News updates: UDSM kwawaka moto muda huu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kuna vurugu kubwa katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hasa Mdigree(karibu na jengo la Utawala) hapa UD ambapo wanafunzi wanashinikiza kuachiwa mara moja kwa wenzao walio mahabusu.Wameapa kutositisha mgomo hadi kieleweke.CHADEMA walivyo na damu ya kunguni,watatwishwa na zigo hili...
 
Najiuliza swala mmoja kama police walienda maeneo ya chuo na kukamata watu ovyo vipi walewaliyokuwa busy na mambo yao na kukamatwa kama waandamanaji? hapa hakuna usawa.Nawaunga mkono 100%
 
Andaeni mabomu ya machozi na nyie muwarushie kwanza nilipita juzi nikakuta kokoto nyingi sana hapo mdigrii okoteni hizo ni silaha tosha, wapuuzi kweli hawa kama hao wenzao huko bungeni
 
safi sana, hakuna shule mpaka kieleweke. heri chuo kifungwe kuliko kusoma wenzenu wakiendelea kusota ndani na bila mikopo. Juzi nilicheka sana eti Mkandala anadai chuo kinawapelekea chai na chakula, dhamana na wakili wa kuwatetea wanafunzi waliowekwa rumande. Hivi hii kitu ni kweli au ndo ilikuwa gia ya kuwapooza wanafunzi wasigome?

Duniani kuna mambo, ila haya yatokeayo Tz ni zaidi, mweeeeeeeee!
 
Kuna vurugu kubwa katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hasa Mdigree(karibu na jengo la Utawala) hapa UD ambapo wanafunzi wanashinikiza kuachiwa mara moja kwa wenzao walio mahabusu.Wameapa kutositisha mgomo hadi kieleweke.CHADEMA walivyo na damu ya kunguni,watatwishwa na zigo hili...

Viongozi walivyo vilaza utakuta wanahusisha CDM
Si msikilize kilio chao wanafunzi na mtatue
 
Hivi Chadema ndio chama cha serikali ya wanafunzi? Sielewi kwanini wanahusishwa na vurugu za wana chuo.

Shemeji kwema huko lakini? Usisahau kuwa kwa watu wenye akili finyu, kwao kila jambo litokanalo na ubaya wao, ni lazima walitafutie mchawi. Lakini usisahau pia kwamba 'msiba wa masikini haukosi mchawi'.
 
Kuna vurugu kubwa katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hasa Mdigree(karibu na jengo la Utawala) hapa UD ambapo wanafunzi wanashinikiza kuachiwa mara moja kwa wenzao walio mahabusu.Wameapa kutositisha mgomo hadi kieleweke.CHADEMA walivyo na damu ya kunguni,watatwishwa na zigo hili...[/QUOT

Hivi yule Prof Palamagamba Kabudi na Dr Bana hawapo hapo karibu mkawashughulikia on my behalf? Maana hawa jamaa wananikera kwa kufanya kazi za magamba wazi wazi..
 
Mukandala kama JK.Husema linalomjia kinywani.Huamini hata asichothibitishiwa.Wanafunzi wamepamba moto hapa kwakweli.Nipo hapa Kijamii Forums zaidi..Ona sasa,jamani naombeni maji ya kunawa...
 
Mukandala kama JK.Husema linalomjia kinywani.Huamini hata asichothibitishiwa.Wanafunzi wamepamba moto hapa kwakweli.Nipo hapa Kijamii Forums zaidi..Ona sasa,jamani naombeni maji ya kunawa...
Duh!
Hii kali, haya ukishamaliza kunawa leta habari mkuu...
 
Pambaneni mpaka mwisho mkiwakomboa wapiganaji wenzenu,Taifa linawategemea katika kudai haki na utu wa mwanadamu,ni heri uishi ukija kufa wengine waishi vizuri.Kuliko kuishi maisha mazuri na ya anasa wakati wengine wanaishi kimaskini.Nawatia nguvu pambaneni mpaka mwisho.
 
Wanafunzi wanasisitiza lazima washinde mechi hii.Kwakuwa mgomo huu ulianza jana,ukiendelea na kesho Chuo kitafungwa.Hiyo ndo sheria.Hasira zinazoonyeshwa na wanafunzi hapa ni zaidi ya zile za Wazanzibar waliochana Muswada wa Katiba.DARUSO wamepotezwa kabisa na wanaharakati.Angalia sasa,jamani muda kidogo...
 
Viongozi wa nchi wapumbavu sana!, do once walikuwa wanang'ng'ania kuilipa kwa sababu tu wanamaslai yao. ila kutoa pesa za mikopo kwa watoto wa wenzao ili wasome wanasema serikali haina hela, hzo za kuwalipa do once wanazipata wapi? tatizo viongozi nchi hii wanataka wao na familia zao ndy waelimike na wao na watoto zao ndy waendelee kuitawala nchi hii wasiwepo wengine. lazima haki ipatikane na muda c mrefu tutaingia mtaani, hata nchi za africa ya kaskani hadi mashariki ya kati kulikuwa na ujinga unaofanana na huuu!!!!!!!!! saa yaja kaeni tayari kwa ukombozi wa nchi yetu yenye neema tuliyopewa na mungu... UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UZAIFU.
 
Acheni sheria ichukue mkondo wake. Acheni kuchanganya sheria na siasa.

Polisi wana kosa gani kuwakamata wahalifu. Wanaoandamana hovyo bila sababu ya msingi. Polisi wana wajibu wa kulinda usalama wa raia. Lazma iwashughulikie wote wanaojaribu kuhatarisha usalama wa watu wengine na nchi kwa ujumla.

Polisi hawajawavamia ktk vyumba vyao na kuwakamata. Walikuwa wanafanya uhalifu.

Nyie tulieni msome, acheni kutumiwa na wanasiasa uchwara.
 
Tuwekee na picha mkuu kama unaweza! cha msingi hiki chuo kinanikera sana kuamua kila kitu kisiasa, they have to know their roles as university.
 
Acheni sheria ichukue mkondo wake. Acheni kuchanganya sheria na siasa.

Polisi wana kosa gani kuwakamata wahalifu. Wanaoandamana hovyo bila sababu ya msingi. Polisi wana wajibu wa kulinda usalama wa raia. Lazma iwashughulikie wote wanaojaribu kuhatarisha usalama wa watu wengine na nchi kwa ujumla.

Polisi hawajawavamia ktk vyumba vyao na kuwakamata. Walikuwa wanafanya uhalifu.

Nyie tulieni msome, acheni kutumiwa na wanasiasa uchwara.

Wewe kweli ni Mzee
 
Back
Top Bottom