Mie nadhan heshima ktk ndoa inategemea malezi na makuzi, habari ya shule kumbuka nalo ni jambo jingine. Kwa imani yangu mie, mume ni kichwa lakn iwapo mke ameenda shule LIMBUKENI ni kweli heshima hupungua hususani baada ya kuwa na wigo mpana wa watu anaokutana nao ktk majukumu ya kila siku. Hivyo, shule yao au pesa yake humpa jeuri na kuona mume wa kazi gani? Hili halina ubishi kwa asiye na malezi au maadili mema ya kidini. Ndiyo maana wengi wao huishi peke yao au kuishia kuishi na waume wasio na shule kama yao, na hapo ndio vijana wanaopenda pesa au kuendesha magari burebure hupatia michongo.