Ndoa yangu ipo ICU !dah

Ndoa yangu ipo ICU !dah

chukua maamuzi kama mwanaume cha muhimu hakikisha watoto wako wasiingie katika tofauti zenu, umejitahidi sana kuokoa ndoa yako mpaka umemfata morogoro lakini bado anadai talaka na kuendelea kukucheat wako wanaokusubiri lakini huwaoni sababu ya mkeo mpe nafasi uendelee na maisha yako
 
Mda utaongea,naomba wanaume wenzangu tusiwe wavivu wa kufanya maamuzi magumu,uvumilivu wa mwanaume ndio humpa kiburi mwanamke, hawa viumbe ukiona umeanza kuwapenda sana kuhisi huwezi kuishi bila wao bac ujue wameshaanza kuchepuka, kwa sababu umeturuhusu tutoe ushauri Mimi naomba ufanye maamuzi ambayo moyo utaumia kwa mda mfupi ila baadae furaha yako itarudi na hayo yote yatabaki historia tu! Mkuuu!
 
Kaka naomba namba yake nimtumie link ya hii thread pengine roho inaweza kumuuma kidogo akajirudi.
 
Mateso unayopitia ni makubwa kwa kweli Kuna ndoa naifahamu walikua hawaelewani Kama hivi ila baadae mambo yaka change siku hizi wanapendana balaa.naomba nitumie namba yake ya WhatsApp namtumia hii link akisoma nadhani atajiongeza anaweza kubadilika huwez jua
 
Mtoa mada pole sana, ila kabla sijakushauri naomba nkuulize..kumbuka kipindi kile ndo unamtongoza mkeo kwa mara ya kwanza, alikusumbua sana kwa mda mrefu ndo ukampata? Kama alikusumbua kwa mda mrefu alikusumbua kwa mda mrefu kiasi gani? Au ulimpata kirahisi.

Kwenye mwanzo mahusiano yenu kabla hamjaoana, huyo mkeo alikuwa na tabia ya kukuomba pesa hovyo bila mpangilio? Hata kama mizinga yake ilikuwa haikukeri, au Midogo, specify kiasi cha pesa alchokuwa anakuomba. simon baker
 
Mateso unayopitia ni makubwa kwa kweli Kuna ndoa naifahamu walikua hawaelewani Kama hivi ila baadae mambo yaka change siku hizi wanapendana balaa.naomba nitumie namba yake ya WhatsApp namtumia hii link akisoma nadhani atajiongeza anaweza kubadilika huwez jua
we kunguru John, unadhani yeye hawezi kumtumia link au ndo kucheza na nafasi?
 
Pole brother ,Mungu akiwa upande wetu ni Nani aliye juu yetu,Bibilia inasema Hakuna.
Brother,endelea kuwa mpole na kuendelea kufanya majukumu Kama baba wa Familia.
Note.Endelea kumpenda mke wako vizuri kabisa mwisho wa siku,Mungu atamrejesha na huo uovu wake.
Kitu ambacho unateseka nacho ktk kipindi hichi unapoona mwanamke Hana utii Maana wanaume wengi wanapenda utii kutoka kwa wake zake.

Turudi kwenye maandiko ya Neno la Mungu kidogo.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Efeso5:------
 
Hv wanaume wa hv bado wapo? Pole sana usilazimishe kupendwa utaja jutia siku moja au unaweza fanyiwa vitu vya ajabu.
Itisha kikao cha wazazi pande zote mbili waambie nia yako na baada ya hapo muache aendelee na maisha yake. Huyo Tamaa imeshamuingia na ukiendelea kusubr utaletewa Magonjwa na watoto bado wadogo.
 
Ukishagombana na mkeo akakwambia nataka talaka,na kesho akakwambia nataka talaka jiandae kisaikolojia mapema huyo ndoa ishamshinda,piga chini beba kalee wanao maisha mbele.
 
Mkuu pole sana, wewe ni jasiri sana. Ushauri ni kwamba Fanya kile ambacho moyo wako unahitaji, ilimradi kisiwe na madhara kwako wala kwa watoto.
Ila kwa upande wangu, Mwanamke akisha nitamkia, TUACHANE/NIACHE zaidi ya Mara tatu hatakama ni ndani ya siku moja, Hana round Atasepa tu. Sabab moyo wake najua ukishageuka kurud nyuma ni baadae sana.
 
Back
Top Bottom