Ndugu Zitto ziarani Ulaya

nice 2

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
747
520
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo “Economic Conference: Commitment to Africa Initiative” utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.
Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.
Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.
Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.
Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.
Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini
8 Desemba 2012, Dar es Salaam
 

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
257
Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari
 

nice 2

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
747
520
Amaa kweli wewe ni FISADI-ORIGINAL , hata kabla ya kusoma umeshaanza kumwaga chuki!
 
Last edited by a moderator:

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Zitto amepiga kelele sana kuhusu sheria ya madini na matokeo yake marekebisho yalifanyika, hivyo leseni zinatakiwa zitolewe kwa makampuni ya madini ambayo serikali ina hisa kwa asilimia 50.

Hata hivyo, week chache zilizipita vyombo vya habari vimetoa taarifa za kampuni ya Barrick kupata leseni kwa miaka mingine tena 15 kwa kutumia vigezo vya zamani - yaani serikali haina 50% ya shares!

Ningetaka kusikia toka kwa Zitto, nini maoni yake kuhusu uwekezaji wa Barrick Tanzania na sheria za madini.
 

Kilasara

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
578
116
Hongera Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kuzuru Ujermani kueneza M4C. Uzi ni huo huo. Hakuna Kulala: Mpaka Kieleweke.
 

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Anakwenda kufunga mikataba na CDU (CHRISTIAN DEMOCRATIC UNION )
utaona hapa baada ya hii post watakavyofoka kusikia hii cdu
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,692
93,660
. Big up Zitto! President in the making. Wasipokupitisha CDM utaimgia hata kwa ugombea binafsi. Chapa kazi, CV itajieleza.
Chedema wasipompitisha ZZK, watampitisha nani?. Mkumbuke sisi wengine tunaujua msimamo wa Dr tena sio kwa hearsay but from hoses mouth!. ZZK is the one and only Chadema has! japo mshindi rasmi wa urais wa Tz kwa 2015 ni mgombea wa CCM!.
P.
 

Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
114
jaman tusiwe na negative attitude kiasi hicho kwa Zitto kamani kweli anaenda kufanya hayo ni nzuri kwa nchi yetu, ni juzi tu hapa watu walikuwa wanahoji ooh anaenda kufanya nini mara nani atalipia safari, siungi mkono zitto kugombea uraisi lakini naunga mkono watanzania kuongeza knowledge na kuplay other international roles ni faida kwetu. all the best Zitto
 

Jallen

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
516
193
Safi sana Zito, Jamani zitto kwenda ziarani ulaya siyo kwamba anajifanya rais hapana ,Zitto anajua taratibu zote za kumpata mgombea na anafahamu itifaki zote. Nenda kaka, nenda, pigania mabilioni yetu uswisi, sema kaka, kaseme nenda kaseme, simama juu ya mimbari upaze sauti za wanyonge namna tunavyoibiwa na viongozi wetu na hao wazungu wanaojifanya wafadili. Viva Zitto
 

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
142
Sioni tatizo Zitto kuwepo kwenye mkutano huo kama wahusika wameona atakuwa a good resource person.Huo ni wivu tu.Kuna haja gani ya kumkaribisha mtu kwenye mkutano kama huo ambae hajui hata kwanini wananchi wake ni maskini?
Kiburi, jeuri na tamaa ya madaraka inapozidi ndo matokeo yake haya.Who is Zitto, Rais, Waziri mkuu?
Ofisi yake inatoa Press release ya safari zake?
Zito anaenda kubaya na uchu wa madaraka.
Huyu mtu ni hatari.Inabidi ajiangalie angalau awe myenyekevu kidogo
anajiona Rais wa Tanzania tayari
 

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928
2,030
Hongera Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kuzuru Ujermani kueneza M4C. Uzi ni huo huo. Hakuna Kulala: Mpaka Kieleweke.
Hivi anaenda kueneza M4C? Mbona sijaona sehemu inayoonyesha atafanya kazi za Chama?
 

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,451
Ma pro ccm mnakazi kwelikweli. acheni wivu wa kike.ingekuwa ni mme wenu nape mgeshabikia ile mbaya
 

nice 2

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
747
520
Zitto amepiga kelele sana kuhusu sheria ya madini na matokeo yake marekebisho yalifanyika, hivyo leseni zinatakiwa zitolewe kwa makampuni ya madini ambayo serikali ina hisa kwa asilimia 50.

Hata hivyo, week chache zilizipita vyombo vya habari vimetoa taarifa za kampuni ya Barrick kupata leseni kwa miaka mingine tena 15 kwa kutumia vigezo vya zamani - yaani serikali haina 50% ya shares!

Ningetaka kusikia toka kwa Zitto, nini maoni yake kuhusu uwekezaji wa Barrick Tanzania na sheria za madini.

Hivi kwani Zitto ni waziri kivuli wa madini!
 

Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,288
129
Kila mmoja anatakiwan awe na press club kuongeza uwazi na ywajibikaji sio wkati mwingine utasikia watu wkubwa wanaenda nje kutoa wauza mihadarati
 

bluetooth

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
4,403
2,520
Chedema wasipompitisha ZZK, watampitisha nani?. Mkumbuke sisi wengine tunaujua msimamo wa Dr tena sio kwa hearsay but from hoses mouth!. ZZK is the one and only Chadema has! japo mshindi rasmi wa urais wa Tz kwa 2015 ni mgombea wa CCM!.
P.

mkuu Pasco, EL afya yake siyo convinient kuwa mgombe wa urais ingawa mnajaribu ku-force, membe hana uwezo wa kupanda jukwaani kuomba kura na kujibu maswali kutoka kwa wananchi kuhusu ufisadi, hapa aliyebaki ni Mizengwe Pinda Kayanza

je utampa kura ya urais mtoto wa mkurabita, huyu ndiyo the only option ya ccm
 

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,680
251
Hivi Zitto anatumwa na Chadema au CCM? Maana naona kama wapiga debe wa CCM ndio wanashadadia safari yake hiyo.
 

Wingu

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,319
397
Kwa nini asiende Lema jamani au kwa sababu hajui kingereza
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
44,664
135,890
Hii ni hatua nzuri ya kuwapa nafasi (kuwapa exposure ) wanasiasa wa upinzani katika maswala ya kimataifa.

Zitto anawakilisha na kuwaandalia njia wanasiasa wenzake, hasa vijana, wa upinzani.

He is a model young politician.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom