Ndugu zangu waislamu hii ni kweli!?

Ndugu zangu waislamu hii ni kweli!?

Hakuna Shida kwa Mwanaume wa Kiislam kufua, kupika pamoja na kufanya shughuli nyingine za Nyumbani lakin Mwanamke akimsaidia Mumewe inakuwa Bora zaidi na analipwa thawabu nyingi kutoka kwa Mola wake Mlezi
 
Nadhani si kweli maana sijaliona kwenye vitabu vya dini likizungumziwa hivyo
Bado kutokuliona wewe hakupelekei kutokuwapo

Usigeneralize kwa kuwa hukuliona

Soma kitabu cha Profesa Ibrahim Amin

Principles of the Marriage and family ethics kaelezea mengi kuhusu wajibu wa mwanamke kwa mumewe na wajibu wa mume kwa mkewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jukumu la mwanamume kumtunza mkewe sawa lakini sio lazima umfulie au umpikie, ila unaweza kufanya hivyo kuonyesha kuwa mapenzi yako ni makubwa sana juu yake, kumsaidia au kama anaumwa.
Ila kweli huyo jamaa ni "bwege", yaani kila kitu??, Hapana kwa kweli. Isije kuwa keshaekewa nyama kwenye "maungo"[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubwege kudhani kumfanzia ihsan mkeo ni jambo la utumwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nlivofika kibaruani asbh mjengoni baada ya kusain then maongez n colleagues kdg...

Kuna mzenji afsa mwenzangu uwa tunapenda kumtania kwmb yy kwa mkewe ni bwege coz uwa anamfanyia mkewe kila kitu ilhal mke wake yy ni kula, kunywa, choon, kuvaa n kupatiwa chchte anachohitaji ikiwemo kugegedwa pia tena ad afike peak....

Yaan mwanamke hapiki, hafui, wala kufanya lolote lile,

Sasa jana ile nlimuuliza iv ni kwel anavotuambiaga ivo!

Akadai ni kawaida kwa mwanaume wa kiislam akishaoa tu, yy (mwanaume) ndo ana jukum la kumtunza mwanamke ikiwa ni pa1 n kufanya kaz zte za ndan pa1 n mambo mengine ikiwemo kwnd sokon n kupika....

Ndugu zangu waislam ni kweli iyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hao wa VISIWANI wanasumbuliwa na WIVU TU...ila ni kweli MWANAMKE KAZI YAKE NI KUGEGEDWA TU....lakini haikuzungumzwa kuwa asifanye kazi za ndani.....Imeandikwa kuwa WANAWAKE NI MASHAMBA YENU...haipendezi DUME ZIMA LIFANYE SHUGHULI ZA NDNI...mwanamke ANAANGALIA SEARIES

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wekeni aya/verses, lasivyo tunadanganyana tu

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَ‌حْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُ‌ونَ

And of His signs is that He created for you from yourselves mates that you may find tranquillity in them; and He placed between you affection and mercy. Indeed in that are signs for a people who give thought.
(30:21)

“Men are the protectors/guardians and maintainers of women, because Allah has given the one more than the other, and because they support them from their means.Therefore/so the righteous women are devoutly obedient (to the husband), and guard in (the husband's) absence what Allah would have them guard. As to those women on whose part ye fear disloyalty and ill-conduct (nushuz), admonish them (first), (Next), refuse to share their beds, (And last) separate from them; but if they obey you, seek not against them Means (of annoyance): For Allah is Most High, great (above you all).”

(4:34)
 
Si kupika tu hata akikuzalia mtoto wakati wakumnyonyesha mtoto wako lazima umlipe ujira

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa:

“Let the women live (in 'iddat*) in the same style as ye live, according to your means: Annoy them not, so as to restrict them. And if they carry (life in their wombs), then spend (your substance) on them until they deliver their burden: and if they suckle your (offspring), give them their recompense: and take mutual counsel together, according to what is just and reasonable. And if ye find yourselves in difficulties, let another woman suckle (the child) on the (father's) behalf.”

(65:6)
 
Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻭَﻟَﻬُﻦَّ ﻣِﺜْﻞُ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺑِﺎﻟْﻤَﻌْﺮُﻭﻑِ ﻭَﻟِﻠﺮِّﺟَﺎﻝِ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺩَﺭَﺟَﺔٌ ﻭَﺍﻟﻠّﻪُ ﻋَﺰِﻳﺰٌ ﺣَﻜُﻴﻢٌ
Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah). Na kwa wanaume juu ya hao wanawake wana daraja . (Al-Baqara 2: 228)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Maswahaaba:
)) ﻳﺂ ﺃﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟﻨَّﺎﺱُ ﺇِﻥَّ ﻟِﻨِﺴَﺎﺋِﻜُﻢْ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢْ ﺣَﻘﺎً ﻭَﻟَﻜُﻢْ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺣَﻖّ (( ﺃﺑﻮ ﺩﺍﻭﺩ
((Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu)) Abu Daawuud
Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:
1-Ukweli
Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁَﻣَﻨُﻮﺍ ﺍﺗَّﻘُﻮﺍ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻭَﻛُﻮﻧُﻮﺍ ﻣَﻊَ ﺍﻟﺼَّﺎﺩِﻗِﻴﻦَ
Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli . (At-Tawbah: 11)
2-Mapenzi, huruma na utulivu.
Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻭَﻣِﻦْ ﺁﻳَﺎﺗِﻪِ ﺃَﻥْ ﺧَﻠَﻖَ ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦْ ﺃَﻧﻔُﺴِﻜُﻢْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟًﺎ
ﻟِّﺘَﺴْﻜُﻨُﻮﺍ ﺇِﻟَﻴْﻬَﺎ ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢ ﻣَّﻮَﺩَّﺓً ﻭَﺭَﺣْﻤَﺔ ًﺇِﻥَّ ﻓِﻲ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﺂ ﻳَﺎﺕٍ ﻟِّﻘَﻮْﻡٍ ﻳَﺘَﻔَﻜَّﺮُﻭﻥَ
“Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.” (Ar-Ruwm 30: 21)
3-Amana, Uaminifu na kutumiza ahadi:
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:
ﻭَﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻫُﻢْ ﻟِﺄَﻣَﺎﻧَﺎﺗِﻬِﻢْ ﻭَﻋَﻬْﺪِﻫِﻢْ ﺭَﺍﻋُﻮﻥَ
Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (wanazitimiza).
[Al-Muuminuwn 8] (Al-Ma’aarij: 32)
Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:
ﻓَﺈِﻥْ ﺃَﻣِﻦَ ﺑَﻌْﻀُﻜُﻢ ﺑَﻌْﻀًﺎ ﻓَﻠْﻴُﺆَﺩِّ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﺍﺅْﺗُﻤِﻦَ ﺃَﻣَﺎﻧَﺘَﻪُ ﻭَﻟْﻴَﺘَّﻖِ ﺍﻟﻠّﻪَ ﺭَﺑَّﻪُ
Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah Mola wake (Al-Baqarah: 283)
4-Tabia njema
Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:
ﻭَﻋَﺎﺷِﺮُﻭﻫُﻦَّ ﺑِﺎﻟْﻤَﻌْﺮُﻭﻑِ
Na kaeni nao kwa wema ((An-Nisaa 4: 19))
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:
((Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake)) Al-Bukhaariy na Muslim
5-Kuhifadhiana siri
Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake)) Muslim
Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
ﻭَﻻَ ﺗَﻨﺴَﻮُﺍْ ﺍﻟْﻔَﻀْﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢْ ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ ﺑِﻤَﺎ ﺗَﻌْﻤَﻠُﻮﻥَ ﺑَﺼِﻴﺮٌ
Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). (Al-Baqarah 2: 237)
Haki za mke kutoka kwa mume:
1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.
2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
ﻭَﺍﻟﻼَّﺗِﻲ ﺗَﺨَﺎﻓُﻮﻥَ ﻧُﺸُﻮﺯَﻫُﻦَّ ﻓَﻌِﻈُﻮﻫُﻦَّ ﻭَﺍﻫْﺠُﺮُﻭﻫُﻦَّ ﻓِﻲ ﺍﻟْﻤَﻀَﺎﺟِﻊِ ﻭَﺍﺿْﺮِﺑُﻮﻫُﻦَّ ﻓَﺈِﻥْ ﺃَﻃَﻌْﻨَﻜُﻢْ ﻓَﻼَ ﺗَﺒْﻐُﻮﺍْ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺳَﺒِﻴﻼً ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ ﻛَﺎﻥَ ﻋَﻠِﻴًّﺎ ﻛَﺒِﻴﺮًﺍ
Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa).
(An-Nisaa 4: 34)
Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu:
((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: “Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali” (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: “Ina maana mpigo usio wa nguvu”.
Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:
i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.
ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.
iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:
ﻋﻦ ﺟﺎﺑﺮ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : ﺃﻧﻪ ﻗﺎﻝ ﻓﻲ ﺣﺠﺔ ﺍﻟﻮﺩﺍﻉ : )) ﻭﺍﺗَّﻘُﻮﺍ ﺍﻟﻠﻪَ ﻓﻲ ﺍﻟﻨِّﺴﺎﺀِ، ﻓﺈﻧﻬﻦ ﻋﻨﺪﻛﻢ ﻋَﻮَﺍﻥٌ، ﻭﻟﻜﻢ ﻋﻠﻴﻬﻦ ﺃﻻ ﻳُﻮﻃِﺌْﻦَ ﻓُﺮُﺷﻜﻢ ﺃﺣﺪﺍ ﺗﻜﺮﻫﻮﻧﻪ، ﻓﺈﻥ ﻓَﻌَﻠْﻦ ﻓﺎﺿﺮﺑﻮﻫﻦ ﺿَﺮْﺑﺎ ﻏﻴﺮ ﻣُﺒَﺮِّﺡ، ﻭﻟﻬﻦ ﺭﺯْﻗُﻬﻦَّ ﻭﻛِﺴْﻮﺗﻬﻦ ﺑﺎﻟﻤﻌﺮﻭﻑ ((
Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha)) Muslim
3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa kama ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaamrisha hivyo:
ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁﻣَﻨُﻮﺍ ﻗُﻮﺍ ﺃَﻧﻔُﺴَﻜُﻢْ ﻭَﺃَﻫْﻠِﻴﻜُﻢْ ﻧَﺎﺭًﺍ ﻭَﻗُﻮﺩُﻫَﺎ ﺍﻟﻨَّﺎﺱُ ﻭَﺍﻟْﺤِﺠَﺎﺭَﺓُ ﻋَﻠَﻴْﻬَﺎ ﻣَﻠَﺎﺋِﻜَﺔٌ ﻏِﻠَﺎﻅٌ ﺷِﺪَﺍﺩٌ ﻟَّﺎ ﻳَﻌْﺼُﻮﻥَ ﺍﻟﻠَّـﻪَ ﻣَﺎ ﺃَﻣَﺮَﻫُﻢْ ﻭَﻳَﻔْﻌَﻠُﻮﻥَ ﻣَﺎ ﻳُﺆْﻣَﺮُﻭﻥَ ﴿٦﴾
Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.
(At Tahriym 66: 6)
4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.
5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:
ﺍﻟﺮِّﺟَﺎﻝُ ﻗَﻮَّﺍﻣُﻮﻥَ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀِ ﺑِﻤَﺎ ﻓَﻀَّﻞَ ﺍﻟﻠَّـﻪُ ﺑَﻌْﻀَﻬُﻢْ ﻋَﻠَﻰٰ ﺑَﻌْﺾٍ ﻭَﺑِﻤَﺎ ﺃَﻧﻔَﻘُﻮﺍ ﻣِﻦْ ﺃَﻣْﻮَﺍﻟِﻬِﻢْ ۚ
Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao . (An-Nisaa 4: 34)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake)) Al-Bukhaariy na Muslim
6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anakataza kutokufanya uadillifu:
ﻭَﻟَﻦ ﺗَﺴْﺘَﻄِﻴﻌُﻮﺍ ﺃَﻥ ﺗَﻌْﺪِﻟُﻮﺍ ﺑَﻴْﻦَ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀِ ﻭَﻟَﻮْ ﺣَﺮَﺻْﺘُﻢْ ۖ ﻓَﻠَﺎ ﺗَﻤِﻴﻠُﻮﺍ ﻛُﻞَّ ﺍﻟْﻤَﻴْﻞِ ﻓَﺘَﺬَﺭُﻭﻫَﺎ ﻛَﺎﻟْﻤُﻌَﻠَّﻘَﺔِ ۚ
Na wala hamtaweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msielemee muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mke mwengine (msiyempenda) kama kining’inio (aliyetundikwa). (An-Nisaa 4: 129)
Na Anasema:
ﻓَﺈِﻥْ ﺧِﻒ ْﺗُﻢْ ﺃَﻻَّ ﺗَﻌْﺪِﻟُﻮﺍْ ﻓَﻮَﺍﺣِﺪَﺓً ﺃَﻭْ ﻣَﺎ ﻣَﻠَﻜَﺖْ ﺃَﻳْﻤَﺎﻧُﻜُﻢْ ﺫَﻟِﻚَ ﺃَﺩْﻧَﻰ ﺃَﻻَّ ﺗَﻌُﻮﻟُﻮﺍْ
Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki (masuriya). Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea (kudhulumu). (An-Nisaa 4: 3)
Juu ya hivyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:
((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu)) At-Twabaraaniy
Haki za Mume kutoka kwa Mke:
1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:
)) ﻟَﻮْ ﻛُﻨْﺖُ ﺁﻣِﺮﺍً ﺃَﺣَﺪﺍً ﺃَﻥْ ﻳَﺴْﺠُﺪَ ﻷِﺣَﺪٍ ﻷَﻣَﺮْﺕُ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓَ ﺃَﻥْ ﺗَﺴْﺠُﺪَ ﻟِﺰَﻭْﺟِﻬَﺎ ﻣِﻦْ ﻋِﻈَﻢِ ﺣَﻘَّﻪِ ﻋَﻠَﻴْﻬﺎَ ((
((Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake))
Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr
2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:
)) ﺇﺫﺍ ﺩَﻋَﺎ ﺍﻟﺮَّﺟُﻞُ ﺍﻣْﺮَﺃﺗَﻪُ ﺇِﻟﻰَ ﻓِﺮَﺍﺷِﻪِ ﻓَﺄَﺑَﺖْ ﻋَﻠَﻴْﻪ ﻟَﻌَﻨَﺘْﻬَﺎ ﺍﻟْﻤَﻼﺋِﻜَﺔُ ﺣَﺘَّﻰ ﺗُﺼْﺒِﺢَ ((
((Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi)) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy
3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
)) ﻻَ ﺗُﻨْﻔِﻖُ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﺷَﻴْﺌًﺎ ﻣِﻦْ ﺑَﻴْﺘِﻬَﺎ ﺇِﻻ ﺑِﺈِﺫْﻥِ ﺯَﻭْﺟِﻬَﺎ (( ﻗﺎﻟﻮﺍ : " ﻳﺎ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ! ﻭَﻻ ﺍﻟﻄَّﻌَﺎﻡَ؟ ﻗﺎﻝ : )) ﺫَﺍﻙَ ﺃَﻓْﻀَﻞُ ﺃَﻣْﻮَﺍﻟِﻨَﺎ (( ﺻﺤﻴﺢ ﺍﺑﻦ ﻣﺎﺟﻪ - ﺣﺪﻳﺚ ﺣﺴﻦ
ﺍﻷﻟﺒﺎﻧﻲ
((Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe)). Wakasema: “Hata chakula ee Mtume wa Allaah”? Akasema: ((Hicho ni mali bora yetu)). Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.
Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe.
Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:
ﻋﻦ ﻫﻤﺎﻡ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻗﺎﻝ : ﺳﻤﻌﺖ ﺃﺑﺎ ﻫﺮﻳﺮﺓ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﻗﺎﻝ : )) ﺇِﺫَﺍ ﺃَﻧْﻔَﻘَﺖِ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﻣِﻦْ ﻛَﺴْﺐِ ﺯَﻭْﺟِﻬَﺎ ﻋَﻦْ ﻏَﻴْﺮِ ﺃَﻣْﺮِﻩِ ﻓَﻠَﻪُ ﻧِﺼْﻒُ ﺃَﺟْﺮِﻩِ (( - ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
Kutoka kwa Hamaam (Radhiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake))
Al-Bukhaariy
4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).
5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi:
ﻋﻦ ﻋﺒﺪ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﺑﻦ ﻋﻮﻑ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻗﺎﻝ : ﻗﺎﻝ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : )) ﺇِﺫَﺍ ﺻَﻠَّﺖْ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﺧَﻤْﺴَﻬَﺎ، ﻭَﺻَﺎﻣَﺖْ ﺷَﻬْﺮَﻫَﺎ، ﻭَﺣَﻔِﻈَﺖْ ﻓَﺮْﺟَﻬَﺎ، ﻭَﺃَﻃَﺎﻋَﺖْ ﺯَﻭْﺟَﻬَﺎ , ﻗِﻴﻞَ ﻟَﻬَﺎ : ﺍﺩْﺧُﻠِﻲ ﻣِﻦْ ﺃَﻱِّ ﺃَﺑْﻮَﺍﺏِ ﺍﻟْﺠَﻨَّﺔِ ﺷِﺌْﺖِ (( ﺻﺤﻴﺢ ﺍﻟﺘﺮﻏﻴﺐ
Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao)) Swahiyh at-Targhiyb

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa:

“Let the women live (in 'iddat*) in the same style as ye live, according to your means: Annoy them not, so as to restrict them. And if they carry (life in their wombs), then spend (your substance) on them until they deliver their burden: and if they suckle your (offspring), give them their recompense: and take mutual counsel together, according to what is just and reasonable. And if ye find yourselves in difficulties, let another woman suckle (the child) on the (father's) behalf.”

(65:6)
Hivi hakuna Quran ya kiswahili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa wanaume na wanawake wako sawa katika uhusiano na Kristo, maandiko yanatoa majukumu maalum kwa kila mmoja katika ndoa. Mume anapaswa kuchukua uongozi katika boma (1 Wakorintho 11:3, Waefeso 5:23). Uongozi huu usiwe wa kihimla, kukandamisa, au shupavu kwa mke, lakini lazima iwe kwa mujibu wa mfano wa Kristo kuongoza kanisa. "Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neon" (Waefeso 5:25-26). Kristo alivyolipenda kanisa (watu wake) na huruma, rehema, msamaha, heshima, na kutokuwa na ubinafsi. Kwa njia hiyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao.
Wake wanapaswa kunyenyekea kwa mamlaka ya waume zao. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili wake. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo" (Waefeso 5:22-24). Ingawa wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa waume zao, Biblia pia anawaambia wanaume mara kadhaa jinsi wanatakiwa kuwafanyia wake zao. Mume hapaswi kuchukua nafasi ya kiihimla, lakini wanapaswa kuonyesha heshima kwa mke wake na maoni yake. Kwa kweli, Waefeso 5:28-29 anawahimiza watu kuwapenda wake zao katika njia sawa wanavyoipenda miili yao wenyewe, kuwalisha na kuwatunza. Upendo wa mume kwa mke wake unapaswa kuwa sawa na upendo wa Kristo kwa mwili wake, kanisa.
"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi Waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao "(Wakolosai 3:18-19). "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpamke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (1 Petro 3: 7). Kutokana na mistari hii tunaona kwamba upendo na heshima ni sifa ya majukumu ya waume wote na wake. Kama haya yapo katika ndoa, basi mamlaka, uongozi, upendo, na kunyenyekea hakutakuwa na tatizo kwa mpenzi yeyote.
Kuhusiana na suala la mgao wa majukumu katika boma, Biblia inawaamuru waume kukimu familia zao. Hii ina maana kuwa anafanya kazi na kupata fedha za kutosha kukimu mahitaji yote ya maisha kwa mke na watoto wake. Kwa kushindwa kufanya hivyo ina madhara maalum ya kiroho. "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa numbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini" (1 Timotheo 5:8). Hivyo, mume ambaye hafanyi juhudi za kukimu mahitaji ya familia yake haiwezi kujiita Mkristo halisi. Hii haimaanishi kwamba mke hawezi eza katika kusaidia familia Mithali 31 inaonyesha kuwa mke mcha Mungu anaweza hakika kufanya hivyo-lakini kukimi familia si hasa wajibu wake; ni wa mume wake. Wakati mume anasaidia kutayarisha watoto na kufanya kazi za nyumbani (hivyo kutimiza wajibu wake wa kumpenda mke wake),

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naanza kukuelewa mukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukipata fursa ya kuonyesha mahaba mazito kwa mwenza wako muonyeshe tuuu

Kama ikitokea kusigana kwa kumfanzia wema basi huna lawama Mkuuu maana mioyo iliyokosa shukran huwa na Tabia ya kukanusha Neema zote


Muhim unafanya ukitegemea kupata Baraka za mola wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom