Chewale
Senior Member
- Jul 1, 2016
- 131
- 285
Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki amesema kuanzia jana kuna ujumbe mfupi wa video uliozunguka katika mitandao ya kijamii uliorekodiwa na Raia wa Uingereza mwenye asili ya Tanzania Martina Farrall, akielezea maisha yake kuwa hatarini huko anapoishi Ireland ya Kaskazini.
Kwenye taarifa aliyoitoa leo August 06,2024 Balozi Kairuki amesema kufuatia ujumbe huo, Ubalozi umewasilisha taarifa ya Martina kwa Mamlaka za Uingereza na kuomba hatua za kufuatilia suala hilo zichukuliwe mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha usalama wake sambamba na kufanyia kazi shutuma alizotoa ili kubaini ukweli wa shutuma hizo na hatua kuchukuliwa.
“Aidha, leo tarehe 6 Agosti 2024 Afisa Ubalozi wa Tanzania anakwenda Ireland ya Kaskazini katika Mji anapoishi Bi. Farrall ili kukutana na Mamlaka zinazohusika kufuatilia suala hilo”
Anatishia kumuua kwa kumpa vitisho na unyanyasaji.