Habari zenu GT.
Nmetumiwa sasa hivi taarifa na ndugu yangu amempata mchumba kupitia hii mitandao kua amesoma profile yake na amegundua ni mtu makini. Sasa kilichotokea huyo mchumba ni wakike amemwambia asitoe siri maana atamtumia $ million kadhaa katika acount yake...halafu achukue kidogo amtumie kwa ajili ya safari ili amfuate alipo!
Je inawezekana au ndugu yangu wanataka kumwibia?
Maana mchumba mwenyewe yuko Senegal!
Namuwakilisha!
mwacheni aibiwe kidogo tuu atatusimulia na sisi!
<br />Teh teh teh teh! Kweli ng'ombe hawawezi kuisha hata wachinjwe vipi
kifulambute nimependa meseji ya avater yako.
Hii hunisumbua sana! Ukijua a/c ya mtu inahamishwa vipi?akituma hiyo account # jamaa wana uwezo wa kuchota hela huko walipo. muambie ndugu yako aache kupenda dezo jamani, sasa uchumba na kutumiana hela vinahusianaje?isee, nisije nikasema neno baya.
<br />"UKIONA UMEKULA, UJUWE UMELIWA".... by Mrisho Mpoto
Hiyo tabia ya kutumia third part inazidi kuota mizizi hapa JF.Ni mwenzio au wewe mwenyewe...acha kutuzuga bhana