Kwanza nashukuru sana kwa kuleta suala hili. Sheria mpya ya madini inataka leseni mpya zote zitakazotoka chini ya sheria ile Serikali iwe na hisa kwenye mgodi husika kwa kuanzia asilimia 15(free carried). Pia sheria mpya iliyotungwa kutokana na mapendekezo ya kamati ya Bomani imeweka masharti mapya ya leseni na mfumo wa kodi.
Natumai Waziri kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika ataweza kueleza nini hasa kimetokea kwenye mgodi wa North Mara.
Sio hivyo tu, kampuni ya Mantra pia imepewa leseni ya maalumu ya kuchimba Urani wakati bado hawajalipa capital gains tax yetu kufuatia mgodi mradi kununuliwa na warusi.
Sijui Prof Muhongo ana maelezo gani kuhusu suala hili maana yeye ndie mtoa leseni kwa mujibu wa sheria
Tuna mambo mawili makubwa ya kuangalia:
1. Umiliki wa hisa wa makampuni ya madini kwa mujibu wa sheria za madini hapa nchini.
2. Ulipaji kodi toka kwa haya makampuni -tax evation au ukita 'profit allocation' ni tatizo kubwa sana.
Sasa hivi UK wananchi wameamua kuundamana baada ya kuambiwa makampuni kama Starbucks, Amazon, Google wamekuwa wanakwepa kulipa kodi stahiki. Hapa Tanzania sio tu kodi hatupati, ila hata utoaji wa leseni unakwenda kinyume na sheria za nchi!
Marekani must think watanzania ni mazezeta. Wamekazana kuimba wimbo wa afya ya mama na mtoto wakati huku nyuma wanachimba urani! Nilimsikiliza juzi balozi wa Marekani akitoa 'statistics' za jinsi afya mama na mtoto (maternal health) ilivyoimarika nchini (thanks to USA atataka watu waimbe hivyo), and it is shocking kwanza mtu kuja nyumbani kwako na kuanza kuongelea mambo ya mji wake tena outside the context halafu sisi tunapiga makofi.
Tanzania, kama zilizo nchi nyingi Africa, hatuhitaji misaada ya net za mbu, hatuhitaji vyakula vya jioni, hatuhitaji makongamano na nyimbo eti 'malaria no more'. Hivyo vitu vimo ndani ya uwezo wetu kama tutapata kodi toka kwa hawa hawa wanaotupa net za mbu.
Hili la Barrick ni kichefuchefu, na limekuja muda mfupi baada ya rais kufanya ziara ya kitaifa huko Canada. Ubalozi wa Canada Tanzania uko- downgraded, mambo mengi yanafanyiwa Nairobi, and that tells you nafasi ya Tanzania ni cash-cow as far as these Canadians are concerned. Hawachangii la maana hapa nchini, kuanzia bajeti ya kuu hadi kodi ya makampuni yao.
Nategemea bunge la bajeti litajidili hili. Waziri wa fedha anatakiwa atoe ufafanuzi kuhusu ukusanyaji kodi. Lakini wa Madini naye anatakiwa aeleze leseni zimetolewa kwa sheria ipi?