Full 8
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 313
- 272
Duniani kila kitu kina pande mbili, wema na ubaya, mbele na nyuma bila kusahau juu na chini.
Siko hapa kuongelea mabaya ya Kangi Lugola maana atayaongelea mwingine. Mimi naongelea jambo moja tu ambalo ni miongoni mwa mazuri mengi aliyoyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Bodaboda wasinyanyaswe, bodaboda kama haijahusika kwenye jinai isikae kituoni n.k.
Ni wazi kuwa katika kipindi cha Kangi, bodboda wamepata nafuu sana. Uonevu wa kukamatwa na askari wa barabarani ulipungua sana.
Pia, bodaboda walifanya kazi zao kwa uhuru mkubwa n kupata faida mara kutokana na kutotoa rushwa na faini za kubambikiwa kwa askari wa barabarani.
Lakini pia bodaboda waliweza kufanya kazi kwa uhuru na amani kwani walisajiliwa, wakapewa mafunzo na leseni za udereva. Mafunzo haya yamechangia kwa kiasi fulani kupunguza ajali barabarani.
Naimani waziri ajaye atafanikisha pendekezo la wadau la kuwa na faini tofauti kati ya dereva wa gari na bodaboda hasa ukizingatia vipato havilingani na zaidi lengo la adhabu ni kufunza. Hivyo, kuhekimisha madereva wa bodaboda kutasaidia sana kupunguza ajali kuliko kuwaadhibu kwa faini kubwa.
Ni hayo tu.
Sent using Jamii Forums mobile app