NEC yazika mzimu wa Richmond

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
NEC yazika mzimu wa Richmond
*Baadhi ya wabunge watetea watuhumiwa rasmi

*Wataka mijadala ya EPA, Richmond iwekwe kando

* Wengine wataka wachukuliwe hatuza zaidi

*Kikwete awaruhusu kuikosoa serikali kwa hoja

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchgi

KUNDI la wabunge na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliopangwa kutetea Kampuni ya Richmond Development wamejitokeza rasmi jana kwenye kikao chao.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zilithibitisha kuwa kundi hilo liliwashambulia wabunge wanaotaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya watu waliohusika na Richmond na uchotaji fedha kutoka kwenye Akauti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwa mmoja wa wajumbe wa NEC, Mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Manyara alikuwa wa kwanza kuchangia hoja hiyo, akitaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wa Richmond na EPA na kwamba, wananchi

hawatawaelewa kama itaishia kwa waliotuhumiwa kujiuzulu.

Mbunge huyo alisema, wananchi wanahitaji hatua zaidi kwa wahusika badala ya kuishia kujiuzulu na kwamba, hali hiyo itakuwa ni kuimarisha CCM.

Mbunge kutoka Mkoa wa Singida (jina tunalo) aliongezea kuwa zinahitajika hatua za makusudi, kurejesha imani ya wananchi kwa chama chao kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zimedai kuwa, mwelekeo wa upepo kwa wabunge wanaotaka kuchukuliwa hatua, ulibadilishwa na kiongozi mmoja wa Jiji la Dar es Salaam ambaye alitaka wabunge wasilaumu, badala yake wakisaidie chama kujijenga.

"Niko Magogoni, nataka kuvuka kwenda Kigamboni, nahitaji kivuko imara kitakachonifikisha ng'ambo. Wabunge wa CCM hamsaidii chombo kuwa imara kama mtaendelea kushutumiana," alinukuliwa Kimbisa.

Msumari wa moto uliongezewa na Mbunge mmoja wa Kigoma (jina tunalo), aliyesema mwaka 2010, wananchi hawatahoji Richmond wala EPA zaidi ya kuhoji barabara na maji.

"Mwaka 2010, wananchi hawatatuuliza Richmond wala EPA, watatuuliza maji na barabara tulizowaahidi ziko wapi?" alisema Serukamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa mmoja aliwacharukia wabunge hao akidai kuwa wanalipwa vizuri, lakini wanashindwa kutetea chama, wakati viongozi wa chama wako taabani.

Mbunge wa jimbo moja mkoani alimsifu mmoja wa watuhumiwa wa Richmond kuwa, anakisaidia chama na kutoa mfano wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto akisema walikuwa hatarini kushindwa kama si msaada wa mtu huyo.

"Kule Kiteto nilipofika nilimwangalia Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM), naye akaniangalia, ilikuwa wazi tushindwe, lakini tukasema inahitajika helikopta tukampigia simu mtu huyo (jina tunalo) helikopta ikafika kesho yake," alisema Komba.

Pia hoja hiyo ilichangiwa na Mbunge wa jimbo moja mkoani Tabora, ambaye aliunga mkono kuwatetea watuhumiwa hao wa Richmond.

Habari kutoka ndani ya kikoa hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi walikana kuhusika na Richmond, huku Lowassa akisema alijiuzulu ili kulinda maslahi ya chama.

Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema, kila mtu ana mawazo na hakuna anayeweza kuwasilisha aliyotumwa na kundi fulani na kwamba, yaliyowasilishwa yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.

Rais Kikwete aliwataka wabunge wawe na uhuru kuikosoa serikali bungeni, lakini kwa hoja na kwamba kusema hivyo haina maana kuwa ana lengo la kuwanyamazisha.
 
Naona watasema hivi ....."Sasa hizi ripoti za EPA na RICHMOND zimeongezea muda ili mapendekezo ya wajumbe na wabunge wa ccm yazingatie kwa hio ripoti kamili tutawapa kikao kijacho. Asanteni naomba kutoa hoja" Watapiga makofi na wale wachache wataishiwa nguvu mana kama mambo yalikuwa magumu kiteto ya majimbo yao je? hapo 2010
 
Kazi ni kubwa sana. Nafikiri bado tunahitaji kuongeza nguvu. Kwa mwendo huu sina cha kuongeza........................
 
Ukisikiaa siasa ndio hizii sasa.........jama wanajuaa siasa hawa..huwezi kuwashinda kwa longolongo...wamepikwa wakapikika hasa.....
 
hawajui siasa hao,kinachofanyika ni wao kutumia madaraka yao vibaya.vyombo vyote vya dola vinafuata ilani ya ccm ktk kutekeleza majukumu yao.
 
NEC yazika mzimu wa Richmond
*Baadhi ya wabunge watetea watuhumiwa rasmi

*Wataka mijadala ya EPA, Richmond iwekwe kando

* Wengine wataka wachukuliwe hatuza zaidi

*Kikwete awaruhusu kuikosoa serikali kwa hoja

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchgi

KUNDI la wabunge na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliopangwa kutetea Kampuni ya Richmond Development wamejitokeza rasmi jana kwenye kikao chao.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zilithibitisha kuwa kundi hilo liliwashambulia wabunge wanaotaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya watu waliohusika na Richmond na uchotaji fedha kutoka kwenye Akauti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwa mmoja wa wajumbe wa NEC, Mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Manyara alikuwa wa kwanza kuchangia hoja hiyo, akitaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wa Richmond na EPA na kwamba, wananchi

hawatawaelewa kama itaishia kwa waliotuhumiwa kujiuzulu.

Mbunge huyo alisema, wananchi wanahitaji hatua zaidi kwa wahusika badala ya kuishia kujiuzulu na kwamba, hali hiyo itakuwa ni kuimarisha CCM.

Mbunge kutoka Mkoa wa Singida (jina tunalo) aliongezea kuwa zinahitajika hatua za makusudi, kurejesha imani ya wananchi kwa chama chao kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zimedai kuwa, mwelekeo wa upepo kwa wabunge wanaotaka kuchukuliwa hatua, ulibadilishwa na kiongozi mmoja wa Jiji la Dar es Salaam ambaye alitaka wabunge wasilaumu, badala yake wakisaidie chama kujijenga.

"Niko Magogoni, nataka kuvuka kwenda Kigamboni, nahitaji kivuko imara kitakachonifikisha ng'ambo. Wabunge wa CCM hamsaidii chombo kuwa imara kama mtaendelea kushutumiana," alinukuliwa Kimbisa.

Msumari wa moto uliongezewa na Mbunge mmoja wa Kigoma (jina tunalo), aliyesema mwaka 2010, wananchi hawatahoji Richmond wala EPA zaidi ya kuhoji barabara na maji.

"Mwaka 2010, wananchi hawatatuuliza Richmond wala EPA, watatuuliza maji na barabara tulizowaahidi ziko wapi?" alisema Serukamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa mmoja aliwacharukia wabunge hao akidai kuwa wanalipwa vizuri, lakini wanashindwa kutetea chama, wakati viongozi wa chama wako taabani.

Mbunge wa jimbo moja mkoani alimsifu mmoja wa watuhumiwa wa Richmond kuwa, anakisaidia chama na kutoa mfano wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto akisema walikuwa hatarini kushindwa kama si msaada wa mtu huyo.

"Kule Kiteto nilipofika nilimwangalia Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM), naye akaniangalia, ilikuwa wazi tushindwe, lakini tukasema inahitajika helikopta tukampigia simu mtu huyo (jina tunalo) helikopta ikafika kesho yake," alisema Komba.

Pia hoja hiyo ilichangiwa na Mbunge wa jimbo moja mkoani Tabora, ambaye aliunga mkono kuwatetea watuhumiwa hao wa Richmond.

Habari kutoka ndani ya kikoa hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi walikana kuhusika na Richmond, huku Lowassa akisema alijiuzulu ili kulinda maslahi ya chama.

Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema, kila mtu ana mawazo na hakuna anayeweza kuwasilisha aliyotumwa na kundi fulani na kwamba, yaliyowasilishwa yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.

Rais Kikwete aliwataka wabunge wawe na uhuru kuikosoa serikali bungeni, lakini kwa hoja na kwamba kusema hivyo haina maana kuwa ana lengo la kuwanyamazisha.

Hii hoja si mali ya ccm bali ya bunge zima, hivyo naona kama haki ya wanachi inazidi kuibiwa hivi hivi hao waliotetea huo upuuzi Mungu anawaona watahukumiwa mbele ya haki, na hukumu hiyo haipo mbali, watahukumiwa huku tukiona, na tutawanyoshea kidole baada ya hiyo hukumu, Watanzania tukaze uzi, hakuna kulala
 
Mikakati ya CCM kuhakikisha ya kwamba maovu yao wanayafunika... Kuepukana na hili hawatachelewa kuzusha kitu kingine ili tu Attention ya Mwananchi Mlalahoi iwe Diverted.

Sikubaliani na hatua Ya CCM kuendelea kuwakumbatia Mafisadi na huku Wajumbe wengine vwa hiyo Kamati Kuu wakidiriki kuwapongeza wale MAFISADI ambao waliamua kujiuzuru nyadhifa zao za uwaziri.

Kujiuzuru pekee haitoshi... Hawa ni wahalifu na kwa upeo wangu mdogo wa Sheria nafahamu kwamba Tuhuma zinapokuwepo ni mpaka pale utakapokuwa umethibitishwa ya kwamba wewe si mhalifu ndipo utakuwa umetakasika. Na si Tuhuma hizo kusafishwa na Maswahiba wako, bali na Sheria za Nchi.

Fisadi angekuwa ni Mlalahoi wa Mwakaleli pale nna uhakika wangejaa Magerezani lakini kwa kuwa ni wale Wala Nchi kwa Kura za Wananchi basi inakuwa ni tabu tena... Siamini kama kuna watu wapo juu ya Sheria Tanzania hii...

JF Tuendelee kupiga kelele na natumaini matunda yake yataonekana. Nilikuwa naangalia Documentary moja ya Activist wa MArekani Michael Moore "SICKO" na humo alipowaongelea Wafaransa akasema wananchi wa Ufaransa, ili sauti zao zisikike huwa wanaandamana...na ni katika kila kitu!!! Watanzania tu waoga bado, hatuna mwamko wa Kimapinduzi. Lakini wachache tukisimama na kutetea kile kilicho haki na kukipigania kwa Mioyo yetu na kujitoa Mhanga kufika pale ambapo Mafisadi hawategemei tutafika hakika Tutashinda!!!

Lazima Tugeuze Mwendo!
 
Baada ya kusoma haya kama ni kweli CCM wameamua kuafanya haya basi nimechanganyikiwa .Kwambva tutakuwa tumesahau ya Richomdon na EPA ? hawajui kwamba huduma hakuna za barabara wala Elimu kwa kuwa wamechota pesa hizi ? Hizi si kodoi yetu ?

Ripoti ya Mwanyika na EPA itakuwa haina maana tena maana majibu ya CCM yamesha patikana .
 
Huyu Serukamba ni aibu kwa watu wa Kigoma. Mkoa wake ni miongoni mwa mikoa ilyo nyuma kabisa kimaendeleo, badala ya kuangalia ni njia zipi zingefuatwa kuwakomboa wapiga kura wake, amegeuka kuwa mpiga debe wa Lowasa. Nakumbuka Lowasa aliposurubiwa kabla ya kuachia ngazi, huyu alikuwa wa kwanza kusimama na kusema kamati ya Mwakyembe haikumtendea haki Lowasa kwa kutomhoji.

Anatia kinyaa huyu na faraja pekee niliyonayo ni imani yangu kwa wapiga kura wa Kigoma mjini. For sure, hili jimbo 2010 CHADEMA wanalirejesha.
 
ccm imeshindwa kusoma alama za nyakati. hivi mtu hata kama ni fisadi as long as alitoa helikopta kwa ajili ya kampeni ndo aachiwe ale mali ya umma! totaly stupid
 
1. "Niko Magogoni, nataka kuvuka kwenda Kigamboni, nahitaji kivuko imara kitakachonifikisha ng'ambo. Wabunge wa CCM hamsaidii chombo kuwa imara kama mtaendelea kushutumiana," alinukuliwa Kimbisa.

2. Msumari wa moto uliongezewa na Mbunge mmoja wa Kigoma (jina tunalo), aliyesema mwaka 2010, wananchi hawatahoji Richmond wala EPA zaidi ya kuhoji barabara na maji.

3. "Mwaka 2010, wananchi hawatatuuliza Richmond wala EPA, watatuuliza maji na barabara tulizowaahidi ziko wapi?" alisema Serukamba.

4. Mwenyekiti wa CCM Mkoa mmoja aliwacharukia wabunge hao akidai kuwa wanalipwa vizuri, lakini wanashindwa kutetea chama, wakati viongozi wa chama wako taabani.

5. Mbunge wa jimbo moja mkoani alimsifu mmoja wa watuhumiwa wa Richmond kuwa, anakisaidia chama na kutoa mfano wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto akisema walikuwa hatarini kushindwa kama si msaada wa mtu huyo.

6. "Kule Kiteto nilipofika nilimwangalia Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM), naye akaniangalia, ilikuwa wazi tushindwe, lakini tukasema inahitajika helikopta tukampigia simu mtu huyo (jina tunalo) helikopta ikafika kesho yake," alisema Komba.

7. Pia hoja hiyo ilichangiwa na Mbunge wa jimbo moja mkoani Tabora, ambaye aliunga mkono kuwatetea watuhumiwa hao wa Richmond.

8. Habari kutoka ndani ya kikoa hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi walikana kuhusika na Richmond, huku Lowassa akisema alijiuzulu ili kulinda maslahi ya chama.

Hizo Point nane zinaonyesha jinsi tulivyo na safari ndefu kufikia kumkomboa Mtanzania. Hao ndio tunaowategemea watuletee maendeleo.

Jk sijui atabaki upande gani? Nafikiri inatakiwa achukue eithe mafisadi au watanzania.
 
ccm imeshindwa kusoma alama za nyakati. hivi mtu hata kama ni fisadi as long as alitoa helikopta kwa ajili ya kampeni ndo aachiwe ale mali ya umma! totaly stupid

Yaani hapo nilipo soma mdomo ukabaki umeachama, kwani sikuamini kwamba CCM wako this much cheap!

Yaani mtu kama una hela yako hata ufanye madudu kwa vile unaweza kuwapa pesa usiguswe. looo? wadanganyika twafa!

Kwa lugha nyingine hata akija mafya akafanya umafya wake kwa vile anahela ya kuikodishia CCM helokopta ya kampeini basi wote inbbidi tu kimyeeeee!

Hapa sasa naona hata soni zimewaishia wanatamka bila hofu wala haya kubariki madudu yao!

Nionavyo, mzimu wa richmond hautakaa uache kuwaandama kama watendelea kuwakumbatia wahusika. Enyi CCM jitengeni na hao mafisadi na hiyo tu ndo itakuwa pona yenu.
 
ccm imeshindwa kusoma alama za nyakati. hivi mtu hata kama ni fisadi as long as alitoa helikopta kwa ajili ya kampeni ndo aachiwe ale mali ya umma! totaly stupid

Yangekuwa yapo chini ya uwezo wangu nadhani ningetoka na Sheria ya Kuponda mawe hawa mafisadi wote...

Inakera haya mambo and yanauma saaana... Hivi Lunyungu naomba niambie hii kodi yangu inaenda wapi... Nakatwqa kila mwisho wa mwezi, achana na hizi Indirect taxes!!!
 
Sisi ndio wa kushangawa tunaoendelea kuwategemea CCM wafanye makubwa. Ni ujinga wa kutisha kutarajia jambazi aliyekuibia ajikamate na kujisalimisha polisi. Tulisema jana kwenye mada ya "Kutoka Dodoma" kuwa hizo pilikapilika zitaishia kwa wao kukubaliane yaishe kwa "maslahi ya chama". Inatia hasira sana kuona watanzania wanaendelea kutegemea miujiza kutoka CCM hata baada ya kuwaangusha kwa miaka zaidi ya 40.

CCM wamshukuru na kumsifu sana aliyewanywesha watanzania hili limbwata la kutisha kiasi kwamba inapowapiga na kuwaumiza hawaamini kwamba anayewapiga ni "kipenzi" chao CCM!
 
[Mbunge wa jimbo moja mkoani alimsifu mmoja wa watuhumiwa wa Richmond kuwa, anakisaidia chama na kutoa mfano wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto akisema walikuwa hatarini kushindwa kama si msaada wa mtu huyo.

"Kule Kiteto nilipofika nilimwangalia Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM), naye akaniangalia, ilikuwa wazi tushindwe, lakini tukasema inahitajika helikopta tukampigia simu mtu huyo (jina tunalo) helikopta ikafika kesho yake," alisema Komba.

Pia hoja hiyo ilichangiwa na Mbunge wa jimbo moja mkoani Tabora, ambaye aliunga mkono kuwatetea watuhumiwa hao wa Richmond.

Habari kutoka ndani ya kikoa hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi walikana kuhusika na Richmond, huku Lowassa akisema alijiuzulu ili kulinda maslahi ya chama.
 
mnafahamu kuhusu helikopta inayozungumziwa? ilibidi kinana awasiliane na chadema kutafiti kuhusu bei ya kukodi helikopta, manake hiyo halikopta ccm walikodisha kwa siku mbili wakalipa 312,000,000. waKATI CHADEMA WALIKODI KWA KIPINDI CHOTE CHA KAMPENI KWA 18,000,000.

huyu mhindi atawamaliza hawa
 
Hakuna jipya,
alishajisemea mrema zamani sana
CCM haiwezi kujisafisha yenyewe.
Nani alisikiliza?
 
kutegemea mageuzi toka ccm ni sawa na kutegemea supu toka kwenye chungu kitupu! acheni kuumiza vichwa vyenu
 
Sisi ndio wa kushangawa tunaoendelea kuwategemea CCM wafanye makubwa. Ni ujinga wa kutisha kutarajia jambazi aliyekuibia ajikamate na kujisalimisha polisi. Tulisema jana kwenye mada ya "Kutoka Dodoma" kuwa hizo pilikapilika zitaishia kwa wao kukubaliane yaishe kwa "maslahi ya chama". Inatia hasira sana kuona watanzania wanaendelea kutegemea miujiza kutoka CCM hata baada ya kuwaangusha kwa miaka zaidi ya 40.

CCM wamshukuru na kumsifu sana aliyewanywesha watanzania hili limbwata la kutisha kiasi kwamba inapowapiga na kuwaumiza hawaamini kwamba anayewapiga ni "kipenzi" chao CCM!

Angalau SIO miaka zaidi ya 40 ingawa hilo sio muhimu sana kwa sasa. Usisahau pia kwamba NDOA za WAKURYA ambao wanasifika saana kuwapiga wake zao HAZIVUNJIKI kirahisi!
 
Back
Top Bottom