Ninapoongelea juu ya Ngara sijakurupuka, tembea iwe ni Nyakanazi, Lusahunga, Ngara mjini yenyewe, Rulenge, Rusumo na hata Kabanga sehemu hizo za wilaya hii si sawa na maeneo mengine ya mipakani mwa nchi hii kama ilivyo Tunduma, Namanga, Sirari, Mbamba bay, Mutukula etc
Sasa nipo Ngara, najionea hali ilivyo, kumesheheni wanyarwanda kuliko warundi, vitendo vya kiharamia vimesheheni, huwezi kuendesha gari yako private baada ya saa mbili usiku hata uwepo Ngara mjini, mgeni anajulikana kwa aina ya kiswahili
Ni aghalabu kukuta watu wakiongea kiswahili, hakuna FM radio zaidi ya radio za kinyarwanda tena wakilonga kinyarwanda na ndizo zinazosikika, ipo radio KWIZERA ambayo pia baadhi ya nyakati ilidiriki kutumia kilugha badala ya kiswahili katika utangazaji wake
Ninachoamini, ni eneo ambalo limetelekezwa kiujumla ndio maana hata matukio mengi ya uharamia yamesheheni katika mapori mazito na milima mirefu inayoizunguka wilaya hii ya Ngara
Kwa yeyote, na aitembelee wilaya hiyo ajionee