Waziri Makamba abainisha mafanikio ya Serikali kwa Mwaka 2023 kupitia Utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.) ameainisha mafanikio yaliyopatikana kwa Taifa kutokana na utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi kuwa ni pamoja na kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine, kukua kwa biashara, uwekezaji na utalii na kuongezeka kwa ushawishi na sauti ya Tanzania katika majukwaa ya kikanda na kimataifa.

Makamba ameanisha mafanikio hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 17 Desemba 2023 wakati akitoa Tathmini ya Mafanikio ya Wizara katika Kueneza, Kukuza na Kupanua Diplomasia ya Tanzania Kimataifa kwa mwaka 2023 pamoja na kutoa Mwelekeo na Matarajio ya Wizara kwa Mwaka 2024.
GBj6QF5XwAA3ZpW.jpeg

GBj6QF6W0AAPhhc.jpeg

Makamba amesema kuwa, Diplomasia ya Tanzania chini ya uongozi imara wa Mwanadiplomasia namba moja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarika katika nyanja mbalimbali ambapo kupitia uratibu wa Wizara na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Tanzania katika kipindi cha mwaka 2023 imefanikiwa kuimarisha uhusiano ya uwili, kukuza biashara na uwekezaji, kuongeza ushawishi wa Tanzania katika masuala mtambuka yanayohitaji ushirikiano wa kimataifa, kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimkakati na kuongezeka kwa watalii.

Akifafanua kuhusu kuimarika kwa ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na nchi mbalimbali duniani na mashirika ya kimataifa, Mhe. Makamba amesema kupitia ziara mbalimbali zilizofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia, Viongozi Wakuu Serikalini na zile zilizofanywa na Marais na Wakuu wa Mashirika kutoka nje ya nchi hapa nchini zimeiwezesha Tanzania kunufaika kiuchumi kwa kuimarika zaidi kwa ushirikiano na nchi hizo pamoja na mashirika ya kikanda na kimataifa.

Kadhalika amesema kuimarika kwa ushirikiano huo kumeiwezesha Tanzania katika mwaka 2023 kuwa mwenyeji wa mikutano mikubwa ya kikanda na kimataifa ukiwemo Mkutano wa Kimataifa kuhusu Mifumo ya Uzalishaji wa Chakula na Mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya Rasilimali Watu.
 
View attachment 2845964
View attachment 2845965

Kazi iendelee.
P
 
Back
Top Bottom