TRA wana jambo lao, Sio kwa watu maarufu tu, ndugu yangu alieanza biashara 2015 kwa mara ya kwanza kapigwa faini nzito ya kukwepa kodi,

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Nimejiridhisha kwamba kwa sasa TRA wana jambo lao kwa wakwepa kodi maana si kwa kelele hizi, wakiona unakwepa wanapita na wewe.

Mwezi uliopitwa nilipatwa na simanzi baada ya kuona ndugu yangu kapatwa na pigo zito la kulipa faini ya TRA, masikitiko yake yamenigusa na mwanzoni nilidhani kaonewa lakini hali ni tofauti.

Hawa kina diamond na huyo pck wanaolalamika ni kwasababu ni maarufu ndio maana wanasikika lakini wakae wakijua sio wao tu, hii ni operation kubwa sana iliyonasa wengi tena kihalali bila uonevu wala mabavu.

Binafsi nina ndugu yangu alianza biashara kwenye mwaka 2015 hivi, Enzi hizo Magu kaingia na msisitizo watu watoe risiti kwa mashine, hapa waliokuwa hawana mashine ndio walikiona cha mtemakuni, kukwepa huu mhaho wengi ilibidi wanunue hizo mashine ila wakawa wanatoa risiti chache za kuzugia, ila kwa sasa hali ni tofauti kabisa, hio style ya kutoa risiti za kuzugia utapigwa pini tu,

yaani kwa sasa wanafatilia mfano biashara za kuuza bidhaa inabidi mzigo ulionunua uwe na risiti yake ya mashine ya tra na pia uwe unauza kwa kutoa risiti kwa mashine, huyu ndugu yangu alipodakwa ni kwamba alikuwa ananunua bidhaa na alikuwa anapewa risiti lakini yeye anatoa tu risiti chache za kuzugia kwa bidhaa alizouza, Tra wakastuka wakaenda dukani kwake kukagua mzigo wakamwambia wameona kwenye system yao anauziwa bidhaa nyingi na watu wanaomuuzia kwa risiti lakini yeye vitu anavyouza kwa risiti ni vichache, mzigo uliobaki uko wapi ? Akaanza kupiga kiswahili pale lakini haikusaidia, TRA wakahitimisha kihalali kwamba anauza bila kutoa risiti a.k.a anasaidia ukwepaji wa kodi.

Wakati anasubiri hatma ya kitachomkuta alitumia connections zake na kwenda kuwabembeleza Tra kwenye ofisi zao lakini wapi... Kwanza hata huko akagundua wapo wengi.

mwezi uliopita kapigwa faini ya takribani milioni 160, hio faini ni mchanganyiko wa VAT walizokadiria kakwepa + interest + efd penalty, n.k.

Cha kushukuru ni kwamba hawakufunga akaunti zake ama kumpeleka mahakamani, hadi hapa alipo imebidi aanze kurejesha mdogo mdogo kwa maumivu makali sana, yaani kwa sasa yupo makini sana kuuza bidhaa kwa kutoa risiti za vat.

Ila nikowa muwazi bila kupepesa macho, kapigwa faini kwa uzembe wake maana haiingii nimeshangaa inakuwaje anunue mzigo wenye kodi ya vat alafu asitoe risiti jli kuikomboa vat, nimeumia sana hapa maana hili lilikuwa linakwepeka.

Kimbembe kipo kwa wanaonunua mizigo isiyo na risiti za tra, hii mara nyingi ni kwa wale wanaouza magendo yaliyoingizwa nchini bila vibali, Yani hapa utayaita maji Mma!!
 
Na nimejirodhisha kwamba kwa sasa TRA kwa sasa wanadili na wakwepa kodi bila kujali connection zako, wakiona unakwepa wanapita na wewe.

Hawa kina diamond na huyo pck wanaolalamika wakae wakijua sio wao tu, hii ni operation kubwa sana iliyonasa wengi.

Binafsi nina ndugu yangu alianza biashara kwenye mwaka 2015 hivi na kiukweli mambo mengi ya kodi yalikuwa yanazungumzika tu, lakini hapo mwezi uliopita kapigwa faini ya takribani milioni 100 kwa kosa la kuuza bidhaa bila kutoa risiti.

Connections anazo si haba maana kama awali nilivyosema hapo nyuma alikuwa na uwezo wa kuyazungumza na kuyamaliza na TRA alkini kwa sasa juhudi zilihonga ukuta, Alihangaika huku na kule lakini maamuzi hayo yalikuwa ni final, na ana bahati hawakufunga akaunti zake ama kumpeleka mahakamani, hadi hapa alipo imebidi aanze kurejesha mdogo mdogo kwa maumivu makali sana, yaani kwa sasa yupo makini sana kuuza bidhaa kwa kutoa risiti za vat.

Kwa ninachokiona hadi sasa TRA wamedhamiria sana kupiga msako a kufa mtu kwa uhalali na kufata sheria kuwataiti wanaokwepa kodi,
ILA WATANZANIA JAMANII KWA NINI TUNA HULKA YA KUKWEPA KODI SANA,!! HATA KAMA CHANZO NI MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI ILA TUMEZIDI BANA.
 
ILA WATANZANIA JAMANII KWA NINI TUNA HULKA YA KUKWEPA KODI SANA,!! HATA KAMA CHANZO NI MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI ILA TUMEZIDI BANA.
Hivi unajisikiaje unajikaba kulipa kodi halafu unakuja kuambiwa serikali imekopa pesa Trillion 4 kwa ajili ya kuboresha uwezo wa kiutendaji wa watumishi wa umma, just imagine, ndio kitua gani hicho? Halfu riba tilllion 2, hivi hata ingekuwa wewe utajisikiaje?
 
Nimejiridhisha kwamba kwa sasa TRA wana jambo lao kwa wakwepa kodi maana si kwa kelele hizi, wakiona unakwepa wanapita na wewe.

Hawa kina diamond na huyo pck wanaolalamika ni kwasababu ni maarufu ndio maana wanasikika lakini wakae wakijua sio wao tu, hii ni operation kubwa sana iliyonasa wengi tena kihalali bila uonevu wala mabavu.

Binafsi nina ndugu yangu alianza biashara kwenye mwaka 2015 hivi, Enzi hizo Magu kaingia na msisitizo watu watoe risiti kwa mashine, hapa waliokuwa hawana mashine ndio walikiona cha mtemakuni, kukwepa huu mhaho wengi ilibidi wanunue hizo mashine ila wakawa wanatoa risiti chache za kuzugia, kwa sasa hali ni tofauti kabisa, hio style ya kutoa risiti za kuzugia utapigwa pini tu, yaani kwa sasa wanafatilia mfano biashara za kuuza bidhaa inabidi mzigo ulionunua uwe na risiti yake ya mashine ya tra na pia uwe unauza kwa kutoa risiti kwa mashine, huyu ndugu yangu alipodakwa ni kwamba alikuwa ananunua bidhaa na alikuwa anapewa risiti lakini yeye anatoa tu risiti chache za kuzugia kwa bidhaa alizouza, Tra wakastuka wakaenda dukani kwake kukagua mzigo wakamwambia wameona kwenye system yao anauziwa bidhaa nyingi na watu wanaomuuzia kwa risiti lakini yeye vitu anavyouza kwa risiti ni vichache, mzigo uliobaki uko wapi ? Akaanza kupiga kiswahili pale lakini haikusaidia, TRA wakahitimisha kihalali kwamba anauza bila kutoa risiti a.k.a anasaidia ukwepaji wa kodi.

Wakati anasubiri hatma ya kitachomkuta alitumia connections zake na kwenda kuwabembeleza Tra kwenye ofisi zao lakini wapi... Kwanza hata huko akagundua wapo wengi.

mwezi uliopita kapigwa faini ya takribani milioni 160 kwa kosa la kuuza bidhaa bila kutoa risiti.

Ana bahati hawakufunga akaunti zake ama kumpeleka mahakamani, hadi hapa alipo imebidi aanze kurejesha mdogo mdogo kwa maumivu makali sana, yaani kwa sasa yupo makini sana kuuza bidhaa kwa kutoa risiti za vat.

Ma huyu kapigwa faini kwa uzembe wake maana haiingii akilini ununue mzigo wenye kodi ya vat alafu wewe uwe mvivu wa kutoa risiti, ni kama vile unajipiga risasi mguuni.

Kimbembe kipo kwa wanaonunua mizigo isiyo na risiti za tra, hii mara nyingi ni kwa wale wanaouza magendo yaliyoingizwa nchini bila vibali, Yani hapa utayaita maji Mma!!

Ni kawaida kwa wasio nacho kukenua wakidai madhila yoyote kwa wanayedhania anacho yakimkuta kuwa ni halali.

Kwamba unaoekana kuwafagilia sana TRA? Ni wazi kuwa wewe ni mwenzao au huna uzoefu nao kabisa.

Anzisha biashara yoyote ndugu kuwafahamu hawa mabwana na hasa kwenye yale mambo yao (au yenu) pendwa - rushwa!
 
ILA WATANZANIA JAMANII KWA NINI TUNA HULKA YA KUKWEPA KODI SANA,!! HATA KAMA CHANZO NI MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI ILA TUMEZIDI BANA.

Hudhani kuwa ni kwa sababu kodi na tozo hizi ni nyingi mno na kwetu tu wakati walamba asali na watoza ushuru wenyewe haziwahusu?

Hudhani sote kabisa tukiwa tunawajibika kulipa kodi kwa usawa kodi zitakuwa fair kwa wote?

Kwanini kodi na tozo ziwe kwetu lakini si kina Mwigulu, Zungu au hawa vibopa wa TRA.
 
Mkuu,
Hiyo risiti yenye VAT unayoiongelea 18% unajua ikipigwa kwa kila bidhaa unafiliska haraka?

Hivi unajua mfuko mmoja wa simenti au nondo kuna faida ya sh. Ngapi?

afu utoe risiti ya efd na serikali ikate kodi Yake pamoja na vat 18%

Hivi haya unayoshabikia unafanya biashara au uliwahi KUFANYA biashara kweli?
 
Niwaambie TU wanajf
Hamna mfanyabiashara anapenda kukwepa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake

Tatizo Ni

1. mfumo wetu wa Kodi umekaa kinyonyaji sana, anaetunga sheria na kanuni za Kodi ni mwanasiasa bill kumhusisha mfanyabiashara na hayajui mazingira halisi ya biashara.

Ukiifuata sheria ya Kodi inavotaka unafilisika mchana kweupe na hakuna anaekuonea huruma, kiukweli Kodi zetu sio rafiki kwa mfanyabiashara yeyote mzalendo.

2. Matumizi ya Kodi,
Inaumiza Sana unalipa Kodi kizalendo afu unaskia Kodi yako uliolipa Kuna wahuni wanafuja fuja TU kwa maslahi Yao binafsi Tena kwa majigambo lukuki wakiitana majina wanayojua wao kana kwamba sisi wengine hatuna akili wametupa limbwata.Inaumiza sana na kuvunja Moyo.
 
Ni kawaida kwa wasio nacho kukenua wakidai madhila yoyote kwa wanayedhania anacho yakimkuta kuwa ni halali.

Kwamba unaoekana kuwafagilia sana TRA? Ni wazi kuwa wewe ni mwenzao au huna uzoefu nao kabisa.

Anzisha biashara yoyote ndugu kuwafahamu hawa mabwana na hasa kwenye yale mambo yao (au yenu) pendwa - rushwa!
Mtoa mada ana roho ya kimaskini kufurahia matatizo ya wenye nacho
 
Mkuu,
Hiyo risiti yenye VAT unayoiongelea 18% unajua ikipigwa kwa kila bidhaa unafiliska haraka?

Hivi unajua mfuko mmoja wa simenti au nondo kuna faida ya sh. Ngapi?

afu utoe risiti ya efd na serikali ikate kodi Yake pamoja na vat 18%

Hivi haya unayoshabikia unafanya biashara au uliwahi KUFANYA biashara kweli?
Umenunua bidhaa ya elf 20,.... Kwenye risiti inaonesha umelipia vat asilimia 18% sawa na 3,050

Unaenda kuiuza kwa shilingi elf 25,000, ukitoa risiti ya tra kwa bei hio ni kwamba chako ni 21,186 na kodi ya vat ambayo kalipia mteja ni shilingi 3,814, kwenye hii kodi aliyolipia mteja utajilipa mwenyewe ile vat ya mwanzo ya 3,050, Tra wanachotaka ni hio vat iliyozidi ambayo haikuhusu 3,814 - 3,050 = 764.

hata auze kwa faida ya jero bado atajilipa vat aliyolipia wakati ananunua mzigo

unakomboa hela ya kununua mzigo + faida + unafidia vat uliyolipa mwanzo ... Tatizo lipo wapi ???
 
Niwaambie TU wanajf
Hamna mfanyabiashara anapenda kukwepa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake

Tatizo Ni

1. mfumo wetu wa Kodi umekaa kinyonyaji sana, anaetunga sheria na kanuni za Kodi ni mwanasiasa bill kumhusisha mfanyabiashara na hayajui mazingira halisi ya biashara.

Ukiifuata sheria ya Kodi inavotaka unafilisika mchana kweupe na hakuna anaekuonea huruma, kiukweli Kodi zetu sio rafiki kwa mfanyabiashara yeyote mzalendo.

2. Matumizi ya Kodi,
Inaumiza Sana unalipa Kodi kizalendo afu unaskia Kodi yako uliolipa Kuna wahuni wanafuja fuja TU kwa maslahi Yao binafsi Tena kwa majigambo lukuki wakiitana majina wanayojua wao kana kwamba sisi wengine hatuna akili wametupa limbwata.Inaumiza sana na kuvunja Moyo.
Mfumo wa Kodi kwetu ni wakuumiza, wameweka hivo maksudi Ili ushindwe wapate rushwa. Amini Amini hizi Sheria na mifumo wanaipenda sana sababu inawapa mianya wao kupokea rushwa sababu wanajua hakuna anayetoboa Kwa mfumo huu kihalali.
 
Tatizo la Tanzania walipa kodi hawafiki 6mil.
Hivyo ni asilimia 10 tu ndo hulipa, tungeongeza wigo wa kodi kelele zisingekuwa nyingi.

Leo mfanyabiashara akisema atoe risiti kamili ataumia yeye maana atakosa wateja kwani itabidi aongeze ile 18%

Viwanda ndo vinafaidi kwenye VAT ila biashara ndogo ndogo ambazo hesabu zake hazijulikani ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom