Ndugu wa wafanyabiashara waliopotea waiangukia Polisi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1706001531070.png

Ndugu wa wafanyabiashara wawili wa mbao waliopotea mwaka jana, wameliangukia Jeshi la Polisi nchini, wakitaka liwasaidie kuwatafuta ndugu zao.

Familia hiyo imesema kuwa imewatafuta ndugu zao hao bila mafanikio, hivyo inaliomba jeshi hilo kuwasaidia kufanya hivyo.

Wafanyabiashara hao wa mbao Juma Iddi (45) na Haruna Iddi (50) walitoweka mnamo Desemba 28, 2023 saa 10 jioni katika maeneo tofauti ya Mwenge na Mghanga, mjini Singida

Akizungumza na Mwananchi Digital, mmoja wa wanafamilia hao, Seif Juma amesema wao kama familia hawana tena cha kufanya zaidi ya kuvisikiliza vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuwatafuta bila mafanikio tangu mwaka jana.

Amesema licha ya kutoa taarifa Polisi hadi sasa hawajapata mrejesho wowote kutoka jeshi hilo juu ya kupotea kwa ndugu zao.

"Hatuna tena cha kufanya tumewaachia Polisi watusaidie kuwatafuta ndugu zetu, mpaka leo hii hawajatupa ushirikiano. Hakuna chochote walichotuambia kuwa kinaendelea kwa hiyo tupo tu na majonzi hatujui walipo," amesema Seif.

Januari 3, 2024, mmoja wa mashuhuda, Hassan Seif alisema akiwa Mwenge mkoani Singida, alishuhudia mmoja wa wafanyabiashara hao akichukuliwa na watu wawili walioshuka kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye rangi nyeupe.

Alidai baada ya kumpakia kwenye gari hilo liliondoka kwa mwendo wa kasi kutoka kwenye eneo hilo.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa alisema wamefanya taratibu zote za kipolisi na kuwasilisha makao makuu.

"Kuhusu hao wafanyabiashara tulishafanya taratibu zote za kipolisi na tumeshawasilisha makao makuu. Kwa hiyo anayetakiwa kutolea maelezo ni Msemaji wa Jeshi la Polisi ngazi ya Taifa Kamanda David Misime na siyo sisi,” alisema.

Hata hivyo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Misime jana hakupatikana kwa siku nzima baada ya simu yake ya mkononi kuita bila majibu.

Juhudi za kumtafuta Misime kulizungumzia suala hilo zinaendelea japo kuanzia saa tatu asubuhi ya leo, simu yake haikuwa ikipatikana.
 
25 January 2024
Singida, Tanzania

Familia yafikisha suala mbele ya Paul Makonda kuhusu kupotea kwa wafanyabiashara, waomba msaada


View: https://m.youtube.com/watch?v=hmHHz99lm0s
Bi. Mwanahamisi Ally mke wa mmoja ya watu waliopotea aelezea ... ilivyo toka mumewe na shemeji yake kupotea, familia imefika hadi ofisi ya RPC Singida na mkuu wa wilaya DC Moses Machali anadai wawili waliopotea waliaga kuwa wanatoka kwenda kazi.... naye mkuu wa mkoa wa Singida RC Peter Serukamba asema .....
 
25 January 2024
Singida, Tanzania

Familia yafikisha suala mbele ya Paul Makonda kuhusu kupotea kwa wafanyabiashara, waomba msaada


View: https://m.youtube.com/watch?v=hmHHz99lm0s
Bi. Mwanahamisi Ally mke wa mmoja ya watu waliopotea aelezea ... ilivyo toka mumewe na shemeji yake kupotea, familia imefika hadi ofisi ya RPC Singida na mkuu wa wilaya DC Moses Machali anadai wawili waliopotea waliaga kuwa wanatoka kwenda kazi.... naye mkuu wa mkoa wa Singida RC Peter Serukamba asema .....

Usipokuwa mwanaccm utakula kwako! Ili ushughulikiwe lazima uwe mwanaccm.
 
Wafanyabiashara wawili wa familia moja, wakazi wa Manispaa ya Singida wametekwa na watu wasiojulikana.

Ni mwezi mzima sasa wakiwa hawajulikani waliko huku hofu ikiendelea kutanda kwa ndugu na jamaa kama wako hai au wameuawa.

Wafanyabiashara hao wanaodaiwa kutekwa katika Manispaa ya Singida Desemba 28, mwaka jana, ni Juma Mwiru ambaye ana ofisi eneo la Mitunduruni na Haruna Mwiru, mmiliki wa kiwanda cha kuchana mbao kilichoko Unyankindi, Manispaa ya Singida.

Source - Nipashe
 
Hiyo habari yao ilishaletwa huku
Vp hawajapatikana tu
Vp na yule aliyetekwa mikocheni kapatikana naye

Ova
 
Haya mambo ya kutekana naona watu wamebobea sasa, serikali ichukue hatua kali mno mno kwa wahusika na iwe wazi na adhabu yake iwe kifo kwa wahusika yaani watekaji..!!

Tabia mbaya sana hii ya kijambazi na ushetani mkubwa sana
 
Poleni mno kwa ndugu na jamaa wa wahanga hao,ILA watanzania wenzangu tuwalazimishe watawala wetu wawajibike kwetu na sio kuangalia ya kwao tu,tatizo hili ni la muda mrefu na watekaji wanajua hawatakuja kukamatwa, tufanye yafuatayo;biashara zote wamiliki walazimishwe kufunga cctv ambazo zitakua linked na police, pia municipalities zote zifunge cctv kwenye maeneo yao ya kiutawala,police wafunge cctv ambazo zitakua na uwezo wa kuyatambua magari yote yanapoingia na kutoka, tusisubiri matapeli kama yule aliyetuambia kuwa atafunga cctv pale kitonga pass, ni lazima tutumie technology na ndio dunia ya sasa, traffic officer's wetu wote wavae body cum wanapokua kazini
 
Back
Top Bottom