NECTA yatangaza Matokeo ya Kidato cha 6 mwaka 2022

Chief_mataka

Member
Jan 27, 2022
97
92
Watahiniwa 93,136 (98.97%) wamefaulu Mitihani yao, ikielezwa Wasichana ni 40,907 na Wavulana ni 52,229. Aidha, Baraza la Mitihani (NECTA) limesema jumla ya Watahiniwa 83,877 (99.24%) wamefaulu katika Daraja 1 hadi 3

Ufaulu katika Masomo ya Historia, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Physics, Chemistry, Biology, Kilimo, Advanced Mathematics, Economics, Accountancy na Food/HumanNutrition umepanda ikilinganishwa na mwaka 2021

Hata hivyo, NECTA imesema Ufaulu wa Masomo mengine yakiwemo General Studies, Geography na Basic Applied Mathematics (BAM) umeshuka

=======
SHULE 10 BORA

10. Ziba, Tabora - Serikali
9. Mkindi, Tanga - Serikali
8. Mzumbe, Morogoro - Serikali
7. Nyaishozi, Kagera - Binafsi
6. Dareda, Manyara - Serikali
5. Ahmes, Pwani - binafsi
4. Tabora Girls - Serikali
3. Tabora Boys - Serikali
2. Kisimiri, Arusha - Serikali
1. Kemebos, Kagera - Binafsi

10 BORA KIDATO CHA 6 MASOMO YA SAYANSI

1: Catherine Mwakasege,- St.Mary's Mazinde Juu
2: Lucy Magashi - St.Mary's Mazinde Juu
3: Muhewa Kamando - Tabora Boys
4: Minael Mgonja - St.Mary's Mazinde Juu
5: Norah Eliaza - St.Mary's Mazinde Juu
6: Jenifer Chuwa- St.Mary's Mazinde Juu
7: Pauline Mabamba- St.Mary's Mazinde Juu
8: Rachel Joachim- St.Mary's Mazinde Juu
9: Kulwa Elias - Tabora Boys
10: Oscar Eliakim- Tabora Boys

Form Six 2022 Kachungulie Matokeo Yako.

Screenshot_20220705-120600_Opera.jpg
 
Attachments

  • PRESS ACSEE2022.pdf
    592.3 KB · Views: 15
Kufaulu ni rahisi hivi these days!?
Urahisi ulianzia kwenye awamu ya 5, ikawa kila wizara inataka kujionesha kwamba kuna mabadiriko yanaonekana, hapo ndio percentage ya ufaulu ilipotoka kwenye range ya 75-78% mpaka 98%

Wakaanzia primary watoto wakawa wanafaulu Hadi wale wasiojua kusoma na kuandika, ikafkia hatua shule zinakuwa chache, wengine wanakaa nyumbani

Ikaja secondary, ndio ikawa kichekesho maana kuna kipindi ata wazazi na walezi wakawa wanashangaa watoto wao wanafaulu vipi kwenda Advance

Kama hiyo haitoshi ikafkia hatua shule za kata zikaanza kuingia kwenye shule Bora, hiyo yote ni kumfurahisha tu muheshimiwa bila kujua kuwa tunaharibu elimu yetu

We ngoja baada ya matokeo kutangazwa very soon utaanza kusoma nyuzi za wadogo zetu humu wakiulizia vyuo nk, ndio utajua ni Kwa kiasi kuna wadogo zetu hawajui wamefaulu vipi
 
Usomaji umekuwa rahisi zaidi siku hizi siyo kama zamani.

Material, walimu wakutosha
 
Back
Top Bottom