Kila yanapozungumzwa maswala mazito yanayohusu namna taifa letu hili masikini lilivyodhulumiwa nakuibiwa na wajanja hawa wachache,sioni kauli ya JK ikinielekeza kwamba anaside na wananchi walio wengi ambao hawawezi kupata milo 2 ya siku na ambao kwao wao JK ni kama mkombozi wao badala yake najikuta kubakia kuamini kwamba pengine JK si mtetezi wao,pengine ni mtetezi wa hao wachache ambao wanatumia nafasi zao kuwanyima watanzania walio wengi fursa ya kupata huduma muhimu za afya na elimu bila tatizo.Kama JK yuko pamoja nasi namuomba aonyeshe kwa vitendo na maneno kwamba yuko pamoja nasi! Bado nabakia kuamini JK ni jawabu la matarajio ya wananchi wa Tanzania kwahivyo namuomba athibitishe hilo kwa vitendo haraka iwezekanavyo. Mungu Ibariki Tanzania