Nenda Lugola, Bodaboda watakukumbuka

Nenda Lugola, Bodaboda watakukumbuka

Tutamkumbuka kwa yale mauno aliyokata siku ile
Hata hivyo naweza kusema ,Mh.Rais alichelewa kumuondoa huyu jamaa, kwasababu hana utendaji zaidi ya porojo tu!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
nadhani askari wamefanya sherehe zaidi ,hata hivyo maisha ni yin na yang kuna usiku na mchana ,uzuri na ubaya ,weusi na weupe NK acha maisha yaendelee
 
Hakuna zuri hata moja alilofanya? Au tunasibiri hadi afe ndo tuseme?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna aliyoyafanya ambayo ni mazuri. Kwanza ni lile la kuruhusu mabasi yasafiri masaa 24. Nakumbuka sana ile kauli yake ya kwanini majambazi wawapangie wananchi muda wa kusafiri wakati jeshi la Polisi lipo.

Lingine ni kuzuia Polisi wasikamate bodaboda na kuzirundika vituo vya Polisi bila sababu ya maana. Ila kwa hili naona alizidiwa nguvu na Polisi na utekelezaji wake ulikuwa mdogo kwa kuwa Polisi wako "above the law"!

Ukimlinganisha Mheshimiwa Lugola na yule mnyiramba mvaa skafu, Lugola anastahili kuitwa mwenyeheri!
 
Cliffhanger, Mengi mazuri tu pia kuhusu watu kulazwa selo kisa ni wikiend, alisema hata kama ni wikiend mtu atolewe kwani mbona wanaingizwa ndani wikiend

Pia kwenye faini za barabarani alipiga marufuku trafiki anakutozzo faini kwa kila kitu kibovu kwenye gari mfano taa mbovu faini, tairi zina upara faini, kioo kimepasuka faini

Pia upigaji wa tochi wa kuvizia

Sema alikumbana na upinzani mkubwa sana kwa polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya Lugola kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani bodaboda walikuwa wananyanyaswa sana na askari, kila askari aliyekuwa ana shida na pesa alikuwa anazitafutia kwa bodaboda, lakini Lugola alidhibiti hali hii na huenda ikawa sababu ya kuchukiwa na askari polisi maana alikata mirija yao.

Leo nimeshuhudia tena polisi wakianza kukamata pikipiki tena kwa kuwafukuza waendesha bodaboda kwenye vijiwe ni dhahiri kuwa pikipiki zinaenda kujazana tena kwenye vituo vya polisi, lakini ajali nyingi za bodaboda zinasababishwa na kufukuzwa na askari polisi.

Wito kwa waziri mpya azuie hili la polisi kuwafanya bodaboda mitaji zuio la Lugola liendelee kufanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom