Ndoa zina matukio jamani

Ndoa zina matukio jamani

Haswa za kizazi hiki.

Usaliti umekuwa kitu cha kawaida, magomvi kama yote, wengi wanafeki furaha ila ndani kunafurukuta. Matukio ya kutisha, najiuliza walewale waliokuwa wanacheza romantic songs sijui blues kwa hisia na upendo ndo hawahawa leo wanakimbizana na mapanga?

Wamechafukwa hawatamani kuonana tena, ndo hawa kila mmoja kamchoka mwenzake? Wanapigana wengine wanauana.

Ndoa imekuwa kifungo cha maumivu, nimeshuhudia wengi wakiteseka kihisia, kimwili, kiroho nk

Ndoa sio salama tena imekuwa njia ya kujipatia magonjwa ya kila aina, ukitaka magonjwa yote ingia kwenye ndoa na malaya asiejua kuridhika wala kutulia. Ndoa zimegeuka tanzi na mtego.

Hata ukiweka vigezo 100 lakini ukweli watu hubadilika kutokana ma situations zinazotokea maishani. Mpaka baba mchungaji anachepuka. Ukiyumba kiuchumi kidogo tu mwenzio kakukimbia. Ukipata hata ajali ukilala tu kitandani mwenzio anaomba talaka ama anahamia kwa mwingine.

UKITAKA KUINGIA KWENYE NDOA JIPANGE NA UWE NA ROHO NGUMU!
Mazoea yana tabu sana,
Fanyeni usafi kama kabla ya ndoa Mbona mlikua Smart sana no smell sasa ivi ni nini imetokea?
 
Ndoa ni tamu sana, acha kupotosha vijana wadogo waziogope.
Sijawapotosha mkuu..ila naongelea matukio yake nnayoshuhudia
Hata hii inaweza pelekea kupata idea how to make it last and sweet
Kila kitu kina pande mbili nzuri na mbaya..
 
Utafiti wangu umegundua wanawake wengi ambao hamjaolewa mna mtazamo hasi kuhusu ndoa.
Kwakweli !
Though mi Nina mtizamo chanyq.
Nimegundua wengi waliokosea kwenye hili eneo wanataka kuaminisha watu kuwa ndoa ni mbaya,kitu ambacho sio sawa
Kuna watu hawajui shida kwenye ndoa zao!
Lkn pia changamoto kawaida watu mmelelewa ,mmezaliwa tofauti unategemea nn?
Mungu kwanza,upendo, uvumilivu...basi
 
Ndoa ni kama kifo na kuishi
Huwezi kuogopa kifo kama unaishi
na kinyume chake ni sahihi.

Tutaendelea kuishi humohumo mwisho tutafika. Kiufupi maisha sahivi yanachangamoto sana.
Uaminifu katika mambo mengi iwe ni kwenye pesa ni changamoto pia.

Wavumilivu watakula mema ya Nchi
You said well bro. Humo humo tunaishi na tutafika,No way
 
Mwambie inawezekana anaumwa. Kushindwa kumwambia ni udhaifu na humtendei haki.
ukiiangalia tu, unaona kabisa ukiigusa tu lazma utibue hali ya hewa na kua nzito mithili ya dalili ya korona,

acheni hizo bana,
Lips zimeshine ile mbaya, zinang'aa kama malaika,
akuhemee sasa akiwa karibu yako heeeheeeee......
naona aibu kusema.....

sitaki kusema kuzidi ya hapo, haya ni baadhi ya matukio muhimu yanayopatikana kwenye manyumba mengi ya watu na wanateseka nayo taratibu....


Mbayaaeee.......
 
ukiiangalia tu, unaona kabisa ukiigusa tu lazma utibue hali ya hewa na kua nzito mithili ya dalili ya korona,

acheni hizo bana,
Lips zimeshine ile mbaya, zinang'aa kama malaika,
akuhemee sasa akiwa karibu yako heeeheeeee......
naona aibu kusema.....

sitaki kusema kuzidi ya hapo, haya ni baadhi ya matukio muhimu yanayopatikana kwenye manyumba mengi ya watu na wanateseka nayo taratibu....


Mbayaaeee.......
Achane hizo kwani una wake wangapi wewe? Anayenuka ni huyo wa kwako...
 
Mkeo kabaki mpweke now 😂😂
sasa si mngetoka wote? Nyie si mwili mmoja?
Sasa natokaje na wife kwa maswala ya kazi mkuu, yeye yupo home nikienda nakuta chakula safi kaniandalia, naamua nianzie wapi na weekend hii🤣🤣. Haya single na upweke wake anaona bora ale chips na pepsi yake siku iende, single anaona bora aende beach akakae peke yake huko kupunguza stress, guys ndoa pamoja na mapungufu yake yote ni tam, tena tamuuu
 
Back
Top Bottom