Wanafunzi 4,224 pekee wachaguliwa Shule za Bweni Kidato cha Kwanza kati ya 50,475 wanaostahili

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,375
8,114
Uchache wa Shule za Bweni nchini umesababisha Wanafunzi 46,251 kukosa nafasi ya kujiunga na Shule zenye huduma hiyo Nchini

Idadi ya Shule za Serikali zinazochukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mwaka 2023 ni 4,307 ambapo Shule za Kutwa ni 4269 na Bweni ni 38 zenye uwezo wa kupokea Wanafunzi 4,224 tu.

====================

Ofisi ya Rais (TAMISEMI), imefafanua suala la wanafunzi 4,224 waliochaguliwa kidato cha kwanza kwenda katika shule za bweni, ikisema kuna vigezo vya wazi vinavyotumika katika kuwachagua wanafunzi hao.

Ufafanuzi huo ulitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI (Elimu), Dk Charles Msonde akisema sababu nyingine za wanafunzi 4,224 kwenda katika shule hizo ni pamoja na ufinyu wa shule za bweni zilizopo.

Hivi karibuni yameibuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya wazazi kuwa utaratibu uliotumika si wa uwazi na umewanyima fursa watoto kukaa bweni.

Baadhi ya wazazi walisema wangependa watoto wao wachaguliwe katika shule hizo hasa kutokana na kufauli vizuri.

Katika ufafanuzi wake jana, Dk Msonde alisema wanafunzi waliofaulu na kuwa na sifa ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 1,073,941 na kati ya hao waliochaguliwa shule za bweni ni 4,224, sawa na asilimia 0.39 ya wanafunzi wote waliochaguliwa.

Alisema idadi ya shule za sekondari za Serikali zinazochukua wanafunzi wa kidato cha kwanza ni 4,307 na kati ya hizo, shule za kutwa 4,269 na bweni ni 38 zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 4,224.

“Kutokana na idadi ndogo ya shule za bweni tulizonazo na ili watoto wakae darasani vizuri, kulala katika bweni kwa mujibu wa mwongozo, shule hizo 38 zina uwezo wa kupokea wanafunzi 4,224,” alisema.

Kuhusu namna ya kuwapata wanafunzi kujiunga na shule za bweni, Dk Msonde alisema mchakato huo umekuwa ukizingatia vigezo mbalimbali, ikiwemo kuzingatia viwango vya ufaulu.

“Wale wenye viwango vya juu ndio waliochaguliwa, lakini hata hivyo waliofaulu kwa viwango vya juu pia ni wengi, hivyo mfumo ulitumika kuchagua wale waliofaulu zaidi ya wenzao.

“Hapa tunasema waliochaguliwa kwenda bweni wamepata daraja la kwanza A, lakini ukiangalia waliopata daraja hilo wapo wanafunzi 50,475, hivyo hata kwenye daraja hili la kwanza ipo kanuni iliyotumika ya kugawa nafasi za wanafunzi waliofaulu vizuri,” alisema.

Hata hivyo, Dk Msonde alisema shule za bweni zimegawanyika katika makundi matatu, ambayo ni lile lenye ufaulu wa juu, kundi la pili ni shule za bweni za ufundi na kundi la tatu shule za bweni kawaida.

Dk Msonde alisema kwa upande wa shule zenye ufaulu wa juu ziko saba, zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 932 ambao ndio waliopangiwa.

Kwa upande wa shule za bweni kawaida, Dk Msonde alisema kanuni yake ni uwiano wa watahiniwa wote wa darasa la saba katika shule za vijijini au mazingira magumu katika Halmashauri mara idadi ya nafasi zote za bweni kwa wavulana na wasichana wa vijijini au mazingira magumu Tanzania bara.

MWANANCHI
 
Ujinga tu darasa la saba 2007 mwenzangu alipata 194/250 na mimi nilipata 216/250 then shule me napelekwa shule ya kata jamaa kaenda mzumbe...kisa shule yake ipo ilala vijijini ambapo mpaka ni kuvuka reli lakini tunaishi mtaa mmoja.
 
Makando kando ni mengi
 
Hili ni janga la kitaifa. Elimu itazidi kuporomoka na kiwango cha wajinga na wasiojua KKK wataongezeka. Hawo wote sasa itabidi wakarundikwe kwenye shule za kata (makaburi ya kuzikia elimu ya watanzania).
 
Ujinga tu darasa la saba 2007 mwenzangu alipata 194/250 na mimi nilipata 216/250 then shule me napelekwa shule ya kata jamaa kaenda mzumbe...kisa shule yake ipo ilala vijijini ambapo mpaka ni kuvuka reli lakini tunaishi mtaa mmoja.
oyaaa Huwezi pelekwa Mzumbe kwa wastani huo..hii uwongo uwongo..nimesoma msumbe form 1 hadi 6 pale..!! pale wanaenda watu hadi wana 250/250
 
Back
Top Bottom