Kamati yangu haijapata taarifa wala mpango mkakati wa Tanesco, lakini sisi hatuna wasiwasi kwa sababu tunajua tutamkamata Ngeleja wiki ijayo, mambo mengine subiri utayapata wakati wa kamati," alisema Shellukindo na kuongeza kuwa "yeye mwenyewe anajua kwamba hawezi kuikwepa kamati yangu...kwa sababu pamoja na mambo mengine, anategemea tuipitishe bajeti ya wizara yake kwa hiyo hawezi kutukwepa,".

Katika vikao vya Kamati za Bunge vilivyokaa jijini Dar es Salaam katikakati ya mwezi Aprili, kamati ya Nishati na Madini ilishtushwa na taarifa ya serikali kuhusu mgodi wa Mwadui uliokuwa unaendeshwa kwa ubia kati ya serikali na Kampuni ya Willcroft Diamond Limited (WDL).

Kampuni ya Willcroft Diamond Limited imeieleza serikali kuwa inadaiwa deni la dola milioni 87.5 jambo ambalo serikali haikubaliani nalo na hivyo imemwagiza mkaguzi kulihakiki kabla haijalikubali.

Hata hivyo, serikali imekwisha achana na kampuni hiyo na tayari imesaini mkataba wa awali na Kampuni ya kuchimba madini ya Petra Diamond Limited ya nchini Afrika Kusini.

Kamati ya Shellukindo ilidai mkataba huo ambao serikali imeusaini na kampuni ya Petra, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa una utata na kwamba kamati ingeujadili ili kurekebisha upungufu uliomo.

Ngeleja alikwishatangaza kwamba serikali inatafuta kampuni huru ambayo itaweza kuchunguza uhalali wa deni hilo kwa kuwa linatiliwa shaka.

Kadhalika, kamati hiyo ilikataa kujadili mpango mkakati wa Tanesco kutokana na shirika hilo kuchelewa kuiwasilisha kama ilivyotakiwa kufanya.

Shellukindo alisema kamati yake itahitaji taarifa za kina kutoka kwa Waziri wa Nishati na sababu za kutowasilishwa kwa taarifa hizo kwa wakati. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Kamati za Bunge, Wizara hiyo itakutana na Kamati ya Shellukindo Jumatano wiki hii, ambapo itakuwa inawasilisha taarifa ya utendaji wake kwa mwaka wa fedha unaoishia Julai, 2009.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima, alipozungumza na Nipashe kwa njia ya simu alikataa kuzungumzia ucheleweshwaji huo wa taarifa na badala yake alikata simu.

"Mwulize Katibu Mkuu wa wizara ndiye mwenye ratiba ya vikao vya Bunge," alisema Malima na kukata simu.

NIPASHE

Here we go again. Our leaders can talk the talk but they hardly walk the walk. Lets see if they will live up to there words au kama ni business as usual
 
Hawa wanataka kuuza magazeti wajua ngeleja hivi sasa..anakuwa ana nguvu sana baada ya kufanikisha ule ubunge wa Busanda.....maana aliweka kambi mwezi mzima.....na pia yeye ni mwana mtanadao hakuna wa kumsulubu Bungeni......JK na RA tuu ndio jama anawagwaya zaidi hakuna....................
 
Tanesco yaibuka na tahadhari mpya yataka Sh312 bilioni kununua mitambo
broken-heart.jpg
Na Leon Bahati

BAADA ya kimya cha muda mrefu, Shirika la Umeme (Tanesco) limeibuka na kuiangukia Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiomba iikingie kifua ili itengewe Sh312 bilioni kwa ajili ya kununulia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura nchini, huku ikitahadharisha kuwa nchi inaweza kuingia gizani.

Shirika hilo limeamua kuachana na Wizara ya Nishati na Madini, ikidai kuwa ilishawasilisha maombi hayo muda mrefu, lakini ikaona hayafanyiwi kazi ndio maana limeamua kuyapeleka maombi hayo ya dharura kwenye kamati hiyo ili iikingie kifua.

Tanesco, ambayo sakata lake la kutaka kununuliwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited, lilizimwa na kamati hiyo ya Bunge, limesema kama serikali haitaharakisha mpango huo mapema, kuna hatari ya nchi kuingia gizani kwani tayari baadhi ya vituo vya umeme nchini vimezidiwa nguvu ya matumizi kwa asilimia 10.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya kamati hiyo, jana, mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashidi alisema upungufu huo wa umeme tayari umesababisha kuanza kwa mgawo wa umeme kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na sasa tatizo hilo linaunyemelea mkoa wa Arusha.

Alisema mahitaji ya fedha hizo ni kwa ajili ya nakisi ya Sh44.23 bilioni kwa ajili ya kukamilisha seti za jenereta 12 zitakazozalisha umeme wilaya za Kasulu, Loliondo, Kibondo na Sumbawanga, Sh161 bilioni kwa ajili ya mtambo wa kuzalisha megawati 100 utakaowekwa Ubungo na Sh107 bilioni kwa ajili ya mtambo unaotumia mafuta mazito utakaowekwa Mwanza, ukitegemewa kuzalisha megawati 60 za umeme.

"Tanesco inaomba angalau Sh312 bilioni katika kipindi cha mwaka 2009/10 kukamilisha miradi hiyo ya umeme wa dharura. Inashauriwa fedha hizi zipatikane kwa wakati ili kukamilisha jitihada hizi kubwa kabla ya mwishoni mwa Juni, 2010," inasema taarifa ya Dk Rashidi.

Mkurugenzi huyo wa Tanesco alikabidhi ombi hilo kimaandishi kwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, William Shelukindo, ambaye ni mbunge wa Bumbuli kwa tiketi ya CCM na kusihi Bunge liipigie debe ili serikali iridhie kuipa fedha hizo.

Akifafanua ombi ya shirika lake, Dk Rashidi alisema ombi siyo geni kwa serikali, akiwa na maana kwamba tayari alishaliwasilisha, lakini akasema utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua.

Hivyo, akaitaka Kamati ya Nishati na Madini iongeze nguvu ili serikali iidhinishe fedha hizo katika mwaka ujao wa fedha 2009/2010.

Alisisitiza serikali kupitisha fedha hizo mapema kwa sababu mchakato wa kununua mitambo hiyo mipya huchukua zaidi ya mwaka hadi kuwasili nchini na kuanza kufanya kazi.

Shelukindo alipokea ombi hilo lililokuwa kwenye karatasi yenye kurasa tatu na kuahidi kuwa kamati yake, italijadili na kuweka mikakati ya kuishinikiza serikali, ilitekeleze.

Kamati hiyo ilipokea ombi hilo wakati ikiwa njiani kwenda kutembelea kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 45 kilicho Tegeta wilayani Kinondoni.

Ombi hilo, Tanesco imeligawanya katika sehemu tatu ambazo zinahusisha ununuzi wa jenereta 17 kwa maeneo ambayo hayafikiwi na mtandao wa gridi ya taifa na mitambo miwili, mmoja kwa ajili ya kuzalisha umeme kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam na mwingine Mwanza kwa ajili ya Kanda ya Ziwa.

Kuhusu suala la jenereta 17, Dk Rashidi alisema kuwa bunge tayari liliidhinisha kwenye bajeti ya mwaka 2008/2009, lakini kiwango cha fedha kilichotolewa kilitosha kununua jenereta mbili tu ambazo zinatarajia kuanza kufanya kazi mkoani Kigoma kabla ya Juni, mwaka ujao.

Dk Rashidi alisema Tanesco inahitaji Sh44.23 bilioni kwa ajili ya kununua jenereta 12, ambazo zitagawanywa katika miji ya Loliondo, Kasulu, Kibondo na Sumbawanga.

Zabuni ya kununua jenereta hizo, alisema Dk Rashidi, ilitolewa kwa kampuni ya M/S Zwart Techniek Januari mwaka huu na ilikuwa ikamilishwe ndani ya miezi 15 kwa mkataba wa Sh59.5 bilioni.

Mradi wa pili kwenye ombi hilo ni wa kununua mtambo wa megawati 100 inaotumia gesi asilia, ambao utagharimu Sh161 bilioni.

Dk Rashidi alisema kuwa lengo la mtambo huo ni kukidhi mahitaji ya umeme katika kipindi cha mwaka 2009/2010.

Mradi wa tatu ni wa kununua mtambo wa megawati 60 unaotumia mafuta ambao utawekwa Mwanza na ambao utaigharimu serikali Sh107 bilioni.

Dk Rashidi alisisitiza kuwa mitambo ya umeme kwenye Kanda ya Ziwa tayari inaelemewa kutokana na mahitaji ya umeme kuzidi kwa asilimia 10 ya uwezo wake.

Kwa sababu hiyo, alisema tayari wameanza kutoa umeme kwa mgawo eneo hilo.

Lakini alisema mradi huo ni wa dharura tu kwa sababu Tanesco inatengeneza njia ya Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga na inatarajia utakamilika katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2010 hadi 2014.

Ombi hilo la Tanesco limekuja miezi michache baada ya vuta nikuvute iliyosababisha malumbano juu ya kununua ama kutonunua jenereta mbili za kuzalisha umeme wa dharura zinazomilikiwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilirithi zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond Development Limited LLC iliyoshinda zabuni hiyo kwa utata.

Hata hivyo, serikali ilifikia uamuzi wa kutonunua jenereta hizo zilizokuwa zinauzwa kwa Sh90 bilioni na zenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, badala yake ikaahidi kununua mpya.

Waliokuwa wanashawishi ununuzi wa jenereta hizo, walisema kuwa bado zipo katika hali nzuri, ni za bei nafuu na tayari zinafanya kazi badala ya kutumia muda mrefu kuziagiza hadi kuzifunga. Lakini Kamati ya Shelukindo ilisema Sheria ya Manunuzi ya Umeme inakataza serikali kununua vitu vilivyokwishatumika.
 
Mradi wa pili kwenye ombi hilo ni wa kununua mtambo wa megawati 100 inaotumia gesi asilia, ambao utagharimu Sh161 bilioni. huu ni wizi wa mchana
Dk Rashidi alisema kuwa lengo la mtambo huo ni kukidhi mahitaji ya umeme katika kipindi cha mwaka 2009/2010.

Mradi wa tatu ni wa kununua mtambo wa megawati 60 unaotumia mafuta ambao utawekwa Mwanza na ambao utaigharimu serikali Sh107 bilioni. huu ni wizi wa mchana

Dk Rashidi alisisitiza kuwa mitambo ya umeme kwenye Kanda ya Ziwa tayari inaelemewa kutokana na mahitaji ya umeme kuzidi kwa asilimia 10 ya uwezo wake.

Kwa sababu hiyo, alisema tayari wameanza kutoa umeme kwa mgawo eneo hilo.

Lakini alisema mradi huo ni wa dharura tu kwa sababu Tanesco inatengeneza njia ya Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga na inatarajia utakamilika katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2010 hadi 2014.

Ombi hilo la Tanesco limekuja miezi michache baada ya vuta nikuvute iliyosababisha malumbano juu ya kununua ama kutonunua jenereta mbili za kuzalisha umeme wa dharura zinazomilikiwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilirithi zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond Development Limited LLC iliyoshinda zabuni hiyo kwa utata.

Hata hivyo, serikali ilifikia uamuzi wa kutonunua jenereta hizo zilizokuwa zinauzwa kwa Sh90 bilioni na zenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, badala yake ikaahidi kununua mpya.

Waliokuwa wanashawishi ununuzi wa jenereta hizo, walisema kuwa bado zipo katika hali nzuri, ni za bei nafuu na tayari zinafanya kazi badala ya kutumia muda mrefu kuziagiza hadi kuzifunga. Lakini Kamati ya Shelukindo ilisema Sheria ya Manunuzi ya Umeme inakataza serikali kununua vitu vilivyokwishatumika.
==========================================
Rashid Utaendelea kuiba mpaka lini, au unatak pesa za CCM kwa ajili ya uchaguzi:

GE: 100MW (2 unit of LM 6000=50MW each 17 million) Equipment cost $35 Million for 100MW + $15-20 million engineering cost (Installation)=$50-55 million Why $160 million for 100MW.

If you do the manth ($55million for 100MW, and $105Million for CCM election campaign)

Rolls Royce: Trent 60=58MW=$20 Million x2 =$44million+engineering cost $15-20milllion=$59-64million for 100MW Why Rashid want to spend $160million for 100MW only.

Solar Turbine: 100MW= $40Million+ Engineering Cost $15-20million total $55-60million Why Rashidi want to spend $160 million

Pratt & Whitney Power Systems: 100MW= $40 Million+ Engineering cost $15-20million=$60million

Siemens Energy, Inc: 100MW= $42 Million+ Engineering cost $15-20million=$62million.

Kama kuna mtu anajua email za hao waeshimiwa (Sherukindo/ etc wapelekee hii information:
 
Akiwasilisha ombi hilo mbele ya kamati hiyo, jana, mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashidi alisema upungufu huo wa umeme tayari umesababisha kuanza kwa mgawo wa umeme kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na sasa tatizo hilo linaunyemelea mkoa wa Arusha.

Alisema mahitaji ya fedha hizo ni kwa ajili ya nakisi ya Sh44.23 bilioni kwa ajili ya kukamilisha seti za jenereta 12 zitakazozalisha umeme wilaya za Kasulu, Loliondo, Kibondo na Sumbawanga, Sh161 bilioni kwa ajili ya mtambo wa kuzalisha megawati 100 utakaowekwa Ubungo na Sh107 bilioni kwa ajili ya mtambo unaotumia mafuta mazito utakaowekwa Mwanza, ukitegemewa kuzalisha megawati 60 za umeme.

"Tanesco inaomba angalau Sh312 bilioni katika kipindi cha mwaka 2009/10 kukamilisha miradi hiyo ya umeme wa dharura. Inashauriwa fedha hizi zipatikane kwa wakati ili kukamilisha jitihada hizi kubwa kabla ya mwishoni mwa Juni, 2010," inasema taarifa ya Dk Rashidi.

Mkurugenzi huyo wa Tanesco alikabidhi ombi hilo kimaandishi kwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, William Shelukindo, ambaye ni mbunge wa Bumbuli kwa tiketi ya CCM na kusihi Bunge liipigie debe ili serikali iridhie kuipa fedha hizo.

.

Hapa bila shaka kuna mchongo wa pesa za uchaguzi za CCM mwakani. Lol, CCM hakika ni majangili. Halafu mbona wanakazania mitambo ya mafuta badala ya kuimarisha source za uhakiaka kama zile za kutumia makaa ya mawe? Wenzetu China, Marekani na Australia wana umeme wa uhakika kwa kutumia makaa ya mawe na uzalishaji wake ni wa bei rahisi. 54 % ya umeme wa Marekani unatokana na makaa ya mawe. Sisi TZ bado tunang'ang'ania mitambo ya mafuta. What kind of hopeless management we have from TANESCO to wizara ya Nishati. Shame on you Rashid.
 
==========================================
Rashid Utaendelea kuiba mpaka lini, au unatak pesa za CCM kwa ajili ya uchaguzi:

GE: 100MW (2 unit of LM 6000=50MW each 17 million) Equipment cost $35 Million for 100MW + $15-20 million engineering cost (Installation)=$50-55 million Why $160 million for 100MW.

If you do the manth ($55million for 100MW, and $105Million for CCM election campaign)

Rolls Royce: Trent 60=58MW=$20 Million x2 =$44million+engineering cost $15-20milllion=$59-64million for 100MW Why Rashid want to spend $160million for 100MW only.

Solar Turbine: 100MW= $40Million+ Engineering Cost $15-20million total $55-60million Why Rashidi want to spend $160 million

Pratt & Whitney Power Systems: 100MW= $40 Million+ Engineering cost $15-20million=$60million

Siemens Energy, Inc: 100MW= $42 Million+ Engineering cost $15-20million=$62million.

Kama kuna mtu anajua email za hao waeshimiwa (Sherukindo/ etc wapelekee hii information:

Ingia kwenye website ya Bunge utapata email zao.
 
Back
Top Bottom