Ndoa zina matukio jamani

Miss Champagne

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
2,157
6,309
Haswa za kizazi hiki.

Usaliti umekuwa kitu cha kawaida, magomvi kama yote, wengi wanafeki furaha ila ndani kunafurukuta. Matukio ya kutisha, najiuliza walewale waliokuwa wanacheza romantic songs sijui blues kwa hisia na upendo ndo hawahawa leo wanakimbizana na mapanga?

Wamechafukwa hawatamani kuonana tena, ndo hawa kila mmoja kamchoka mwenzake? Wanapigana wengine wanauana.

Ndoa imekuwa kifungo cha maumivu, nimeshuhudia wengi wakiteseka kihisia, kimwili, kiroho nk

Ndoa sio salama tena imekuwa njia ya kujipatia magonjwa ya kila aina, ukitaka magonjwa yote ingia kwenye ndoa na malaya asiejua kuridhika wala kutulia. Ndoa zimegeuka tanzi na mtego.

Hata ukiweka vigezo 100 lakini ukweli watu hubadilika kutokana ma situations zinazotokea maishani. Mpaka baba mchungaji anachepuka. Ukiyumba kiuchumi kidogo tu mwenzio kakukimbia. Ukipata hata ajali ukilala tu kitandani mwenzio anaomba talaka ama anahamia kwa mwingine.

UKITAKA KUINGIA KWENYE NDOA JIPANGE NA UWE NA ROHO NGUMU!
 
_20231014_085631.JPG
 
Ndoa ni kama kifo na kuishi
Huwezi kuogopa kifo kama unaishi
na kinyume chake ni sahihi.

Tutaendelea kuishi humohumo mwisho tutafika. Kiufupi maisha sahivi yanachangamoto sana.
Uaminifu katika mambo mengi iwe ni kwenye pesa ni changamoto pia.

Wavumilivu watakula mema ya Nchi
 
KIPANDE CHAKO.

Bwana Ralph Hart anasimulia: Hapo kale ilivyokuwa katika uumbwaji, wanawake na wanaume hawakuwa wametengana kama walivyo hii leo. Kiumbe alikuwa mmoja, mwenye mwili na shingo, lakini kichwani alikuwa na nyuso (sura) mbili, zenye uelekeo tofauti. Ilikuwa kana kwamba ni viumbe wawili waliogundishwa pamoja, wakiwa na jinsi (sex) mbili tofauti, pamoja na mikono minne na miguu minne.

Kwa fikra zao, miungu wa Kigiriki wakajawa wivu, kwamba kiumbe huyu mwenye sura mbili (anayeweza kuangalia mbele na nyuma), alikuwa na umakini mkubwa usiokumbwa na mshitukizo wa kitu; pia miguu na mikono minne vilimfanya aweze kusimama muda mrefu na kufanya kazi bila kuchoka. Mbaya zaidi, kwakuwa kiumbe huyu alikuwa na jinsi mbili, hivyo hakuhitaji kutafuta mtu mwingine wa kushiriki naye 'tendo' kwa ajili ya kuendelea kuzaana.

Siku moja kiongozi wa miungu hao alisema: "Nina mpango wa kukipunguzia nguvu kiumbe hiki."

Ndipo akakitenganisha kiumbe hicho, na kupatikana viumbe wawili; mwanaume na mwanamke. Pamoja na hatua hiyo kupelekea ongezeko kubwa la watu duniani, lakini pia ilimfanya mwanaadamu kwa kupungukiwa kipande muhimu cha sehemu ya mwili wake, kiasi cha kumfanya awe dhaifu na mwenye kuhangaika kila uchao kukitafuta kipande chake ili kukisogeza na kukifumbata (walau) karibu, ili kujirejeshea ile nguvu yake ya asili, kurudisha utulivu na kuondoa uwezekano wa usaliti, pamoja na kuitwaa tena ile nguvu ya kusimama muda mrefu, kuwa na umakini, na kufanya kazi bila kuchoka.

Hali hiyo ya kutafuta kipande muhimu kilichoondoshwa, na kujaribu tena kujikumbata pamoja, kitu ambacho tunaona miili ya wanaadamu (mke na mume) kama vile inashindwa tena kuendana, ndio leo tunaita 'tendo la mapenzi'.

Kwa mtazamo wangu: ukiona kila unavyojaribu kumshika na kumfumbata karibu mwenzi wako, ili kumrejesha karibu yako kama sehemu ya kipande ulichotenganishwa nacho, lakini mwenziyo haelekei wala hashikamani - achana naye - hicho kipande pengine hakikutoka kwako. Ni kama vile, umeokota betri ya simu ya Nokia kisha ukataka kuiweka kwenye simu ya Sumsung, simu haitowaka kwa sababu umeiwekea kitu (betri) kisicho chake. Mtu wa maendeleo, akikipata kipande chake—basi kwa shida na raha watafikia malengo. Na mtu wa anasa naye—kipande chake kuna sehemu kinamsubiri ili wakishaungana wanyooshane. Using'ang'anie kipande kisicho chako. Kitupe haraka.
 
Kuishi tu alone kuna changamoto nyingi, yaani alone pale ghetto kwako kuna changamoto kibao, kuna wakati hata hutamani kurudi ghetto, japo upo mwenyewe...
...iwe ndoa au single, bado maisha yana changamoto nyingi sana.
 
Back
Top Bottom