Ndoa yangu iko njia panda, nifanyeje?

Ndoa yangu iko njia panda, nifanyeje?

Ogopa sana Binadamu, mtu anaweza kukuflame na ukaonekana wewe ni mbaya kumbe ukweli ni tofauti sana, unaweza kukuta huyo Mwanamke she is too nice kwa ndugu wa Mumewe kwa madhumuni maalum, mimi nimeshashuhudia Dada wa Mume akimsindikiza wifi yake kwa Mabuzi na wanatunziana siri.

Tunakoelekea ndoa wala siyo issue tena itakuwa kama ni Life style tu, na nasikia siku hizi kina Mama kile kiapo cha tuataishi milele ila kifo tu ndio kitutenganishe hawakitaki tena, wanataka kifanyiwe editing kidogo ili wawe huru.

Matola
ukistaajabu ya Musa.....its true kwamba muwamba ngoma ngozi huvutia kwake, nimejaribu kulielezea tatizo lilivyo ili nipate ushauri na maoni ya wanJF, Matola wewe ni member wa siku nyingi hoja zako zina mashiko, sasa liamini hili kuwa ni la ukweli. Kuna mwanJF ame-critise nimemuomba kama ataweza nimwambie tukutane naye sisi tukiwa wote 2 then atusikie. Wewe matola kama ni mwanaume je, huwa unampa mshahara mkeo?kama ni mwanamama mumeo anakupa mshahara wake? definitely ni very rare kuona jambo hilo, labda mapenzi yangu kwake ndiyo yamenifikisha ktk hali hii. Am burning up, acheni kejeli
 
Mkuu wewe ndio unaharibu hiyo ndoa yako, tatizo ni wewe huthamini mchango wa mkeo..

1. Ina maana katika hiyo miaka 21 ya ndoa mkeo hana mchango wa familia au wewe unaona mchango ni kuchangia pesa tu? je hu-do nae? je anakuadai pesa ukim-do?

2. Unamuona yeye kama mpira tu au bakuli la kutumia tu si ndio? kwanini hukulalamika hiyo miaka 15 ya ndoa yenu....endapo kama kweli tatizo toka lianze ni five years ago now?

NB: wewe umekuja hapa kulalamika ili upate justification ya kuwa na nyumba ndogo.....USHINDWE NA ULEGEEE KABISA....!

.....Unavyolalamika hasimamii miradi na mafundi hadi wanachakachua...ana-angalia tu...je huoni kama huo nao ni mchango wake au? Acha kuwa self-fish wewe kijana....TAMAA MBAYAAA by 20%.

Lumechaorijino,
Asante kwa mchango wako, ashindwe na alegee shetani anayemgiribu my wife, naamini kwa michango ya wanajamvi atalegea
 
kweli una moyo...mimi hata kwa kurogwa sifanyi huu upuuzi

Kifulambute
Labda ndio kosa langu, lakini mbona ni jambo la kawaida tu jamani hakuna haja ya kumficha mwenzako kipato.
Asante kwa mchango wako
 
Hebu funguka ........... LAZIMA kuna jambo BAYA sana ulimfanyia mkeo ........... Kama ulivyosema "sahani zinagongana" hiyo ni excuse na kujisafisha .......... kuwa MKWELI .... ulimfanyia nini "my wife wako"????? UMEMUUMIZA MOYO WAKE NDIO MAANA AMEAMUA KULIPIZA KISASI

CHEZEA MWANAMKE WEYE??? Labda alikunyamazia kipindi hicho .....sasa amekuweka kwenye kona.
USHAURI WANGU: Tengeneza na Mke wako - jishushe umwombe MSAMAHA ULICHOMFANYIA ..... inaonekana ulimkabidhi miradi yote ukidhani ndio kuomba msamaha ......... MWOMBE PERSONALLY KWA MANENO KWANI SI MPENZI WAKO? MBONA UNAONEKANA UNAMWOGOPA??? JIKAZE KIUME - HAYO NDIO MAISHA - OTHERWISE NAKUTAKIA KILA LA KHERI.:frown:

Yatima,
Sijamkosea kihivyo, kusema kukaa pamoja uwezekano wa kutofautiana upo ni kweli can you imagine 21 yrs ya ndoa lazima mtofautiane nyakati fulani ila inategemeana mnatofautiana kwa jambo linye ukubwa gani.

Omba yasikufike, utalilia siku iendelee bila giza kuingia ili ukae nje ya nyumba bila kurudi home
 
Kifulambute
Labda ndio kosa langu, lakini mbona ni jambo la kawaida tu jamani hakuna haja ya kumficha mwenzako kipato.
Asante kwa mchango wako

Fungwe kwa wanawake wa karne hiii hawatakiwi kabisa kupewa vitu kama hivyo utaishia kunawa
 
kaka inaonekana una kiburi ktk ndoa yako na unamwona mke wako kama hana lolote katika utafutaji wako, na ndiyo hicho kinachokufanya usielewane naye mama yoyo. kama una gari au mali yeyote ifanye iwe yenu wote na awe huru hadi ajisikie kuwa na yeye anamilki hizo mali, sijui nieleze vipi...Let her own you with your assets. then you can find happiness otherwise the way you have wrote it seems you are so arrogant before her and thus why she act like that because the assets yo posses doesnt belong to her according to your statements above.

Before the Law:
50% of your wealth belong to your wife and no question on that,
i do hope yo gat,
i will b RT Back ngoja tufanye kazi kwanza.

Von Mo,
Ni kweli yawezekana kuna tatizo kwa upande wangu, nimeleta suala hili kupata ushauri na nini nifanye, acha nirudie tena kujirekebisha ingawa hayo uliyosema, yeye amekabidhiwa gari na miradi yake. Nitaendelea labda kuchunga kauri yangu miaka hiii niliyonayo nitakuwa mgeni wa nani? Asante kaka
 
Kama kweli unataka msaada Hebu eleza na mapungufu yako bana, usieleze ya mkeo tu,

Angel Msoffe,
Mapungufu yangu, nina hasira lakini si mgomvi, kiburi kipo ni huruka yangu, natumia maneno makali ninapokasirishwa bila kupiga ngumi. Mimi labda naona ni hayo. Mama yoyo nitamshawishi aje aelezee matatizo yangu mpate pa kuanzia.

Kaka asante kwa ushauri wako
 
Hanikabidhi, tunakabidhiana through joint account.

Familia hazina formular Smile...chanzo cha ugomvi wao sidhani kama ni kukabidhi mshahara; kuna kitu anachojua mwenyewe kilichowagombanisha au kilichomfanya awe anatoa mshahara wote kwa wife...maana naona kama hiyo ya kukabidhi mshahara imeanza ghafla siyo from day one ya ndoa yao...isije ikawa ni katika hasira na kususa ndio kaamua kumbwagia wife wake mshahara.

Nyumba kubwa,
hapana nilianza kumkabidhi mshahara mwanzoni kabisa kwani ndivyo tunashauriwa mwenzako usimfiche kipato chako. Sasa nimekuja kumnyima hiyo fursa baada ya kuona fedha hazionekani

Otherwise I value your advice
 
Von Mo,
Ni kweli yawezekana kuna tatizo kwa upande wangu, nimeleta suala hili kupata ushauri na nini nifanye, acha nirudie tena kujirekebisha ingawa hayo uliyosema, yeye amekabidhiwa gari na miradi yake. Nitaendelea labda kuchunga kauri yangu miaka hiii niliyonayo nitakuwa mgeni wa nani? Asante kaka

ok, nothing u can do to heal yo marriage! only Love can heal your marriage!
nakupemu ufanye nini.
 
Angel Msoffe, Mapungufu yangu, nina hasira lakini si mgomvi, kiburi kipo ni huruka yangu,
ukikasirika unaweka kiburi kula chakula cha kujenga mwili na kile kingine cha ndoa?
natumia maneno makali ninapokasirishwa
kama haya,Mwanamke gani wewe kwanza umezeeka,Takataka mkubwa wewe,hukufunzwa adabu huko kwenu nk?
Mama yoyo nitamshawishi aje aelezee matatizo yangu mpate pa kuanzia.
wazo zuri sana lakini hakikisha ni yeye kweli,usije ukaja ww mwenyewe na id nyingine
Kaka asante kwa ushauri wako
mimi ni dada,....Thanks anyway
 
Nimesoma jumbe na michango mingi ya wanabodi na kiukweli nakubaliana na baadhi...kikubwa usisahau kuchanganya na za kwako....ILA tatizo ninaloliona hapa ni kwamba KESI imekuwa ya upande mmoja na kwa vyovyote ushauri mwingi unakuwa wa kukupasa!!!..

Jiulize tu kuwa pale mliposhauriwa ilhali wote wawili mkiwa mmejieleza IMESHINDIKANA kuwork out..leo itakuwaje hapa ambapo unajieleza wewe peke yako??....My Take: Kuanza moja sio Ujinga..Jipeni nafasi ya kuwa mbali ikibidi 'temporal separation' manake sioni unacholoose ikiwa una 2 years tayari no unyumba...Yasipojiset basi haikuwa riziki..let the unsolved problems do u part!!
 
Mi ndo nafunga ndoa j,pili, dah umeanza kunitisha, ila japo ndo naanza ningekwambia umchunguze labda watu wanamega kisela ndo maana anakiburi, chunguza, pia fanya maombi kwa MUNGU yote yanawezekana
 
"wanawake huwa hawataki wanaume wapole,kuwa mkorofi utaona"
 
Kumbe mshahara ulikuwa unampa zamani; sasa hivi umeacha...inawezekana hilo likawa moja ya sababu...kama toka umemuoa ulikuwa unakabidhi mshahara alafu ukaja kusema from today sikupi mshahara tena; lazima akununie.

Kwa nini msipange matumizi pamoja?

Well kama ulivyosema mwambie nae aje afunguke...maana haya mambo ya ndoa unaweza shangaa akija humu akaanza kuandika mambo ambayo hata wewe hukufikiria kuwa ndio source ya conflicts zenu.

Communication ni ngumu sana kwenye ndoa nyingi; ndio maana ni muhimu sana kuhusisha thrid party mambo yakiwa ndivyo sivyo.

Afu nikwambie kitu; kwa wanawake wengi (kutokana na life experience yangu na kuongea na wamama aged) wanasema ni bora kuwa na mume anayepiga kuliko mwenye mdomo. Kwa hiyo usi underestimate maneno unayotoa ukiwa na hasira...maneno ni sumu kuliko kipigo.

Nyumba kubwa,
hapana nilianza kumkabidhi mshahara mwanzoni kabisa kwani ndivyo tunashauriwa mwenzako usimfiche kipato chako. Sasa nimekuja kumnyima hiyo fursa baada ya kuona fedha hazionekani

Otherwise I value your advice
 
Mfano umwambie wife mwanamke mwenyewe performance zero...akyanani hata mimi ntakupa likizo ya miaka 3 si 2; ili ulijue jiji (natania. Lol)

ukikasirika unaweka kiburi kula chakula cha kujenga mwili na kile kingine cha ndoa?kama haya,Mwanamke gani wewe kwanza umezeeka,Takataka mkubwa wewe,hukufunzwa adabu huko kwenu nk? wazo zuri sana lakini hakikisha ni yeye kweli,usije ukaja ww mwenyewe na id nyingine mimi ni dada,....Thanks anyway
 
Fugwe si mpole kama ulivyo perceive...mbona mwenyewe keshasema hapa kuwa alishaacha kumpa mshahara wife long time. Lol. Angekuwa mpole hiyo jeuri ya kukatiza kitu alichomzowesha mkewe ameitoa wapi?

Kurudi kwenye mada ya kuwa kimada muadilifu..bado napinga...mimi niwajuao waadilifu na walokosa waume bado wanasita kutembea na waume za watu...maana the moment watakubali kuwa kimada...neno heshima linapotea hapo hapo.

Huwezi kuwa kimada ukatulia kwa sababu uhusiano wako unategemea na maugomvi ya familia uliyoiingilia...once waki seto tofauti zao unabaki una hang; unatafuta familia nyingine yenye ugomvi...kuja zeeka umeshakuwa kimada wa familia kadhaa. Hapo bado kuna kuzungumiza heshima?... au kutumiwa na shetani kufanya matatizo ya familia za watu yaendelee kuwa sugu; hata sala zao zitakuwa watu waendelee kugombana ili aendelee kuwa kimada...si mtumwa wa shetani ni nini?. unless umwambie aoe mke wa pili.

mbona wako wengi tu dadangu, kuna wanawake wengi wametulia tuli lakini kwa bahati mbaya hawajapata waume wa kuwaweka ndani..hao waliopata waume wanawachezea, wenzio wanawatafuta..

kwa nini afe na mastress wakati wako watu wa kumliwaza?

huyo mwanamke hatajua thamani ya mume wake mpaka atakapomkosa.
yani mume anakukabidhi mshahara wote, halafu anakuomba wewe km mke pesa ya matumizi, hivi mume kama huyu utampata wapi dunia hii ya leo?
mume amekupa miradi, hakuulizi pesa unapeleka wapi, bado unamkera? kiruuu
sisi wanawake wala hatujui wanaume wazuri, ndio yale ya MKATAA PEMA PABAYA PANAMWITA..
UNLESS anayosema huyu baba ni uongo lakni huyu mwanamke ana matatizo..
 
Ndugu yangu mimi kwa akili ndogo nilizo nazo nadhani chanzo kikubwa cha matatizo na mke wako ni wewe mwenyewe ingawa hujawa muwazi saana, ninavyojua ni vigumu saana kujaribu kumbadirisha mwenzio kabla ya wewe kubadirika! ni rahisi kwa kufanya mabadiriko kwako mwenyewe kuliko kwa mtu mwingine! siku zote wanadamu tumekuwa na fikira za kulaum wengine, mazingira, kipato.... list inaendelea, lakini ukweli ni kwamba tungekuwa na mtazamo wa kurekebisha matatizo kwa kujitazama wenyewe tungefanikiwa saana kutatua matatizo mengi. Ukweli ni kwamba chanzo cha matatizo yanayo mkabiri mwanadamu ni yeye mwenyewe au yako ndani ya uwezo wake.
Ninachoweza kusema kaa jitathmin wewe kwanza nini unachoweza kubadili/kufanya kwaajili ya ndoa yako, wewe kuwa mwema tu, hasira ondoa, mtoe out, mfanyie vitu vizuri tu, kuwa positive, mpongeze kwa achievements hata kama ni ndogo, utaona baada ya mda ndoa yako inaweza kuimarika saana na mkasonga mbele!
Nawaaombeeni Mungu awasaidie jambo hili liishe na hakika litaisha!
 
Kabla ya mambo yote dhibiti pesa yako.Acha kumpa mshahara wako, muondoe kwenye usimamizi wa miradi (tafuta mtu mwingine) hasa kwa kuwa ameonyesha uzembe kwenye eneo hili. Hakikisha baada ya miezi 6 hana access tena na miradi mingi. Hizo pesa atazitumia kuhonga viserengeti boys kuwa macho. Baada ya hapo anza tena kutafuta suluhu, sikushauri utafute nyumba ndogo japo mmmmhhhhh miaka miwili kavu kavu unaishije? Mimi hata miezi mitatu sitavumilia, tugombene kwenye mambo mengine lakini ndoa ni tendo la ndoa kama halipo maana yake ndoa pia haipo. Alikuja hapo kusimamia miradi?
 
Mpunguzie mkeo kipato labda ndio kinampa jeuri au pia labda ana mtu nje embu cheki na mafundi

inawezekana wanajua siri fulani.

Pole sana. Pia sisi wana jf tumkumbuke katika maombi yetu mungu amsaidie.
 
Back
Top Bottom