Ndoa yangu iko njia panda, nifanyeje?

Ndoa yangu iko njia panda, nifanyeje?

Kiukweli tatizo lipo,kama wewe umekua muungwana na umekuja hapa,inaonekana kuwa unahitaji suluhu.
"
Lakini suluhu hupatikana pale ambapo pande zote mbili zinapokuwa tayari kuitafuta,hili kwa mkeo kwa kiasi inaonekana halipo.
"
Kwa mujibu wa maelezo yako mkeo inaonekana na mtu pembeni,na pia haithamini tena familia.
"
Nimesema hivyo kwa kuwa umesema mnapogombana anakuwa hajishughulishi sana na mambo ya familia.Haya ni matokeo ya mtu mwenye ushirika na mtu mwingine.
"
Anaona familia sio yake na huduma yake kwenye familia hiyo ni kama msaada,hii inasababishwa na ushirika wake kwenye familia nyingine anayoithamini kwa sasa.
"
Kwa sasa ni kuwa kutokana na mambo yalivyo huenda akawa anafanya mambo kwa maelekezo kutoka kwa mtu mwingine,kuna uwezekano wa kukudhuru kama ni mpenda mali au huyo mtu mwingine ni mpenda mali.
"
Siwezi kukuambia uachane na mkeo,ila endelea kutafuta suluhu huenda ikapatikana ikishindikana,utaamua mwenyewe
"
"Mwanamke ni mtihani mwingine kwa mwanaume baada ya pesa",maneno haya yalizungumzwa na Lucky Dube alipokua anahojiwa na chanel 0 mwaka 2001!!

EIYER,
Nakushukuru, kweli option ya kuachana sio priority lakini yakinizidi basi. Nashukuru naendelea kuyafanyia kazi kweli inaniuma na kunipotezea heshma kwa watu wanaonizunguka
 
Rafiki,
Ndoa haina ushauri wa nje.

Odinyo,
Bahati mbaya mganga hajigangi, fani yangu inahusu pia mambo ya ushauri, lakini tulianza wenyewe kutafuta muafaka baada ya siku chache hali inarudia ile ile nimefanya hivyo several time na uzoefu kwenye ndoa ninao tene mwingi tu, lakini sasa imebidi kabla shetani hajakaa kati yetu ebu tuone watu wengine watasaidiaje. Nashukuru kwa hilo wazo lako
 
Aiseee... Hizi ndoa jamani..!!

Naanza kuogopa hii taasisi..!! Pole sana Kaka..!!

huyo mama ananishangaza jamani,miaka 21 kwenye ndoa hata watoto washakua ye bado analeta mambo ya watoto wanaoolewa leo , kweli dunia duara, usifikirie kumuacha bwana ila jikaze kumchunia , wamama wanapenda sana mwanaume akipay atention , so ukiuuchuna kwa mda atajirudi mwenyewe muanze kureconcile
 
Nina uhakika wewe ndio kikwazo kwenye hiyo ndoa na sio mkeo.jirekebishe.
1.punguza majukumu uliyompatia nusu
2.kuna kidume kinahudumiwa pembeni kama huoni hela na zilichofanyia.
3.hiyo miaka yenu imeanza kugonga life expectancy pataneni mfaane uzeeni jamani ni hayo tu.ila angalia wanawake noma asijekuwekea sumu ufe.kama ni wakristo mkonsult mchungaji wako tapika yote naye atapike yote mkaanze maisha upya.unategemea ukimbie nyumba mwanaume ujana umeulia hapo ,hapo umevallia jeans na kaptula ,nani atakupokea ukamvalie msuli weye!!!

NIVEA,
Nimekupata, sikatai kama siwezi kuwa na kasoro kama binadamu lazima, lakini ni kasoro kubwa kiasi gani hilo ndilo la msingi. Sijafikia hali ya kuvaa msuli wali si jadi yangu, najua nikichukua option hiyo nitapokelewa vizuri tu na wale wanaojali huenda lakini sitaki hilo lijitokeze nimeliacha iwe last resort.
 
kaka pole sana kwa makubwa hayo yanayokusibu ndani ya ndoa yako....nimesoma btwn lines na nimegundua machache ambayo yanaweza kuwa chanzo cha matatizo yako ya ndoa.

1- sijajuwa vizuri age difference kati yako na mkeo...isijekuwa umeoa mtoto mdogo ukilinganisha na umri wako na yeye akawa damu inamchemka wakati wewe inapoa..ndo maana 2years kakunyima ndoa unakutoa anapata huduma kwa sharobaro wa jirani kwako

2-hasira zako pia zinaweza kwa asilimia kubwa kuwa chanzo cha tatizo na kutopiga/kupigana hakumaanishi kuwa humuumizi mwenzako na hasa psychological torture kitu ambacho kwa wenzetu huwa kinawakaa sana moyoni na kuwaumiza sana...na naamini kwa hasira zako huwa unatoa kauli zinazomfanya yeye (kama mama wa nyumbani na msimamizi wa miradi unayoibuni wewe) kujiona akinyanyaswa.

3- ndoa yako hapo ilipofikia ni matunda ya uzembe wenu wote kwa pamoja kutokuwa karibu katika kushirikishana kipato na matumizi ya mapato ya miradi yenu... sio jambo jema na la hekima kusema kuwa hujui pesa ya miradi anayoisimamia mama inakwenda wapi na hasa ukiwa kama baba na kichwa cha familia...hata kama unampatia mshahara wako wote ni lazima ujuwe pia miradi imeingiza kiasi gani na kinatumikaje na yeye analipwa kiasi gani kwa usimamizi wa miradi hiyo.

4- nachokiona pia ni uoga wako wa kutaka kugawana mali mlizochuma pamoja na mkeo wa ndoa in 26 years. unanipa picha kuwa mngekuwa hamjachuma mali basi ulikuwa tayari kuachana na mkeo...hii inamaanisha upendo hakuna na uvumilivu umekushinda.

NASHAURI YAFUATAYO:-
1-KWANZA HUJACHELEWA BADO...JIFANYE MJINGA PIGA GOTI MUOMBE MSAMAA MKEO KWA YOTE YALE ANAYOAMINI KUWA UMEMKOSEA NA MWOMBE AKUPE NAFASI YA KUJIREKEBISHA MUANZE UPYA.

2-MPUMGUZIE KIPATO KISICHOKUWA NA MATUMIZI KWA KUMPATIA MAJUKUMU ATAKAYOYATEKELEZA KUPITIA MAPATO YA MIRADI YENU IKIWAMO KULIPIA KARO ZA WATOTO NA KULIPIA VITU KAMA INSURANCE ZA MAGARI, AFYA NA MENGINEYO ..HII ITAMFANYA AJIONE MWENYE MAJUKUMU NA KUMPUNGUZIA PESA AU KIPATO CHA YEYE KUMILIKI PASI MATUMIZI YASOJULIKANA.

3-MKUMBUSHE KUWA MULIPOFIKIA SIO TENA UMRI WA KUGOMBANA NI UMRI WA KUJENGE MAISHA YENU NA HASA YA UZEENI NA MAHUSIANO YAKO NA NDUGUZE YAWE KARIBU NA JITOLEE NA JITOE KATIKA SHUGHULI ZA SHIDA NA RAHA KWA UPANDE WA MKEWE..AMINI NDUGUZE WATAKUPENDA NA KUWASUPPORT NYOTE NA SIO KAMA SAHIVI WANAMSUPPORT YEYE NA KUONA WEWE UNAMNYANYASA.

4- KUWENI WACHAMUNGU NA MUNGU ATAWABARIKI NINYI NA UZAO WENU...KAMA NI MKRISTO MZURI UTAKUWA UNAFAHAMU HABARI ZA AYUBU.

who cares
thnx may be in 2 kwenye comments zako, kweli nikiwa na hasira nazitoa nje. kuhusu age tunapishana miaka 3, kama anatafuta damu changa basi utakuwa uroho wake tu hana sababu za kufanya hinyo. Siogopi kupoteza mali kwani hata sasa nikiamua kumvaa shetani bado naweza kuwa na mali nje na asijue hata kidogo na hilo silitaki. Ushauri wako kaka nimeuchukua, asante
 
Relax kaka. Hivi kweli huyo shetani unamruhusu avunje ndoa yako hivi hivi? Wewe kwa sababu ni muelewa endelea kutafuta suluhu ya hayo matatizlo, nina imani yataisha tena very soon. Bila wewe hao watoto wataathirika sana, watendeeni haki watoto wenu.

Huyo mama nahisi ni wakati wako wa kunyoosha mkono umchape makofi tena mengi ila usimtie ngeu. Omba likizo uanze kufatilia kimoja baada ya kingine, usione aibu. Ainisha makosa yake ya kishenzi yote halafu ita ndugu, jamaa na marafiki waamulie ugonvi.

Narudia tena usimruhusu shetani akakuongoza kwenye maamuzi. Mwanaume unahama unaena wapi?

Mungu akutie nguvu sana.

Caroline Danz,
Asante kwa ushauri, shetani ashinde tena alegee kabisa. Kwa nguvu za Mungu nitamshinda
 
CAROLINE DANZI...hapo nilipo-bold naona unataka ndugu yetu achezee mvua za kutosha....

kati ya kitu asichotakiwa kufanya ni hicho na kwa kosa hilo naona kina mama ananilea nkya na kijo helen bisimba na usu mallya wanavyo-mtolea uvivu ndugu yetu na kuishia segerea kwa miaka mi-5.

na akirudi anakuta mkewe keshaolewa na anawatoto wengine wa-3 na baba mpya na mali zote zishauzwa then anakuwa chizi au anakufa hapohapo.

WANAHARAKATI WA JINSIA WANASEMA MVUMO DUME NI MBAYA...ILA DONT EVEN THINK OF TRYING OTHERWISE...MVUMO JIKE UNAUWA SI MZURI KWA MATUMIZI YA BINADAMU HASA HUKU KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA.

Whocares,
Asante najali na nachukua kwa uzito unaostahili ushauri wako.
 
inauma sana kama ni mume wa namna hiyo halafu mkeo anakunyima mchezo kwa miaka miwili. Kama binadamu lazima nawe utakuwa na mapungufu yako lakini miaka miwili unatoka kapa!!! Duh! Una moyo sana mkuu!! Mie hata sijui nikushauri nini maana mengi inaelekea mmeshayafanya kuinusuru ndoa yenu lakini bila mafanikio. Pole sana mkuu.

bak,
nakushukuru kwa hilo
 
Nazani ubadilishe mfumo wa maisha uliyomzoesha,ya kumkabidhi mpk mshahara wako,mfanye akuheshimu kama baba wa familia,na maombi pia muhimu.
 
huyo mama ananishangaza jamani,miaka 21 kwenye ndoa hata watoto washakua ye bado analeta mambo ya watoto wanaoolewa leo , kweli dunia duara, usifikirie kumuacha bwana ila jikaze kumchunia , wamama wanapenda sana mwanaume akipay atention , so ukiuuchuna kwa mda atajirudi mwenyewe muanze kureconcile
SUPRISE,
Wanasema ukistaajabu ya musa utaona ya filauni. kwa sasa nikiona akina mama nahisi ni wale wale
 
Mshirkishe mungu kwenye hili jambo, kwa kufunga, kuomba na kushirikisha watumishi kimya kimya ili Mungu aingilie kati hili jambo. Unajua sometimes shetani anatest aone kama watu watarespond. Walio wengi wanamruhusu afanya kazi. Kwa hili tunakataa.
 
Nazani ubadilishe mfumo wa maisha uliyomzoesha,ya kumkabidhi mpk mshahara wako,mfanye akuheshimu kama baba wa familia,na maombi pia muhimu.

Penelope,
unajua mapenzi, nilidhani najenga kumbe nabomoa nia ilikuwa nzuri tu
 
Rafiki yangu aliyesimamia arusi yangu aliniambia kipindi fulani kuwa mke wake alimnyima tendo la ndoa kwa miaka 3 nikadhani ni uongo ni sehemu ya mazungumzo yakuniandaa kwa ajili ya ndoa kumbe inatokea..Da sijui kwangu ikianza kutokea itakuwaje..

JAmiii01,
Ukiona kwa mwenzako kunawaka moto anza kujiandaa na hilo sikujua kama mimi hayo yangekuwa hivyo, nikiona maandalizi ya kufunga ndoa yanafanyika zaidi nawaonea huruma
 
wakiitwa wenye ndoa na wewe huwa unaenda mkuu?
miaka 2 upo kwenye ndoa na tendo la ndoa hujafanya while masingle ..mot me ..daily wanapata?
tuyache hayo..huyo mwanammke kwa kweli anachokifanya sio kizuri ila mimi nakushauri mnyanganye vitu vyako vyote simamia miradi yako mwenyewe lipa madeni yako yote benki ,then hama hapo nyumbani kaanze maisha upya hadi siku utahama hii dunia
 
wakiitwa wenye ndoa na wewe huwa unaenda mkuu?
miaka 2 upo kwenye ndoa na tendo la ndoa hujafanya while masingle ..not me ..daily wanapata?
tuyache hayo..huyo mwanammke kwa kweli anachokifanya sio kizuri ila mimi nakushauri mnyanganye vitu vyako vyote simamia miradi yako mwenyewe lipa madeni yako yote benki ,then hama hapo nyumbani kaanze maisha upya hadi siku utahama hii dunia
 
Inakuwaje kuwa pamoja na makosa yote hayo ya mkeo na mazuri yote ufanyayo bado ndugu zako wana side na mkeo? Je kuna kitu kibaya ulichofanya ambacho hujakiandika?

Kama unajua kabisa kuwa ugomvi umeanza miaka 5 ilopita utakuwa unajua pia sababu ya ugomvi...kama unajua umeanza kunyimwa unyumba miaka 2 ilopita unajua incidence ilopelekea wewe kunyimwa unyumba.

Sidhani kuwa mkeo ni kichaa hadi afikie kumyima mumewe unyumba kwa miaka 2; mume anayempa mshahara wote. Kama ulitenda kosa kubwa na unaona vibaya kuliandika humu (which is okay with me) muombe radhi na muanze upya....wengi wanaoacha nyumba zao baada ya kuishi muda mrefu kama nyie hawaishii pazuri...tatua tatizo baada ya kukubali ulipokosea.
 
Fugwe ,usihofu kabisa kuhusu kushindwa kuisimamisha ndoa yako wakati wewe mwenyewe unajihusisha na mambo ya ushauri.
"
Ukweli ni kuwa unaweza kutoa ushauri au maamuzi sahihi pale tu akili yako itakapokuwa na utulivu.
"
Kwa sasa huna utulivu hivyo unaweza usitoe maamuzi sahihi,uamuzi wa kuomba ushauri ni mzuri sana.Unaweza kupata mawazo mema mengi,ila kuwa makini sana na ushauri pia.
"
Unaweza kum-PM Mtambuzi kwa ushauri zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom