Ndugu Zitto ziarani Ulaya

Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari

Wakati mwingine yatupasa kuwa objective, Nchi haijengwi na CCM au CDM, Nchi inajengwa na Watanzania, ZZK ni mmoja wao. ziara ya ZZK haionyeshi kama ni ya kubomoa nchi.
Hata kama inalenga kumjenga kisiasa, what is wrong with that? kazi ya mwanasiasa yeyote ni kujijenga kisiasa and Zito anatumia haki hiyo pia.
 
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo “Economic Conference: Commitment to Africa Initiative” utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.
Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.
Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.
Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.
Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.
Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini
8 Desemba 2012, Dar es Salaam

Lieber Zito,herzlich gluckwuensch fuer Deiner Reise in Deutschland.Du bist einfach kruger person.Moege es Gott Dich schuetzen.Keep it up.Kiukweli chama chetu kwa sasa kimekomaa sana na kipo tayari kuchukua nchi na baada ya hapo naamini Tanzania itakuwa na uchumi imara kuliko nchi yoyote duniani.Kwa sasa tunashindwa kupiga hatua kwaajili ya CCM kuwaongoza watanzania mithili ya mbusi.Zito ni jembe mojawapo katika CDM.Kwa upande wa ccm kwenye mambo makubwa ya kimataifa eti wanamtuma Mlugo,mliona alichokifanya kule SA kwa kusema Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Tanganyika.CCM makeve.
 
Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari

Wivu ni kitu kibaya sana, pamoja na ufisadi wako wote hujawahi hata kupata visa ya ujerumani, wivu ,chuki, majungu na uzandiki ndo unaowasumbua, ZZK ni next level hadi Taifa kama ujerumani ambalo kimsingi ni wenye kujivuna wanamkubali ZZK, nyie laleni na wivu wenu.
 
Tunashukuru kwa taarifa ofisi ya bunge Kigoma,Tunakutakia safari njema ndugu Zitto na tunakuombea mema huko uendako na utuwakilishe vyema.MUNGU AKUBARIKI SANA NA AENDELEE KUKUSTAWISHA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.Sisi watanzania ndo tulivyo wanafiki kwelikweli,mtu afanye mema ni mbaya na akifanya mabaya ndo mwema.
 
Zitto amepiga kelele sana kuhusu sheria ya madini na matokeo yake marekebisho yalifanyika, hivyo leseni zinatakiwa zitolewe kwa makampuni ya madini ambayo serikali ina hisa kwa asilimia 50.

Hata hivyo, week chache zilizipita vyombo vya habari vimetoa taarifa za kampuni ya Barrick kupata leseni kwa miaka mingine tena 15 kwa kutumia vigezo vya zamani - yaani serikali haina 50% ya shares!

Ningetaka kusikia toka kwa Zitto, nini maoni yake kuhusu uwekezaji wa Barrick Tanzania na sheria za madini.

Kwanza nashukuru sana kwa kuleta suala hili. Sheria mpya ya madini inataka leseni mpya zote zitakazotoka chini ya sheria ile Serikali iwe na hisa kwenye mgodi husika kwa kuanzia asilimia 15(free carried). Pia sheria mpya iliyotungwa kutokana na mapendekezo ya kamati ya Bomani imeweka masharti mapya ya leseni na mfumo wa kodi.

Natumai Waziri kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika ataweza kueleza nini hasa kimetokea kwenye mgodi wa North Mara.

Sio hivyo tu, kampuni ya Mantra pia imepewa leseni ya maalumu ya kuchimba Urani wakati bado hawajalipa capital gains tax yetu kufuatia mgodi mradi kununuliwa na warusi.

Sijui Prof Muhongo ana maelezo gani kuhusu suala hili maana yeye ndie mtoa leseni kwa mujibu wa sheria
 
Chedema wasipompitisha ZZK, watampitisha nani?. Mkumbuke sisi wengine tunaujua msimamo wa Dr tena sio kwa hearsay but from hoses mouth!. ZZK is the one and only Chadema has! japo mshindi rasmi wa urais wa Tz kwa 2015 ni mgombea wa CCM!.
P.

Kwa nini unafikiri kwamba mshindi 2015 atatoka thithimu? Lazima uje na sababu ya kuaminika. Isije ikawa uchakachuaji umeanza tayari.
 
Zitto, you are just a talented young man. Keep learning and get as much exposure as you can. No one is perfect, but you are far far better than many of us. You are in the right direction, keep going!
 
Safi sana Zito, Jamani zitto kwenda ziarani ulaya siyo kwamba anajifanya rais hapana ,Zitto anajua taratibu zote za kumpata mgombea na anafahamu itifaki zote. Nenda kaka, nenda, pigania mabilioni yetu uswisi, sema kaka, kaseme nenda kaseme, simama juu ya mimbari upaze sauti za wanyonge namna tunavyoibiwa na viongozi wetu na hao wazungu wanaojifanya wafadili. Viva Zitto
Duuu, hizo sema kaka zilivyo nyingi!
 
Kwanza nashukuru sana kwa kuleta suala hili. Sheria mpya ya madini inataka leseni mpya zote zitakazotoka chini ya sheria ile Serikali iwe na hisa kwenye mgodi husika kwa kuanzia asilimia 15(free carried). Pia sheria mpya iliyotungwa kutokana na mapendekezo ya kamati ya Bomani imeweka masharti mapya ya leseni na mfumo wa kodi.

Natumai Waziri kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika ataweza kueleza nini hasa kimetokea kwenye mgodi wa North Mara.

Sio hivyo tu, kampuni ya Mantra pia imepewa leseni ya maalumu ya kuchimba Urani wakati bado hawajalipa capital gains tax yetu kufuatia mgodi mradi kununuliwa na warusi.

Sijui Prof Muhongo ana maelezo gani kuhusu suala hili maana yeye ndie mtoa leseni kwa mujibu wa sheria

Tuna mambo mawili makubwa ya kuangalia:
1. Umiliki wa hisa wa makampuni ya madini kwa mujibu wa sheria za madini hapa nchini.

2. Ulipaji kodi toka kwa haya makampuni -tax evation au ukita 'profit allocation' ni tatizo kubwa sana.

Sasa hivi UK wananchi wameamua kuundamana baada ya kuambiwa makampuni kama Starbucks, Amazon, Google wamekuwa wanakwepa kulipa kodi stahiki. Hapa Tanzania sio tu kodi hatupati, ila hata utoaji wa leseni unakwenda kinyume na sheria za nchi!

Marekani must think watanzania ni mazezeta. Wamekazana kuimba wimbo wa afya ya mama na mtoto wakati huku nyuma wanachimba urani! Nilimsikiliza juzi balozi wa Marekani akitoa 'statistics' za jinsi afya mama na mtoto (maternal health) ilivyoimarika nchini (thanks to USA atataka watu waimbe hivyo), and it is shocking kwanza mtu kuja nyumbani kwako na kuanza kuongelea mambo ya mji wake tena outside the context halafu sisi tunapiga makofi.

Tanzania, kama zilizo nchi nyingi Africa, hatuhitaji misaada ya net za mbu, hatuhitaji vyakula vya jioni, hatuhitaji makongamano na nyimbo eti 'malaria no more'. Hivyo vitu vimo ndani ya uwezo wetu kama tutapata kodi toka kwa hawa hawa wanaotupa net za mbu.

Hili la Barrick ni kichefuchefu, na limekuja muda mfupi baada ya rais kufanya ziara ya kitaifa huko Canada. Ubalozi wa Canada Tanzania uko- downgraded, mambo mengi yanafanyiwa Nairobi, and that tells you nafasi ya Tanzania ni cash-cow as far as these Canadians are concerned. Hawachangii la maana hapa nchini, kuanzia bajeti ya kuu hadi kodi ya makampuni yao.

Nategemea bunge la bajeti litajidili hili. Waziri wa fedha anatakiwa atoe ufafanuzi kuhusu ukusanyaji kodi. Lakini wa Madini naye anatakiwa aeleze leseni zimetolewa kwa sheria ipi?
 
Wakati mwingine yatupasa kuwa objective, Nchi haijengwi na CCM au CDM, Nchi inajengwa na Watanzania, ZZK ni mmoja wao. ziara ya ZZK haionyeshi kama ni ya kubomoa nchi.
Hata kama inalenga kumjenga kisiasa, what is wrong with that? kazi ya mwanasiasa yeyote ni kujijenga kisiasa and Zito anatumia haki hiyo pia.

zitto ni kichwa,zitto ni jembe hilo halina ubishi.ndani ya chadema sioni mtu makini na mjenga hoja za maana kama zitto,wengine ni pumba tu.wanaompinga zitto ni *******,eti tu kwa sababu zitto ni tishio kwa wakabila.hamuwezi mfanya kitu chochote.
 
quote_icon.png
By FISADI-ORIGINAL

Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari

"by nice 2
Amaa kweli wewe ni
FISADI-ORIGINAL , hata kabla ya kusoma umeshaanza kumwaga chuki!

kweli mwana ulingamua hilo ni fisadi original la ukweli
post ya 18:31 imesomwa na kugundulika zitto ni mwenye uchu na kuandikwa majibu yake na kuipost 18:33!!!!!
kumbe, kelele nyingine dhidi ya zitto zina kusudi flani!!
 
Wakati mwingine yatupasa kuwa objective, Nchi haijengwi na CCM au CDM, Nchi inajengwa na Watanzania, ZZK ni mmoja wao. ziara ya ZZK haionyeshi kama ni ya kubomoa nchi.
Hata kama inalenga kumjenga kisiasa, what is wrong with that? kazi ya mwanasiasa yeyote ni kujijenga kisiasa and Zito anatumia haki hiyo pia.

i like your comment
 
Tatizo la vilaza wengi humu ndani hupenda kumjadili mtu kama yeye bila kuangalia kwa mapana zaidi mtu huyo anafanya kitu hicho kwa manufaa ya nani! Mtazamo na mkakati wa wana magamba wote ni kuona kuwa jitahada zote zinazofantwa na viongozi wachapa kazi wa cdm wanazivuruga kupitia mlango wa mtazamo hasi, lakini kwetu sisi tunaojua nini wanachokifanya tunasema hongerenai sana makamanda wetu.
VIVA CDM, VIVA ZITTO.
 
Zito na ofisi yake wapo sahihi Kabla ya kubisha na kuponda jaribu kujifunza maana ya ofisi ya umma na uwajibikaji wake
 
Chuki na roho mbaya zitakuuwa ndugu yangu hali ya nchi unaona inaelekea kubaya bado watu wanao kuja na solution za matatizo yetu mnawachukia kwa kisingizio cha uchu wa madaraka GIVE US A BREAK PAL.

Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari
 
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani

NAOMBENI MUONGOZO WAKUU
ziara ya kikazi; anawakilisha bunge (kama mbunge wa Tanzania), anawakilisha upinzani (kama waziri kivuli), anawakilisha chama au anawakilisha ofisi yake(mbunge wa Kigoma Kaskazini)?

Tukiacha ushabiki ni wanasiasa wachache sana kwa sasa wenye uwezo wa kutuwakilisha kwenye mikutano kama hii (bila kututia aibu), the next foreign minister? (kwa katiba ya sasa)

naombeni majibu
 
wivu ni kitu kibaya sana, pamoja na ufisadi wako wote hujawahi hata kupata visa ya ujerumani, wivu ,chuki, majungu na uzandiki ndo unaowasumbua, zzk ni next level hadi taifa kama ujerumani ambalo kimsingi ni wenye kujivuna wanamkubali zzk, nyie laleni na wivu wenu.

safi sana kwa kufikisha ujumbe kwa boya huyo wa fb and not jf
 
kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.who is zitto, rais, waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona rais wa tanzania tayari.....

soma kwa makini anaenda kufanya nini huko ujerumani hii ni sehemu ya watu makini kama vip hamia kwa wnzako fb
 
Back
Top Bottom