Ndugu zangu waislamu hii ni kweli!?

Ndugu zangu waislamu hii ni kweli!?

Kusaidiana ni wajibu kwa wanandoa but haimaanishi kuwa mke akae tu miguu juu ya meza anaangalia tv then mume ndo afanye kazi za home...huyo mzenji kapagawa sio bure kuwa hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna mchanganyiko wa majibu but zaidi nimeona majibu ya Hadithi pekee na sio Koran
 
Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻭَﻟَﻬُﻦَّ ﻣِﺜْﻞُ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺑِﺎﻟْﻤَﻌْﺮُﻭﻑِ ﻭَﻟِﻠﺮِّﺟَﺎﻝِ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺩَﺭَﺟَﺔٌ ﻭَﺍﻟﻠّﻪُ ﻋَﺰِﻳﺰٌ ﺣَﻜُﻴﻢٌ
Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah). Na kwa wanaume juu ya hao wanawake wana daraja . (Al-Baqara 2: 228)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Maswahaaba:
)) ﻳﺂ ﺃﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟﻨَّﺎﺱُ ﺇِﻥَّ ﻟِﻨِﺴَﺎﺋِﻜُﻢْ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢْ ﺣَﻘﺎً ﻭَﻟَﻜُﻢْ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺣَﻖّ (( ﺃﺑﻮ ﺩﺍﻭﺩ
((Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu)) Abu Daawuud
Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:
1-Ukweli
Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁَﻣَﻨُﻮﺍ ﺍﺗَّﻘُﻮﺍ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻭَﻛُﻮﻧُﻮﺍ ﻣَﻊَ ﺍﻟﺼَّﺎﺩِﻗِﻴﻦَ
Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli . (At-Tawbah: 11)
2-Mapenzi, huruma na utulivu.
Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Anasema:
ﻭَﻣِﻦْ ﺁﻳَﺎﺗِﻪِ ﺃَﻥْ ﺧَﻠَﻖَ ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦْ ﺃَﻧﻔُﺴِﻜُﻢْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟًﺎ
ﻟِّﺘَﺴْﻜُﻨُﻮﺍ ﺇِﻟَﻴْﻬَﺎ ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢ ﻣَّﻮَﺩَّﺓً ﻭَﺭَﺣْﻤَﺔ ًﺇِﻥَّ ﻓِﻲ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﺂ ﻳَﺎﺕٍ ﻟِّﻘَﻮْﻡٍ ﻳَﺘَﻔَﻜَّﺮُﻭﻥَ
“Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.” (Ar-Ruwm 30: 21)
3-Amana, Uaminifu na kutumiza ahadi:
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:
ﻭَﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻫُﻢْ ﻟِﺄَﻣَﺎﻧَﺎﺗِﻬِﻢْ ﻭَﻋَﻬْﺪِﻫِﻢْ ﺭَﺍﻋُﻮﻥَ
Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (wanazitimiza).
[Al-Muuminuwn 8] (Al-Ma’aarij: 32)
Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:
ﻓَﺈِﻥْ ﺃَﻣِﻦَ ﺑَﻌْﻀُﻜُﻢ ﺑَﻌْﻀًﺎ ﻓَﻠْﻴُﺆَﺩِّ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﺍﺅْﺗُﻤِﻦَ ﺃَﻣَﺎﻧَﺘَﻪُ ﻭَﻟْﻴَﺘَّﻖِ ﺍﻟﻠّﻪَ ﺭَﺑَّﻪُ
Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah Mola wake (Al-Baqarah: 283)
4-Tabia njema
Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:
ﻭَﻋَﺎﺷِﺮُﻭﻫُﻦَّ ﺑِﺎﻟْﻤَﻌْﺮُﻭﻑِ
Na kaeni nao kwa wema ((An-Nisaa 4: 19))
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:
((Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake)) Al-Bukhaariy na Muslim
5-Kuhifadhiana siri
Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake)) Muslim
Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
ﻭَﻻَ ﺗَﻨﺴَﻮُﺍْ ﺍﻟْﻔَﻀْﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢْ ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ ﺑِﻤَﺎ ﺗَﻌْﻤَﻠُﻮﻥَ ﺑَﺼِﻴﺮٌ
Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). (Al-Baqarah 2: 237)
Haki za mke kutoka kwa mume:
1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.
2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
ﻭَﺍﻟﻼَّﺗِﻲ ﺗَﺨَﺎﻓُﻮﻥَ ﻧُﺸُﻮﺯَﻫُﻦَّ ﻓَﻌِﻈُﻮﻫُﻦَّ ﻭَﺍﻫْﺠُﺮُﻭﻫُﻦَّ ﻓِﻲ ﺍﻟْﻤَﻀَﺎﺟِﻊِ ﻭَﺍﺿْﺮِﺑُﻮﻫُﻦَّ ﻓَﺈِﻥْ ﺃَﻃَﻌْﻨَﻜُﻢْ ﻓَﻼَ ﺗَﺒْﻐُﻮﺍْ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻦَّ ﺳَﺒِﻴﻼً ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠّﻪَ ﻛَﺎﻥَ ﻋَﻠِﻴًّﺎ ﻛَﺒِﻴﺮًﺍ
Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa).
(An-Nisaa 4: 34)
Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu:
((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: “Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali” (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: “Ina maana mpigo usio wa nguvu”.
Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:
i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.
ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.
iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:
ﻋﻦ ﺟﺎﺑﺮ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : ﺃﻧﻪ ﻗﺎﻝ ﻓﻲ ﺣﺠﺔ ﺍﻟﻮﺩﺍﻉ : )) ﻭﺍﺗَّﻘُﻮﺍ ﺍﻟﻠﻪَ ﻓﻲ ﺍﻟﻨِّﺴﺎﺀِ، ﻓﺈﻧﻬﻦ ﻋﻨﺪﻛﻢ ﻋَﻮَﺍﻥٌ، ﻭﻟﻜﻢ ﻋﻠﻴﻬﻦ ﺃﻻ ﻳُﻮﻃِﺌْﻦَ ﻓُﺮُﺷﻜﻢ ﺃﺣﺪﺍ ﺗﻜﺮﻫﻮﻧﻪ، ﻓﺈﻥ ﻓَﻌَﻠْﻦ ﻓﺎﺿﺮﺑﻮﻫﻦ ﺿَﺮْﺑﺎ ﻏﻴﺮ ﻣُﺒَﺮِّﺡ، ﻭﻟﻬﻦ ﺭﺯْﻗُﻬﻦَّ ﻭﻛِﺴْﻮﺗﻬﻦ ﺑﺎﻟﻤﻌﺮﻭﻑ ((
Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha)) Muslim
3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa kama ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaamrisha hivyo:
ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁﻣَﻨُﻮﺍ ﻗُﻮﺍ ﺃَﻧﻔُﺴَﻜُﻢْ ﻭَﺃَﻫْﻠِﻴﻜُﻢْ ﻧَﺎﺭًﺍ ﻭَﻗُﻮﺩُﻫَﺎ ﺍﻟﻨَّﺎﺱُ ﻭَﺍﻟْﺤِﺠَﺎﺭَﺓُ ﻋَﻠَﻴْﻬَﺎ ﻣَﻠَﺎﺋِﻜَﺔٌ ﻏِﻠَﺎﻅٌ ﺷِﺪَﺍﺩٌ ﻟَّﺎ ﻳَﻌْﺼُﻮﻥَ ﺍﻟﻠَّـﻪَ ﻣَﺎ ﺃَﻣَﺮَﻫُﻢْ ﻭَﻳَﻔْﻌَﻠُﻮﻥَ ﻣَﺎ ﻳُﺆْﻣَﺮُﻭﻥَ ﴿٦﴾
Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.
(At Tahriym 66: 6)
4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.
5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:
ﺍﻟﺮِّﺟَﺎﻝُ ﻗَﻮَّﺍﻣُﻮﻥَ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀِ ﺑِﻤَﺎ ﻓَﻀَّﻞَ ﺍﻟﻠَّـﻪُ ﺑَﻌْﻀَﻬُﻢْ ﻋَﻠَﻰٰ ﺑَﻌْﺾٍ ﻭَﺑِﻤَﺎ ﺃَﻧﻔَﻘُﻮﺍ ﻣِﻦْ ﺃَﻣْﻮَﺍﻟِﻬِﻢْ ۚ
Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao . (An-Nisaa 4: 34)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake)) Al-Bukhaariy na Muslim
6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anakataza kutokufanya uadillifu:
ﻭَﻟَﻦ ﺗَﺴْﺘَﻄِﻴﻌُﻮﺍ ﺃَﻥ ﺗَﻌْﺪِﻟُﻮﺍ ﺑَﻴْﻦَ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀِ ﻭَﻟَﻮْ ﺣَﺮَﺻْﺘُﻢْ ۖ ﻓَﻠَﺎ ﺗَﻤِﻴﻠُﻮﺍ ﻛُﻞَّ ﺍﻟْﻤَﻴْﻞِ ﻓَﺘَﺬَﺭُﻭﻫَﺎ ﻛَﺎﻟْﻤُﻌَﻠَّﻘَﺔِ ۚ
Na wala hamtaweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msielemee muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mke mwengine (msiyempenda) kama kining’inio (aliyetundikwa). (An-Nisaa 4: 129)
Na Anasema:
ﻓَﺈِﻥْ ﺧِﻒ ْﺗُﻢْ ﺃَﻻَّ ﺗَﻌْﺪِﻟُﻮﺍْ ﻓَﻮَﺍﺣِﺪَﺓً ﺃَﻭْ ﻣَﺎ ﻣَﻠَﻜَﺖْ ﺃَﻳْﻤَﺎﻧُﻜُﻢْ ﺫَﻟِﻚَ ﺃَﺩْﻧَﻰ ﺃَﻻَّ ﺗَﻌُﻮﻟُﻮﺍْ
Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki (masuriya). Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea (kudhulumu). (An-Nisaa 4: 3)
Juu ya hivyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:
((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu)) At-Twabaraaniy
Haki za Mume kutoka kwa Mke:
1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:
)) ﻟَﻮْ ﻛُﻨْﺖُ ﺁﻣِﺮﺍً ﺃَﺣَﺪﺍً ﺃَﻥْ ﻳَﺴْﺠُﺪَ ﻷِﺣَﺪٍ ﻷَﻣَﺮْﺕُ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓَ ﺃَﻥْ ﺗَﺴْﺠُﺪَ ﻟِﺰَﻭْﺟِﻬَﺎ ﻣِﻦْ ﻋِﻈَﻢِ ﺣَﻘَّﻪِ ﻋَﻠَﻴْﻬﺎَ ((
((Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake))
Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr
2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:
)) ﺇﺫﺍ ﺩَﻋَﺎ ﺍﻟﺮَّﺟُﻞُ ﺍﻣْﺮَﺃﺗَﻪُ ﺇِﻟﻰَ ﻓِﺮَﺍﺷِﻪِ ﻓَﺄَﺑَﺖْ ﻋَﻠَﻴْﻪ ﻟَﻌَﻨَﺘْﻬَﺎ ﺍﻟْﻤَﻼﺋِﻜَﺔُ ﺣَﺘَّﻰ ﺗُﺼْﺒِﺢَ ((
((Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi)) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy
3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
)) ﻻَ ﺗُﻨْﻔِﻖُ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﺷَﻴْﺌًﺎ ﻣِﻦْ ﺑَﻴْﺘِﻬَﺎ ﺇِﻻ ﺑِﺈِﺫْﻥِ ﺯَﻭْﺟِﻬَﺎ (( ﻗﺎﻟﻮﺍ : " ﻳﺎ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ! ﻭَﻻ ﺍﻟﻄَّﻌَﺎﻡَ؟ ﻗﺎﻝ : )) ﺫَﺍﻙَ ﺃَﻓْﻀَﻞُ ﺃَﻣْﻮَﺍﻟِﻨَﺎ (( ﺻﺤﻴﺢ ﺍﺑﻦ ﻣﺎﺟﻪ - ﺣﺪﻳﺚ ﺣﺴﻦ
ﺍﻷﻟﺒﺎﻧﻲ
((Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe)). Wakasema: “Hata chakula ee Mtume wa Allaah”? Akasema: ((Hicho ni mali bora yetu)). Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.
Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe.
Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:
ﻋﻦ ﻫﻤﺎﻡ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻗﺎﻝ : ﺳﻤﻌﺖ ﺃﺑﺎ ﻫﺮﻳﺮﺓ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﻗﺎﻝ : )) ﺇِﺫَﺍ ﺃَﻧْﻔَﻘَﺖِ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﻣِﻦْ ﻛَﺴْﺐِ ﺯَﻭْﺟِﻬَﺎ ﻋَﻦْ ﻏَﻴْﺮِ ﺃَﻣْﺮِﻩِ ﻓَﻠَﻪُ ﻧِﺼْﻒُ ﺃَﺟْﺮِﻩِ (( - ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ
Kutoka kwa Hamaam (Radhiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake))
Al-Bukhaariy
4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).
5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi:
ﻋﻦ ﻋﺒﺪ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﺑﻦ ﻋﻮﻑ ‏( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ ‏) ﻗﺎﻝ : ﻗﺎﻝ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ : )) ﺇِﺫَﺍ ﺻَﻠَّﺖْ ﺍﻟْﻤَﺮْﺃَﺓُ ﺧَﻤْﺴَﻬَﺎ، ﻭَﺻَﺎﻣَﺖْ ﺷَﻬْﺮَﻫَﺎ، ﻭَﺣَﻔِﻈَﺖْ ﻓَﺮْﺟَﻬَﺎ، ﻭَﺃَﻃَﺎﻋَﺖْ ﺯَﻭْﺟَﻬَﺎ , ﻗِﻴﻞَ ﻟَﻬَﺎ : ﺍﺩْﺧُﻠِﻲ ﻣِﻦْ ﺃَﻱِّ ﺃَﺑْﻮَﺍﺏِ ﺍﻟْﺠَﻨَّﺔِ ﺷِﺌْﺖِ (( ﺻﺤﻴﺢ ﺍﻟﺘﺮﻏﻴﺐ
Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao)) Swahiyh at-Targhiyb

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeipenda sana hii be bleesed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa wanaume na wanawake wako sawa katika uhusiano na Kristo, maandiko yanatoa majukumu maalum kwa kila mmoja katika ndoa. Mume anapaswa kuchukua uongozi katika boma (1 Wakorintho 11:3, Waefeso 5:23). Uongozi huu usiwe wa kihimla, kukandamisa, au shupavu kwa mke, lakini lazima iwe kwa mujibu wa mfano wa Kristo kuongoza kanisa. "Enyi wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neon" (Waefeso 5:25-26). Kristo alivyolipenda kanisa (watu wake) na huruma, rehema, msamaha, heshima, na kutokuwa na ubinafsi. Kwa njia hiyo waume wanapaswa kuwapenda wake zao.
Wake wanapaswa kunyenyekea kwa mamlaka ya waume zao. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili wake. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo" (Waefeso 5:22-24). Ingawa wanawake wanapaswa kunyenyekea kwa waume zao, Biblia pia anawaambia wanaume mara kadhaa jinsi wanatakiwa kuwafanyia wake zao. Mume hapaswi kuchukua nafasi ya kiihimla, lakini wanapaswa kuonyesha heshima kwa mke wake na maoni yake. Kwa kweli, Waefeso 5:28-29 anawahimiza watu kuwapenda wake zao katika njia sawa wanavyoipenda miili yao wenyewe, kuwalisha na kuwatunza. Upendo wa mume kwa mke wake unapaswa kuwa sawa na upendo wa Kristo kwa mwili wake, kanisa.
"Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi Waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao "(Wakolosai 3:18-19). "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpamke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (1 Petro 3: 7). Kutokana na mistari hii tunaona kwamba upendo na heshima ni sifa ya majukumu ya waume wote na wake. Kama haya yapo katika ndoa, basi mamlaka, uongozi, upendo, na kunyenyekea hakutakuwa na tatizo kwa mpenzi yeyote.
Kuhusiana na suala la mgao wa majukumu katika boma, Biblia inawaamuru waume kukimu familia zao. Hii ina maana kuwa anafanya kazi na kupata fedha za kutosha kukimu mahitaji yote ya maisha kwa mke na watoto wake. Kwa kushindwa kufanya hivyo ina madhara maalum ya kiroho. "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa numbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini" (1 Timotheo 5:8). Hivyo, mume ambaye hafanyi juhudi za kukimu mahitaji ya familia yake haiwezi kujiita Mkristo halisi. Hii haimaanishi kwamba mke hawezi eza katika kusaidia familia Mithali 31 inaonyesha kuwa mke mcha Mungu anaweza hakika kufanya hivyo-lakini kukimi familia si hasa wajibu wake; ni wa mume wake. Wakati mume anasaidia kutayarisha watoto na kufanya kazi za nyumbani (hivyo kutimiza wajibu wake wa kumpenda mke wake),

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana kwa kutujuza mema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nikamalizie mada ya "WANAUME MAMWINYI" ntakuja kuchangia ninachojua.


Ijapokuwa Biblia inatuambia MWANAMKE NI MSAIDIZI wa mwanaume.

Neno "Msaidizi"????

Narudiii
na wanawasaidia mpaka wanakua kama vijakazi , mpaka raha inakwisha, alime yeye , alishe ng'ombe yeye, auze maziwa yeye, mwanaume analewa tu , na usiku mume ampande, sisi hatufanyi udhalilishaji huo, uislam unalinda haki za mwanaumke, ndio maana wake zetu wananukia udi , wanajua starahm kibaoo
 
na wanawasaidia mpaka wanakua kama vijakazi , mpaka raha inakwisha, alime yeye , alishe ng'ombe yeye, auze maziwa yeye, mwanaume analewa tu , na usiku mume ampande, sisi hatufanyi udhalilishaji huo, uislam unalinda haki za mwanaumke, ndio maana wake zetu wananukia udi , wanajua starahm kibaoo
Unaona umeshaanza usebusebu?

Wacha kuuongelea vibaya Ukristo

Kuna udhalilishaji mkubwa kama ule alioufanya mudy wa kumpanda na kumbaka mtoto Aisha mwenye miaka 9 tu na kufanywa Mke?

Kuna udhalilishaji mkubwa kama wa kuoa Wanawake rundo? Ilhali hata wao wenyewe huwa hawapendi kuletewa wake wenza?

Kuna udhalilishaji mkubwa kama wa kusema eti "Kazi ya Mke ni kugegedwa tu na Kuzaa? " [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Yaani wao wapo kama chombo cha starehe tu ama incubator ya kujazwa manii na kuzaa tu?


Wabillah Tawfiq,
 
na wanawasaidia mpaka wanakua kama vijakazi , mpaka raha inakwisha, alime yeye , alishe ng'ombe yeye, auze maziwa yeye, mwanaume analewa tu , na usiku mume ampande, sisi hatufanyi udhalilishaji huo, uislam unalinda haki za mwanaumke, ndio maana wake zetu wananukia udi , wanajua starahm kibaoo
Huo Oud unavutiaga majini...na hao majini huwa wanawafaidi..Ashakum si matusi.
 
Mwanamke si kijakazi mwanamke malkia wa nyumba mwanamke ni mlezi wa nyumba yake

Mtume alikuwa akiwasadia wakeze kupika lakini hakuwa anakubali muda wa ibada ya sala unapofika


Maisha tuuu ndio hufifisha mahaba haya inalazimika kupeana majukum

Ingawa bado yatupasa kuwahudumikia kwa dhati ya haki


Sent using Jamii Forums mobile app
Msidanganye watu.... Mtume saw hakuwa na muda wa kupika kama alifanya ni mara moja moja sana ... Ni kweli kwamba sheria haimlazimishi mwanamke wa kiislam kumpikia na kumfulia mumewe lakini wanawake wa kisahaba walikuwa wakifanya zaidi ya hayo kuonyesha mapenzi Kwa waume zao.... Sema wanawake wa kiunguja ni wavivu na wakipata dume bwege kama hilo ndo kabisaaa. Ila sheria haikurusu kuvidai hivyo vitu Ila inatarajiwa kutokana na mapenzi atakufanyia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekua islamic nngefanya ivo! Au j3 ntaenda kuuliza kwa aletuambia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila atakachokifanya mkeo kwako ni kwa mapenzi yake tuu. Ila si lazima kila kitu utawajibika wewe mwanaume ulie muoa. Na nikwakuwa mkeo c mjakazi wako ispokuwa ni kwa kazi moja tuu uliemuolea. Basi zingine zote afanye kwa kupenda mpka kufua na kupika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom