NGARA ni Tanzania ama?

NGARA ni Tanzania ama?

Tamaduni za watanzania hutofautiana kabila na kabila. Sasa unaposema hakuna tamaduni za tanzania mi sikuelewi. Kumbuka mipaka waliweka wzungu kwa kalamu tu na hivyo makabila yote ya mpakani yana mahusiano sehemu zote mbili za nchi husika. Tamaduni za Tanzania ni kama nembo za taifa basi... Kwani hujakuta bendera za taifa nk?
 
mulusagamba,muvididili.milamila,k9,lwekubu,kabanga,mutendeli,rusumo,kanaz,kote wamejaa wanyarwada na warundi wanaoitwa wahangaza .rujea ule uzi wa uliosema kagame anaingiza watu wake tz.
 
Wacha upuuzi wako. Kama huna habari ya kweli ni vyema kunyamaza. Sehemu zote unazozitaja hata huzitaji sawasawa. Ngara ni Tanzania na wahangaza sio watusi ni wahangaza. Wana clans nne na lugha yao ni moja, kihangaza ambacho hushabihiana sana na kirundi, kinyarwanda , kiha na kisubi.
 
Tamaduni za watanzania hutofautiana kabila na kabila. Sasa unaposema hakuna tamaduni za tanzania mi sikuelewi. Kumbuka mipaka waliweka wzungu kwa kalamu tu na hivyo makabila yote ya mpakani yana mahusiano sehemu zote mbili za nchi husika. Tamaduni za Tanzania ni kama nembo za taifa basi... Kwani hujakuta bendera za taifa nk?

Basi kama ingelikuwa sio dermacation za wazungu, Ngara kiuhalisia ingelikwenda Burundi. Full stop!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kwani dar kuna kabila lipi? kama siyo watusi,wajhutu,watusi nk
 
mulusagamba,muvididili.milamila,k9,lwekubu,kabanga,mutendeli,rusumo,kanaz,kote wamejaa wanyarwada na warundi wanaoitwa wahangaza .rujea ule uzi wa uliosema kagame anaingiza watu wake tz.

Acha upuuzi, dont be a simple minded person, Hiv unajua maneno kama haya ni hatari sana! yaani wewe leo unataka kutuambia kwamba Wahangaza ndani ya taifa hili ni Wanyarwanda au Warundi? Nina mashaka na uwezo wako japo unajua kuchezea keyboard! Na ukitoka Ngara utakwenda Mwambao mwa ziwa Nyasa utasema Wanyasa sio Watanzania ni wamalawi baadaye utasema wengine, kwa nini sasa tunaongea hivi?
 
Wacha upuuzi wako. Kama huna habari ya kweli ni vyema kunyamaza. Sehemu zote unazozitaja hata huzitaji sawasawa. Ngara ni Tanzania na wahangaza sio watusi ni wahangaza. Wana clans nne na lugha yao ni moja, kihangaza ambacho hushabihiana sana na kirundi, kinyarwanda , kiha na kisubi.[/Q

safi!
 
Ngara inatokana na mti mababu zetu wakina BARAMBA walipo kuwa wanafanyia mikutano upo pale halmashauri unaitwa igiti cha ngara ndo wakapata jina la wilaya ya ngara. wenyeji wa ngara ni wahangaza wanaoongea kihangaza na washubi wanao ongea kishubi. ngara ina mchanganyiko wa wahaya, wanyambo na wasubi na waha pia. lugha za watu wa ngara na rwanda, burundi hazitofautiani sana coz hata mipaka ni bikon tu!. mi nimefika hadi kwa akina rutihinda.
utazi umuhangaza amuhanga amaso. mia
 
mbona povu jingi narudia maeneo niliyo yataja yapo ngara ila kama hujaelewa maana yangu ipo hv kuwa kanda ya ziwa hasa ngara kumekuwa na muingiliano mkubwa wa wagen hata baada ya kufunga kambi za rukore a na b. ngara ni tz ila kichaka cha wagen haram
 
Ninapoongelea juu ya Ngara sijakurupuka, tembea iwe ni Nyakanazi, Lusahunga, Ngara mjini yenyewe, Rulenge, Rusumo na hata Kabanga sehemu hizo za wilaya hii si sawa na maeneo mengine ya mipakani mwa nchi hii kama ilivyo Tunduma, Namanga, Sirari, Mbamba bay, Mutukula etc
Sasa nipo Ngara, najionea hali ilivyo, kumesheheni wanyarwanda kuliko warundi, vitendo vya kiharamia vimesheheni, huwezi kuendesha gari yako private baada ya saa mbili usiku hata uwepo Ngara mjini, mgeni anajulikana kwa aina ya kiswahili

Ni aghalabu kukuta watu wakiongea kiswahili, hakuna FM radio zaidi ya radio za kinyarwanda tena wakilonga kinyarwanda na ndizo zinazosikika, ipo radio KWIZERA ambayo pia baadhi ya nyakati ilidiriki kutumia kilugha badala ya kiswahili katika utangazaji wake

Ninachoamini, ni eneo ambalo limetelekezwa kiujumla ndio maana hata matukio mengi ya uharamia yamesheheni katika mapori mazito na milima mirefu inayoizunguka wilaya hii ya Ngara

Kwa yeyote, na aitembelee wilaya hiyo ajionee
 
Wadau,
Tuache masikhara ya kijiografia na tujikite kiuhalisia, wilaya ya NGARA ni Tanzania ama?
Kama ni Tanzania, basi imetelekezwa na warundi/wanyarwanda wamejiotea mizizi na himaya zao,, amini usiamini hakuna tamaduni za kitanzania katika wilaya hiyo, tembelea ujionee

Kama wewe muhutu kazi kwako ,tuondolee ukabila wako hapa
 
Wadau,
Tuache masikhara ya kijiografia na tujikite kiuhalisia, wilaya ya NGARA ni Tanzania ama?
Kama ni Tanzania, basi imetelekezwa na warundi/wanyarwanda wamejiotea mizizi na himaya zao,, amini usiamini hakuna tamaduni za kitanzania katika wilaya hiyo, tembelea ujionee

Tamaduni za Tanzania ni zipi na zilizopo wilaya hiyo ambazo si za Tanzania ni zipi?
 
Back
Top Bottom