NECTA yatoa ufafanuzi kuhusu mjadala wa ufaulu kati ya shule ya Wasichana ya Anwarite na ya Wavulana ya Feza

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
5,304
14,913
Wakuu Sina la kusema Sana nitaatach maswal ya MALISA ambayo amewauliza NECTA

Kama haitofunguka

Anauliza shule ya SEKONDARI ANWARITE ina watoto 76 wote wamepata daraja la 1 na imekuwa ya 11 kitaifa

Lakn sule ya SEKONDARI FEZA WAVULANA ina watoto 62 lakn 59 wamepata daraja la 1 na 2 daraja la 2 na 1 daraja la 3 imekuwa ya 7 kitaifa

Sasa upangaji huu umetumia vigezo gani

Attachment ipo chini


Screenshot_20220123-133255.jpg

--

UPDATE:

MAJIBU KUTOKA NECTA

FB_IMG_1642956100591.jpg
 
Wakuu Sina la kusema Sana nitaatach maswal ya MALISA ambayo amewauliza NECTA

Kama haitofunguka

Anauliza shule ya SEKONDARI ANWARITE ina watoto 76 wote wamepata daraja la 1 na imekuwa ya 11 kitaifa

Lakn sule ya SEKONDARI FEZA WAVULANA ina watoto 62 lakn 59 wamepata daraja la 1 na 2 daraja la 2 na 1 daraja la 3 imekuwa ya 7 kitaifa

Sasa upangaji huu umetumia vigezo gani

Attachment ipo chiniView attachment 2092625

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hiyo shule inamilikiwa na wahalifu wa nchini Uturuki.kwahiyo mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
 
Simple Statistics. Kama shule 2 A, B zina wanafunzi wa 2 kila moja mfano. Shule ya kwanza matokeo div 1 za 9. Hii ina wastani wa 9. Shule ya pili. Div 1 moja ya 7 na div 2 ya 10. Hii ina wastani wa 8.5.
Kwa hio shule B inaongeza kuliko shule A.
 
Maswali nengine ya kijinga mfano A inaanzia 81

Mtoto wa Feza kapata A ya 95 wa Marian kapata A ya 92

Wa Anwarite kapata A ya 90

Ukiambiwa wa kwanza in yupi wa pili ni yupi na wa tatu in yupi hujui?

A's hizo hazifanani kwa marks !!!/jibu rahisi tu hata wote wawe division one

swali la kijinga hilo alilouliza wala halihitaji jibu la NECTA angeuliza hata. Mwalimu wa chekechea angemjibu
 
Maswali nengine ya kijinga mfano A inaanzia 81

Mtoto was Feza kapata A ya 95 wa Marian kapata A ya 92

Wa Anwarite kapata A ya 90

Ukiambiwa wa kwanza in yupi wa pili ni yupi na wa tatu in yupi hujui?

A's hizo hazifanani kwa marks !!!/jibu rahisi tu hata wote wawe division one

swali la kijinga hilo alilouliza wala halihitaji jibu la NECTA angeuliza hata. Mwalimu wa chekechea angemjibu
Unauhakika na jibu lako? Maana naona kwa hasira unawaita wenzio wajinga, wakati alitaka kufamu.
 
Ndio nina uhakika A hazifanani kwa marks tatizo swali dogo mtu anataka NECTA wajibu
Okay. Nilijua thamani ya A inaangaliwa katika kupata wanafunzi 10 bora. Kwahiyo pamoja na kuwa na div 2. na 3 bado kwenye average Feza akabaki juu.
 
Elimu kutumika kisiasa ni jambo la hatari sana maana nchi itazalisha vilaza wa bora liende.Kinachonisikitisha zaidi TZ inamalengo ya kuwa Taifa la viwanda sasa unabaki unajiuliza kwa mfumo huu wa elimu hivyo viwanda si vitaongozwa na wageni wenye ujuzi huku wazawa wakibaki manamba?

Serikali kwa kiu yake ya kutaka kuaminika kua ubora wa elimu umekua na ufauru umeongezeka imejikuta ikifuta adhabu ya penati kwa waliopata F somo la hesabu, awali ilikua kwamba mwanafunzi akiwa na cutpoints zinazomruhusu apate aidha div 1 au 2 lakini akapata F ya somo la Hesabu au uraia basi moja kwa moja atapigwa penati na matokeo yake yatakua sio 1 au 2 bali div 3..Umeona sasa wataka sifa walivyo! Ufaulu wa kidato cha nne 2021umeongezeka kwa kiwango cha kutisha huku one na two ikiwa si kitu tena(thaman ya ufaulu kwisha habari yake) maana wapo waliotakiwa kuwa na div 3 yani wana F ya hesabu ila serikali ilipeta kuongeza idadi ya ufaulu.

Hayo si maajabu maajabu zaidi ni kuwa vijana wanaosoma special wale wenye ufaulu mkubwa sana na vijana wanaosoma shule za Kishua kwa mazingira na ufundishaji kama Feza, St Francis, KEMOBOS nk eti wanapimwa kwa mtihani sawa wa Taifa na kijana anayesoma Nyanembe Sekondari ya kata ambayo picha linaanza shule waalimu hawatoshi kuanzia form 1 hadi four mwalimu wa hesabu na fizikia yupo mmoja shule nzima, darasa moja linawanafunzi zaidi ya 100, madarasa hayaleweki umeme hakuna, maji kilomita buku mwanafunzi ambaye lazima atembee zaidi ya KM 5 kutoka anapokaa hadi shule ndo apate elimu, mwanafunzi huyu hana cha library wala huduma ya Internet desa pekee analotegemea atoboe nalo nekta ni kutoka kwa mwalimu shija ambaye naye mda mrefu anashinda Town akipiga madili ya tuition kweli kabisa mnawapima kwa viwango sawa hawa wanafunzi? Hii ni aibu


Ajabu la ziada elimu hii ni huu uhuni wa kupanga matokeo usioleweka lengo tu ionekane ufaulu umeongezeka tuangalie mfano mdogo hapa Shule Ya ANAWARITE GIRLS ina Wanafunzi 76 Na Wote Wamepata Division 1, Alafu Imekua Shule Ya 11 Kitaifa, Wakati Huohuo FEZA BOYS Yenye Wanafunzi 62 Na Inayo Division 1, 2 Hadi 3 Lakini Imekua Shule Ya 7 Kitaifa(Credit Malisa G) .Hapa unajiuliza Wataalamu Walitumia Vigezo Gani Kuzi Rank Hizi Shule? Wamenunuliwa, bahati mbaya au shida ya kimfumo.

Wanasiasa msitumie elimu kujinufaisha mnaua msingi wa Taifa la kesho

20220123_141818.jpg


Screenshot_20220123-161257_Samsung Internet.jpg


Screenshot_20220123-161216_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom