Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
Mkuu wa Idara ya Marekani na Ulaya kwenye Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Radhia Msuya ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Uingereza akichukua nafasi ya Balozi wa sasa ambaye atapangiwa kazi nyingine Ikulu.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu Jijini Dar, Balozi Msuya ambaye kabla ya nafasi yake ya sasa alikuwa kwenye ubalozi huo wa Uingereza amekuwa akifanya kazi nzuri ambayo inasemekana ilichangia sana katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani nchini karibu mwezi mmoja zaidi uliopita.
"Balozi Radhia amekuwa akifanya kazi nzuri na Rais ameonelea kuwa wakati umefika kwa Bi. Msuya kubeba jukumu hilo zito" Alisema ofisa mmoja wa Ikulu ambaye alikataa kutaja jina lake.
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kumpata Balozi Radhia mapema asubuhi ya leo msaidizi wake amesema kuwa Balozi Msuya amepokea taarifa za kuteuliwa kwake kwa mshtuko mkubwa lakini pia kwa unyenyekevu na hivi sasa anajaribu kuanza mipango ya kurudi Uingereza kuanza jukumu lake hilo jipya.
Muda mfupi uliopita Balozi Msuya ametuma taarifa kwa vyombo vya habari akikiri kuwa kuteuliwa kwake ni imani kubwa ya Rais Kikwete kwake na yuko tayari kufanya kazi yake kwa uadilifu akiwatumikia Watanzania wote bila kujali asili zao, dini, au makabila.
KLHN inampa pongezi za dhati Balozi Radhia kwa uteuzi wake huo mpya.