Naipongeza kambi ya upinzani iliyoko bungeni kwa sasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,299
Watu wengi wa CCM hata upinzani wamekuwa waoga kujitokeza kuwapongeza wabunge wa kambi rasmi ya upinzani ikiongozwa na wabunge 19 wa viti maalum kupitia CHADEMA na mmoja wa kuchaguliwa CHADEMA.

Mimi leo nimeona nijitokeze kuwapongeza kina mama hawa shupavu kutoka CHADEMA wanaoweza kujenga hoja kistaarabu bila kuzua taharuki bungeni kama ilivyokuwa kwenye mabunge yaliyopita.

Mambo mengi waliyoyapeleka bungeni kwa niaba ya wananchi yalisikilizwa na kufanyiwa kazi na serikali ya CCM bila kubagua kama hoja ni ya kutoka kwa mbunge wa CHADEMA.

Kwa mfano mbunge viti maalum CHADEMA mheshimiwa Cecilia Paresso aliwakilisha kilio cha muda mrefu cha wakazi wa wilaya ya Karatu kuvamiwa na wanyama wakali kisha kupata majeraha na wengine kupoteza maisha. Ile kero ilifanyiwa kazi kwa haraka na huko Karatu hakuna tena mambo ya fisi kuvamia wananchi.

Siasa sio uadui. Wabunge wa CHADEMA walioko bungeni wamethibitisha hilo kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom