Kama jamaa yako hana bank overdraft kwenye acc.yake mwambie a test zali hilo manake watakuta acc. tupu and u cant overdraft any ammount....ila kama anaruhusiwa kuoverdraft, itakula kwake manake jamaa watanunua kitu online then mahesabu wanaoverdraft acc. ya jamaa yako. Just saying....
Maalim Jumar?
mbona unatuangusha?
Hadi sasa umesha-post 1016 topics lkn hauna ujanja ktk masuala ya kwny matandao?
I have more than 5 yrs experience vising these bullshit websites, kuna baadhi ya watu ni wakweli - very, very few of them!
Mi' nina rafiki zangu wawili wa USA hadi sasa tunawasiliana nao kwa masuala ya kawaida kabisa for over 4 year!
Lkn nimekumbana na scammers zaidi ya 1,000 toka nianze kuvisit mawebsite hayo!
Kwa kifupi tu visit:
afrikadating.com
badoo.com
Hizo ni website chache kati ya lukuki zenye vichwa vya ajabu ajabu vingi!
Watchout these countries:
Senegal
Nigeria
Ghana,
Cameroon,
Kwa kifupi WEST AFRICAN COUNTRIES
Kenya.
Tena ukiwa makini unaweza hata ukagundua kwa kuangalia vitu vingi vidigovidogo:
English anayotumia kukuandikia au aliyoandika kwny profile yake
Mahali/ nchi aliyosema anaishi inaweza kuwa tofauti na nchi aliyo-log in. n.k, n.k
Kuna jamaa yangu alitaka kuliwa, akaniambia: "Kuna Sister wa kanisa fulani yuko Nigeria anasema ameona mimi nd'o mtu ambaye naweza kusaidia watoto yatima so atanitumia mamia ya mamilioni ili niweze kuwasaidia watoto, lkn amesema nisimwambie mtu yeyote kwa sababu watu wana wivu wanaweza kuniharibia na pia anaumwa ugonjwa ambao anaweza akafariki muda wowote hivyo nifanye haraka!". Nikamwambia: "Mwanangu utaliwa, sasa yeye si mjanja?! Nenda naye tu taratibu ujifanye **** na ujifanye umezishobokea hizo pesa lkn usimpatie account number yako, password au pin number zako za kadi za benki, email n.k. Baadaye utashangaa anaomba utume pesa kwa kisingizio kuwa ili pesa itoke inabidi either uende ukasaini cheque au mwanasheria wa huko ambaye atamchagua yeye asaini kwa ajili yako. Na kwa sabau huwezi kwenda uta-opt kusainiwa na mwanasheria; ukishasema mwanasheria asaini kwa ajili yako atakuambia inatakiwa pesa kidogo tu hata 100,000, hapo nd'o utaamini ninakuambia nini.". Jamaa aliendelea naye, baadaye si akaombwa pesa kama nilivyomwambia!
Kutokana na maujanja niliyompatia akawambia: "Yaani hapa nilipo sina kitu, ninachoomba ni kwamba unikopeshe nilipie hiyo pesa kwa ajili ya mwanasheria then pesa ikitoka uta-deduct, hata uki-deduct mara 5 ya hiyo inayotakiwa kumlipa mwanasheria sawa tu - mimi ninachotaka ni kusadia hawa watoto na ninashukuru kwa kuniona mimi nd'o ninayefaa kwa hilo. Naomba SANA unifikirie kwa hilo. I expect to hear from you soon". Kwani unafikiri alimjibu tena!
Au labda alikufa kweli kutokana na ugonjwa aliokuwa nao, nd'o maana hakumjibu mshikaji wangu? Tehe, tehe, teheeee - watch out!
Mwingine ukimuomba namba ya simu anasita kwa sababu utastukia code number ya simu.
Wapo wengine waliobobea, huwa wanadanganya wako Ulaya au marekani baadaye anakuambia ataenda kufanya tour West Africa na kukupatia namba ya simu yenye code za West Africa (Senegal, Ghana, Nigeia ......), ujue umeliwa tayari. Na kwa experience niliyonayo inawezekana pia mtu akawa yuko Ulaya, Marekani na akaja West Africa au hata asije West Africa na akawa bado anafanya utapeli huo.
Na wengine wana network, unaweza kukuta akakupatia namba ya mshikaji wake wa Ulaya, Marekani et.c, baadaye unaambiwa anaenda West Africa na anakupatia no. ya simu yenye code number za West Africa, tayari unaendea kuliwa!
Nisiongee sana, niwaachie na wengine! (YAMENIKUTA)
Ukiona kitu kinataka kuja kiurahisi kuliko kawaida - THINK TWICE!