NGARA ni Tanzania ama?


Hakumbuki INTERAHAMWE n.k huyo.
 
Sawa unachokisema ila jaribu kuangilia historia ya hizo nchi tulizopakana nazo ndio utajua kwanini hilo kundi la nyakanazi linawatu wengi kuliko kundi la tunduma au kwa kurahisisha kundi la nyakanazi watu wao wengi walihifadhiwa Tanzania kwenye makambi ya wakimbizi sasa sishangai sana hao watu kuwa wengi maeneo hayo huku kwetu
 
 

Nimekupata vilivyo mkuu wangu, shukran!
 
Kama sio watanzania wafukuzwe tu maneno mengi ya nini.Hawa ndo wanatuvurugia nchi

Serikali imelala pasipo kuiangalia Ngara, ilhali ne Tanzania, kwa matukio yake INASHANGAZA
 
Jana nikiwa hospital ya Murgwanza (mjini Ngara) majira ya saa sita mchana, aililetwa majeruhi aliyechomwa mkuki mbavuni na kutoboa mapafu huku mkuki huo ukihusa moyo

Aliletwa hospital huku akiwa mahututi japo alifaulu kuhojiwa na Radio Kwizera na kujieleza kwa ufupi, wanaodaiwa kumchoma mkuki ni wananchi wa Ng'ambo ya Tanzania japokuwa mkazi huyo alikuwa akiishi Kabanga kijiji cha Nzaza,

Mahututi huyo alipewa referal kwenda Bugando huku akiwa ametundikwa Oxygen, alisafirishwa kwa ambulance na walipofika tu Mizani akakata roho majeruhi huyo ambaye alikuwa ni kijana wa miaka 25 tu

Kuna kila sampuli ya matukio tena huwezi kuamini kama ni binaadam, yaani wilaya hii inatisha kwa uharamia

Je, serikali kweli inaitazama Ngara kwa ukaribu?
 
hebu dadavua kidogo kaka...wako so natural and black sijui wanapaka nini wakiwa watoto...

Hali ya hewa inaruhusu, hakuna JOTO Ngara na ipo juu sana kutoka usawa wa Bahari
 

Tamaduni za kitanzania ni zipi? Tanzania ina makabila zaidi ya 120, na kila kabila lina tamaduni zake. Isitoshe, wilaya zilizotelekezwa ni nyingi sana ndugu yangu. Sio ngara peke yake. Nenda msimbati (eneo inapotoka gesi huko mtwara) ukajionee.
 
Hii reaction ya watu humu ndani inanipa wasiwasi,kuna uwezekano watu wameguswa maslahi yao kupitia uzi huu!Ukweli ndo huo wanyaru na warundi wanajimegea ardhi kwa wilaya za Biharamulo,Ngara na Karagwe kama hawana akili nzuri.Serikali imelala fofofo!!

Ni kweli kabisa kwa usemacho mkuu,
Pale Rulenge walikuja wanyarwanda wanaoishi USA na wamenunua ardhi kubwa kwa ajili ya kujenga University wilayani Ngara, ni eneo la jirani ya eneo zitakapokutana reli (inayotarajiwa kujengwa) kwenda Rwanda/Burundi, jamaa wameshanunua ardhi ya vijiji hivyo pasipo kusita kabisa, naamini itawafaidisha zaidi siku chache za usoni
 
We Mzito Kabwela acha dharau,kama umekosa la kuongea bora unyamaze,umetongoza wangapi ukaona kuwa hawakatai?basi unawapenda,wewe kama unaona ni wepesi unawafuata wa nini?wewe ndy hufai,kama umekosa la kuchangia acha tu ndg yangu
teh teh teh teh Umugore wanjye punguza munkari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…