Ndoa za wasomi

Ndoa za wasomi

kabisa, na mimi pia napenda mwanaume aliyesoma, mwanaume/mwanamke asiye na shule hata siri hana yaani akidet na mtu lazima marafiki zake wote wajue.

mimi sipendi kabisa mwansume asiye na shule, huwezi hata kuchat naye, kiingereza kidogo tu anashindwa kuelewa, hata mambo ya duniani anakuwa hajui zaidi ya ushilawadu.


Haha Ushilawadu...lol
Ni kweli Serikali3, inapokuja swala la kupishana kielimu Inahitaji maamuzi ya kweli, kama umeamua kumpenda mtu kwa alicho nacho na alivyo pasipo kuangalia hayo mengine.
Ukisema upende nusu usiangalie mapungufu, kuna siku yatakushinda.
 
Japo mimi ni msomi ila huwa siwazi kuoa msomi, inaweza kutokea lakini sio jambo ninalolipanga.
Ukitaka kuwajua hawa wanawake wasomi jaribu kuongea nao ukiwa huna nia ya kuwa nao, utastaajabu mengi.
Sikatishi tamaa wanaowapenda ila wawe makini maana wengi ni pasua kichwa.
 
Siikani post yangu... Naelewa nilichokiandika ndo maana nikakataa unachosema!!! Nafahamu kua mwanamke na mwanaume hawawezi kua na usawa wanaosema watu. Sema wanaume wanaogopa wadada wasomi sababu ni ngumu kuwapelekesha na kuwaonea
kupelekeshwa kivipi yaan
tolea mfano
yaani bado uko kwenye mainstream ile ile ambayo nasema upo
 
Na kama huyo mama wa Pepsi, naelewa kuna wanawake wa hivyo na ambao waliona hawawezi kufanya yote na kuacha moja.
(for the case I know) Malkia wa nguvu kama mke wa kampelewele but with the MBA, alidrop kazi yake nzuri kwa muda kwa ajili ya kumaliza kuzaa na kulea watoto wake wadogo, then she went back to the workforce. So ni kweli challenges zipo but, someone need to find a way around it and then.. she can have it all.

while nakubaliana na wewe kuwa positive na kudhania kwamba utaweza kubalance mambo (though really hutaweza) umeongea kitu kizuri. lakink mwanamke siku zote akiwa na mimba ni haki yake kuruhusiwa kupata martenity leave nk, mfano umesema ali drop kwenye work force akalea then aka rudi, kwani kulea mtoto kunaisha lini!? na asinge lea nan angelea!? utagundua bado hatuna la kumsifia hapo, ishu yangu ni kuwa idealy uko sawa ila practicaly wanao weza kufanya hivo ni wachache mnooo na si kazi rahisi hata kidogo na wengi ni wale wenye kada flan flan kama walim na manesi kwa mbaaaliii. hata huyo unaye msifia umemfanyankama alilea mtoto halafu aka graduate kulea akaenda kwenye shughuli zake tena , ndio shda hiyo tunayo sema sasa.

all in all mme wako ndio anatakiwa akubaliane na hali yako, hapo mta ish tuu na things will workout, nilimskiliza yule faraja nyalandu naye alisema kabsa kuna zile kazi natural za mama hawezi kuzifanya na alisema ndio kusoma huko kinakuja with a price. na Nyalandu is happy with her so wanaishi, lakin si wanaume woote wako kama Nyalandu ndio tatzo.
 
Hakuna mwanaume anaemuonea mwanamke mtii,mpole na mnyenyekevu kwake.
na wanawake wenye attitude za usawa wa kijinsia kama ndugu yetu hapo hawawez kuwa watiifu na wanyenyekevu, therefore huhisi kila jambo wana onewa na hujikuta sasa wanaingiza harakati kwenye ndoa, ndoa zenye za kibongo et
mweer!!
 
Kuoa mwanamke msomi ni bora hasa kwa kupata malezi bora kwa watoto ,kuwa na muono wa mbali.
Hata maamuzi ya familia yanakuwa positive mkisikilizana.
Na hapa ili heshima iwepo inabidi mume awe na elimu zaidi au kipato zaidi,hapo mambo yanakuwa sawia. Pili mke awe mcha Mungu hapo mambo yanakuwa sawia maana mke mcha Mungu anaamini mume ni kichwa cha nyumba.
Na kuna tabia za makabila na malezi aliyopata mke vinachangia ndoa.
Changamoto za wanawake wasomi ni
1.huwa wanakazi hivyo inamfanya kuchoka na hivyo swala la mapenzi ktk ndoa kulipuuzia hivyo waume kukereka na kuchepuka na mwisho wake mgogoro.
2.Wanawake wasomi rahisi kuchepuka. Mbinu nyingi,maklasmate,wamepita kwingi.
3. Kuna aina za kazi kama uaskari,unesi, wachomomokaji sana. Maana msomi rahisi kupata Kazi
4. Kipato na uhakika wa maisha kusonga bila mume nako ni shida kwa hawa wasomi.
5. Heshima ndani ya nyumba ni ndogo kwa mume,wanaweza vumilia waume wa kizungu kuishi kwa usawa ila kwa tamaduni za kiafrika ni mgogoro

Kwa ujumla kuwa na mwanamke msomi inabidi ujipange au uwe zezeta lasivyo utaishia kuwa mlevi au chizi.
Na ndoa nyingi huwa hazidumu.

Changamoto nyingine msomi ukioa mwanamke ambaye hajasoma nako ni lugha gongana,interest hazita endana.

KWA UJUMLA MKE NI TABIA SIO ELIMU AU SURA.
 
ndio maana jamaa hataki nyie mlo soma
si umeona kasema hapo yeye la saba!!
Kama jamaa la saba wala simshauri aoe msomi sana... Angalau alieishia form 4...
Gepu la elimu nalo likiwa kubwa ni majanga kwa kweli...
Ex wangu aliishia la saba, yaani tukajikuta tunapishana kwenye mengi sana... Nna mpango wa kuchukua PhD ila mwenzangu akanikataza... Alijifeel kua threatened kama mwanaume.
 
Wanaume mmeshaagizwa kuishi na wake zenu kwa akili,haihalishi ni msomi au sio msomi. Usipotumia akili huwezi ishi na mke!
 
Challenges zipo mr Iceman, nakubali. Nakupata pia unavyosema upande wako uvumilivu hakuna, I can only imagine mwanaume anayepitia hali kama hiyo. Kwa kweli inahitaji uvumilivu.

Na kama huyo mama wa Pepsi, naelewa kuna wanawake wa hivyo na ambao waliona hawawezi kufanya yote na kuacha moja.
(for the case I know) Malkia wa nguvu kama mke wa kampelewele but with the MBA, alidrop kazi yake nzuri kwa muda kwa ajili ya kumaliza kuzaa na kulea watoto wake wadogo, then she went back to the workforce. So ni kweli challenges zipo but, someone need to find a way around it and then.. she can have it all.
Ila watch out hata siku moja mwanamke asizidi kiwango cha elimu, umri au hata kipato! Challenges zipo ila kama mwanaume umesoma hakikisha mkeo hampishani sani ili kuondoa inferiority complexity ambayo inaweza kuleta shubiri katika ndoa. Nikupe mfano mdogo katika Barabara zetu akinamama vijana wenye magari ni wakorofi sana hawatoi nafasi kwa wenzao hasa wakiwa wanaume ati atanidharau, ananizidi nini etc. hata ajali nyingi ni wao na ubishi hiyo yote ni inferiority tu. Ikiingia katika ndoa ni hatareee. Naturahi Paprika amethibitisha
 
Inategemea na historia iliomkuza huyo mwanamke, kama ametoka katika umasikini sana na elimu pamoja na kazi mzuri ndio vimemuweka juu.. Basi mashauzi atakua nayo..
Mke wangu ni msomi, ana shahada mbili.. Na ni mtumishi wa Umma.. Ila Hana mashauzi.. Ana heshima sana.. Anafanya kila Kitu kinachotakiwa afanye Mke.. Kingine sababu na mimi mwenyewe Mbabe Mbabe kidogo.. Ila familia ipo Good..

Nb. Ila sijawai kuogopa wanawake wasomi wala walio nizidi kiuchumi..
 
Wengi wao wanaleta uanaharakati katika ndoa. Badala ya ndoa kuwa faraja inageuka kuwa uwanja wa kutunishiana misuli.
 
Wakati mwingine mazingira ya namna mlivyokutana hadi kuanzisha mahusiano mpaka Ndoa huchangia, mathalani umeajiriwa ktk ofisi fulani haujakaa hata mwaka wenzako wanaanza kukupigia chapuo et fulani mnaendana kwann msioane tu, kinachotokea pale ni mtu kuoa pasipo kutumia logical thinking but ametumia advices from other stuff members, na unakuta na binti nae deadline yake iko kweny msitari mwekundu inabidi pia a kubali coz she regards that as a fortune to her kupata mume in simple way like that, sasa majuto huja baada ya kuwa amepata mtoto, /watoto hapo ule utulivu wake alokuwa nao unaisha na ndipo matatizo ktk familia huanzia pale.... But this base only to some ladies not all of them who reached University level.
 
Mimi nina diploma ya clinical medicine mchumba wangu ana degree ya public relation nkimuoa still ataniletea madharau??
 
Marehemu mama yangu alikuwa ameishia darasa la saba, baba ana degree moja lakini sikuona tatizo lolote kati yao walitulea kwa upendo, sikuona mama akiyumba au baba akimdharau kwa kuwa hajasoma, Tumekulia kwenye familia ya raha hadi mama yangu Mungu alipomuita miaka ya hivi karibuni.
Ndoa ni maelewano tu!!
 
Back
Top Bottom