Ndugulile: Magufuli hajui sheria, anakurupuka tu...

kivuko ni sawa na daraja ndugulile ndo kachemsha so kipo chini ya wizara ya ujenzi it seems hawa watu hawajui wanachokifanya

Mkuu nadhani hapa kuna issue zinaingiliana! From the Highway Engineering point of view kivuko ni daraja linalotembea. Lakini sasa kwa upande wa usafirishaji kivuko ni usafiri wa majini!! SUMATRA ndio wanaoratibu usafiri wa majini na kukagua vivuko na kuvipa leseni kama inavyofanya kwenye meli, majahazi, mitumbwi, merikebu, nk. Kwa jinsi tunavyochangia humu inaonekana kuna sheria mbili zinaingiliana. Kwamba Wizara ya Ujenzi inakiangalia kivuko kama daraja na hivyo kukawa na sheria ya kumpata Waziri mwenye dhamana uwezo wa kupanga nauli. Kwa upande mwingine huenda SUMATRA wakakiangalia kivuko kama usafiri wa majini basi sheria ikawapa uwezo wa kuratibu na kupanga bei! Huenda huu ndio mkanganyiko.
 
suala la nauli ya kivuko hata wadau wangejadiliana isingebadili chochote ila na wananchi pia tuangalie je unaweza kulinganisha nauli ya mwaka 96 na leo hii ? Fikiria hicho kivuko unapewa wewe unaweza kuendesha kwa gharama ya sh mia?

Hebu jiulize kivuko kimenunuliwa na fedha ya nani ? Wizara inayosimami hicho kivuko inapata fedha za bajeti yake kutoka vyanzo gani kama sio kodi, na kodi hiyo inatoka kwa nani kama sio mwananchi. Je unataka serikali iendeshe kivuko kibiashara ama kutoa huduma nafuu kwa wananchi ambao ndio walipa kodi ?
 
mimi binafsi sijaona tatizo sana kwa nauli kwa watu kufikia 200, tatizon lipo kwa wenye GUTA,ivi kweli guta lilipiwe 1800 zaidi ya gari?ukichukulia guta linaendeshwa kwa kutumia damu,huu ni unyonyaji mkubwa nadhani vitu kama guta,bajaji na pikipiki vingewekwa kwenye kundi moja walipe 500 kwani matokeo yake kwa sasa itakuwa ni kupanda kwa garama ya maisha huko kigamboni kwa bidhaa zinazovushwa kama hususan vyakula vinavyotoka katika masoko ya kariakoo,ilala na madukani kwa ujumla.
 
ina maana mwenye guta ana maisha mazuri kuliko mwenye gari???????????????????
 
Hawa wabunge wanatia aibu sana..... EWURA?
Kile kivuko si kipo chini ya Comworks?

Huyo mbunge yeye ndio hajui sheria. EWURA na kivuko wapi na wapi?!

Pia uwa nashangaa wabunge wanavyotoa malalamiko juu ya sheria wakati wenyewe ndio watungaji wa hizo sheria.

Katika dunia ya sasa ambapo people centred approach kwa kila jambo ni priority,hao wabunge walikua wapi wakati sheria inamruhusu waziri husika kuamua nauli za vivuko mwenyewe?

Tatizo ni wabunge wetu kutaka kupoliticize kila jambo for vested interests.
 
Eh! Ewura wanapandisha nauli za vyombo vya usafiri au nishati tu?
Live Channel Ten Mbunge wa Kigamboni Anamuumbua live Live Magufuli na Wazara yake kuwa Hawana haki ya kuongeza Nauli Mpya kwani hiyo mamlaka amaepewa EWURA tena lazima Wadau washirikishwe...
 
Kupandisha bei ya kuuzia bidhaa yako kunahitaji sheria au uanaangalia gharama zako na faida unayoitaka? Kwa bei hizi sidhani kama waziri ameangalia faida ila kaangalia uwezo wa kuhudumia hicho kivuko pamoja na mambo mengine kama uchakavu wa kivuko na gharama za uendeshaji. Hebu mtu aposti gharama za uendeshaji na gharama za kumaintain kivuko kila mwezi.
Magufuri kakurupuka tu hajui Sheria kazi yake ni kutukana wananchi tu wa Kigamboni Wanaomba Serikali Imchukulie Hatua kali ikiwemo kumvua Gamba... Sasa tuone nani Zaidi Wametengeneza tiketi Bandia wanachumia matumboni mwao pesa nyingi haziingii serikalini Na pia ticket zinauzwa mara kadhaa so pale cha muhimu wadhibiti makusanyo kituo kinaweza kujiendesha na ikiwezekana wabadilishwe wote pale waje waongoza kivuko wapya.
 
Sioni mantiki ya kupata maoni ya wananchi ili upandishe bei ya bidhaa yako. Jamani tuache siasa kwenye mambo ya msingi. Bei bado ziko reasonable.
Like father like son!
Mbona kuandaa mchakato wa katiba rais naye hakuhitaji maoni ya wananchi? Magufuri naye aliona ikiwa jambo zito kama Katiba Rais hakuhitaji maoni ya wananchi au wadau, kwa nini jambo dogo tu kama kivuko?
 
suala la nauli ya kivuko hata wadau wangejadiliana isingebadili chochote ila na wananchi pia tuangalie je unaweza kulinganisha nauli ya mwaka 96 na leo hii ? Fikiria hicho kivuko unapewa wewe unaweza kuendesha kwa gharama ya sh mia?
Swali ni kwa siku kivuko hicho kinavusa watu wangapi na kinaingiza Shilingi ngapi na ngapi zinzingia serikalini?
 
Live Channel Ten Mbunge wa Kigamboni Anamuumbua live Live Magufuli na Wazara yake kuwa Hawana haki ya kuongeza Nauli Mpya kwani hiyo mamlaka amaepewa EWURA tena lazima Wadau washirikishwe...

Sisi huku mwanza kivuko cha busisi tayari tumeanza kulipishwa nauli mpya wizara iliyoipandisha. Ilikuwaga zamani Tsh 300/= kwa mtu mmoja na sasa ni Tsh 400/= sijui kwa gharama za magari zimepanda kiasi gani
 
Sioni mantiki ya kupata maoni ya wananchi ili upandishe bei ya bidhaa yako. Jamani tuache siasa kwenye mambo ya msingi. Bei bado ziko reasonable.

Na mabaraza ya walaji yana kazi gani kama huoni mantiki ya kupata maoni? Serikali inawakamua raia zake hivihivi aisee, tanesko nao wako mbioni kupandisha bado hivi punde tutaskia tena dawasco nao
 
Tuache malumbano acha kila mtu awajibike kwa nafasi yake, Magufuli fanya kazi yako bila woga.USHAURI UDHIBITI KWENYE MAPATO UONGEZWE ILI HICHO KIASI KILICHOONGEZWA KIWE NA TIJA KWA TAIFA.
 
tuangalie na upande wapili wa shilingi hivi hao wanainchi wa kigamboni wao walikuwa na haki ya kumzomea bwana pombe magufuri?:juggle::juggle::juggle:
 
Back
Top Bottom