hakika wabunge wa dar mmeonesha uzalendo kwa kuweka vyama venu pembeni na kupigania watanzania wote.hongereni sana
Nadhani mkuu utakuwa umechanganya na Surface and Marine Transport Regulatory Authority (SUMATRA) Ambayo ndo inahusika na hayo mamboNaomba mwenye uelewa na haya mambo atusaidie, Energy and Water Utilities Regulatory Authority inaingiaje hapa? Au ile WATER inamaanisha na boti, vivuko, kambale nk.
Majuuzi mafuriko ya Dsm mko kimya, Mahosipitalini mfano Muhimbili,Mwananyamala, Amana na TMK huduma haziko sawa, mko kimya.... Hizi gharama za maisha zinavoenda juu namna hii mmeona kivuko tu? Nauli za daladala, mabasi ya mikoani na hapo mmekaa kimya tuuu... Mi na hofu na chanzo cha huu msukumo na huu umoja wa ghafla
hakika wabunge wa dar mmeonesha uzalendo kwa kuweka vyama venu pembeni na kupigania watanzania wote.hongereni sana
Watu wa kigamboni acheni kudekadeka nauli ya 200 ipo sahihi na kauli ya Magufuli ipo sahihi. Kama mnapinga ongezeko la nauli unganeni na wabunge wenu kupinga mfumuko wa bei ya chakula kama mchele, sukuri, unga na pia ongezeko la ada za shule etc sio kushupalia kitu kidogo kupiga mbiziKwako ni ndogo lakini kwa wenzako ni kubwa sana. Fikiri mtu anayefanya shughuli zake K'koo na anakaa Tungi au Mjimwema. Tungi-Kigamboni,300/=; Pantoni-200/=; Kivukoni-K'koo 300/=. Jumla kwenda na kurudi ni 1600 per day. Assume ni siku moja kwa wiki havuki, kwa mwezi atatumia 41,600/=. Sasa hebu tia akili.
Mbunge anajiumbua mwenyewe kwanini hatukumsikia akipinga ongezeko la Posho na marupurupu ya wabunge ache kutuzingua nauli ipo sawa asiweza apige mbizi mbona sisi wakazi wa mbezi mwisho tunalipa nauli ya daladala 1500 kila jioni na wabunge hawapingi shilingi mia mbili mbunge anatufa umaarufu wa kujulikana kwanza tulikuwa hatumfahamu aibue hoja zake binafsi na sio kudandia hoja za waziri mtendajiEWURA???
Mbunge amechemka big time...
Ni kweli kipo chini ya wizara yake lakini nafikiri SUMATRA ndio wanamamlaka ya kupanga bei wakishirikisha wadau. Suala linalomwandama Mgufuri hapa ni kauli ameshindwa kuwasilisha hoja yake kwa maskini lakini nauli kuwa 200 sifikirii kwamba ni tatizo kubwa. Hii inatufundisha viongozi wanatakiwa wachunge midomo yao kwani siku moja tu unaweza ukaharibu sifa zako zote
hiyo ni strategy ya kuwaondoa kigamboni ili bush aingie kilaini
Nimejiuliza hilo swali mara nyingi bila kupata majibu maana ferry Mombasa zina hali nzuri sana, usafiri ni bure na hata wafanyakazi wa ferry wanafanya kazi zao za kwa umakini mkubwa, sijui hapa bongo tatizo ni nini maana basi hata kama wameamua wananchi kuchangia huduma ingekuwa kidogo sana ili angalau kila mtu aweze kutumia.Mombasa kenya kuna ferry nzuri sana na watu huvushwa bure miaka nenda rudi.Kenya ni nchi ya kibepari ambayo kwao kutafuta faida na pesa ni kitu kikubwa.Wao na ubepari wao na uroho wao wamewezaji kuvusha maelfu ya watu kwa ferry kila siku bila kuwatoza pesa? Siri yao ni nini wajuzi mtujuze kama hamjui nendeni mkajifunze Mombasa kwenye ferry zao mtuletee taarifa