Ndoa yangu iko njia panda, nifanyeje?

Fugwe

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,676
650
Nahitaji ushauri wenu wanaJF,
Ndoa yangu ina umri wa miaka 21 na mimi mwenyewe nina umri wa miaka 46. Katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 3. Mke wangu yeye ni mjasiria mali (siwezi kusema ni mama wa home) kwani anasimamia vijimiradi vya familia na mimi nimwajiriwa wa seriakli. Katika maisha ya ndoa mimi kama baba nimejenga nyumba 2, nina usafiri mzuri magari 3, nina mashamba 2 ya nguvu na vimifugo kidogo si haba. kati ya hivyo vyote hakuna senti iliyotoka mfukoni mwa wife. Nyumbani kama mnavyofahamu kuna facilities za kumuwezesha wife aihudumie familia kwa urahisi, kule kitchen kila kifaa cha kurahisisha mapishi kipo.

Sikilizeni tatizo lilipo, kama mnavyojua sahani zikikaa pamoja lazima zigongane, sasa ikitokea kutoelewana wife hawajibiki kwa maana sipikiwi chai, hakuna kusimamia mafundi na vibarua wataachwa wachakachue wapendavyo, achilia mbali tendo la ndoa ambalo lazima nisahau. Kaenda mbali ndugu kawaambia ninavyomnyanyasa nao bila kuuliza wameungana naye. mambo hayo ni karibu miaka 5 na zaidi hakuna maelewano ndani ya nyumba. Labda nijisemee na mimi, kweli najijua nina hasira lakini pamoja na hayo kwa miaka yote hiyo 21 ya ndoa sijawahi kunyosha mkono kumpiga wife, kurudi nyumbani usiku sio tabia yangu, sina mtoto wa nje wala small house na sijawahi lala nje hata siku moja. Nilikuwa nikipokea mshahara namkabidhi, then naomba hela ya matumizi lakini yeye hela inayopatikana kwenye vijimradi vyetu sijui inatumikaje.

Hatua tulizochukua kujaribu kupata muafaka, sisi wenyewe tumekaa several time hakuna kusikilizana ikabidi tushirikishe family friend tunakaa kidogo yanajirudia, ndugu wa pande zote wamejaribu hakuna muafaka, Hali iliyopo sisi wenyewe hatuwezi tena kuyamaliza ingawa ndio tulikuwa na dhamana ya kuyamaliza.

Nipeni ushauri, ni-sacrify kila kitu niondoke zangu? maana naona uchungu eti tugawane mali wakati najua nina madeni bank kwa ajili ya mali hizo ambapo yeye hakuchangia achilia mbali usemi wa sasa hivi kwamba mali ya ndoa ni ya wanandoa wote. Nitafute small house maana tunda nimeshanyimwa takribani mk2 sasa. Nisiwachose, maoni yenu tafadhali

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,528
Kuna uwezekano mkeo akawa limbukeni au amejiona sasa anaweza kuwa kila kitu bila wewe. Ingawa stori yako ni upande mmoja, uwezekano wa kukudhuru ni mkubwa hasa kama anatoka kwenye makabila yanayojulikana kwa tabia hiyo. Muhimu kaa ufikiri na umuite umpe ukweli wa moyoni bila vitisho wala kugusia kuwa unataka kuachana naye. Akijua kuwa una mpango huo atakuwahi na kukuharibia maisha. Ningekuwa wewe ningebadili usimamizi wa mali kiasi cha kupunguza kipato chake. Ningeweza hata kujaribu kumpunguzia hiyo biashara nikimpa somo kuwa kukaa nyumbani ni jambo muhimu. Kama anakunyima chakula cha bwana basi kuna kidudu mtu ambaye ameishamuingia. Fanya utafiti ujue kiburi chake kinatoka wapi ili ujue jinsi ya kupambana naye. Waweza kuanza ku-diversify miradi yako ili kuanza kukusanya nguvu mpya in case if anything happened. Nadhani kwa leo haya yanatosha mwanangu. POLE SANA KWA YANAYOKUKUTA.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,145
3,187
Mimi si mshabiki wa nyumba ndogo lakini mazingira yako hayo yanaweza kushawishi uwe na nyumba ndogo. Maana kuvunjwa kwa ndoa huko sishauri kabisa. Kinachoweza kufanyika ni kujikausha tu, na kujifanya kama huoni kinachoendelea, focus kwenye watoto kuhakikisha mahitaji yao yote wanapata lakini huduma nyingine za upendo na ndoa uzitafute mahali pengine.
Kama akiona hujali, anaweza kuanza kutafuta namna ya kureconcile. Kuna watu wengi hapa mjini wanaishi kwa style hiyo. Yeye home anarudi kulala na kwa ajili ya watoto na miradi yake tu. Ila ni jambo gumu pia, though ni nafuu zaidi kuliko kuachana.
 
Akijikausha na kuwa na nyumba ndogo atakuwa anamwanga mafuta kwenye moto. Si jibu ni balaa. Lazima afanye utatifi na kujua tatizo ni nini vinginevyo ataishia kuumia zaidi. Huwezi kujiingiza kwenye zinaa kwa sababu ya mtu. Kuna miwaya huko nje ukiachia mbali nyumba ndogo kumchuna na kumpunguzia kipato wakati madeni benki hayapungui. Go tell it the birds. Hujamsaidia bali kumuumiza zaidi.
 
kapistrano

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,244
450
Tuliza akili kiongozi kama mungu alikupa akili ya kutafuta hizo mali zote pmj na mkeo iweje leo ushindwe kukaa meza moja na kutatua hayo matatizo najua yanakupa wakati mgumu ila yashinde ndoa ni msoto.
 
neggirl

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
4,836
2,094
Mmh .. No comment!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
49,750
35,817
Nashauri ukae tena na mkeo tena sasa hivi ikiwezekana mkiwa na viongozi wa kiroho na hata wazazi wakiwepo tena ili kunusuru hilo tatizo. Usikimbie nyumba ukidhani ni suluhu, maana muda ulio kaa kwenye ndoa unaonesha una uwezo kabisa wa kutafuta suluhu tatizo ulilo nalo kwani najua umekutana na mengi na umeweza kuyatatua!

Hili swala lisikuvunje moyo jaribu kuwa shirikisha viongozi wa kiroho kwanza.
 
Neylu

JF-Expert Member
May 28, 2012
2,942
1,838
Aiseee... Hizi ndoa jamani..!!

Naanza kuogopa hii taasisi..!! Pole sana Kaka..!!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
Miaka 21 ya ndoa, na umenyimwa unyumba kwa miaka 2 sasa? Nina hakika mkeo alishavumilia mengi na wewe ukamvumilia haswaa. Umebold sana fact kuwa mkeo anasimamia miradi ya familia, lakini hatoi hata senti pamoja na kuwa anahodhi mshahara wako wote. Na unajiongelea kuwa una hasira. Je ndo kosa pekee aliloliona kwako? Sema vizuri ni nini kimemchefua mkeo kiasi hicho? Na kama hauwezi kusema, hasira zako zimetokana na nini?

Hapo ulipo small house itakuchosha zaidi kakangu. Nakushauri kuwa mpole. Msamehe mkeo na kumuombea. Akiona upole wako bila kuzozana huenda akagundua anapokosea. Ikishindikana mtafute ndugu yake ama rafiki yake ambae unajua anammudu, uongee nae na akaongee nae wakiwa peke yao.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,145
3,187
Akijikausha na kuwa na nyumba ndogo atakuwa anamwanga mafuta kwenye moto. Si jibu ni balaa. Lazima afanye utatifi na kujua tatizo ni nini vinginevyo ataishia kuumia zaidi. Huwezi kujiingiza kwenye zinaa kwa sababu ya mtu. Kuna miwaya huko nje ukiachia mbali nyumba ndogo kumchuna na kumpunguzia kipato wakati madeni benki hayapungui. Go tell it the birds. Hujamsaidia bali kumuumiza zaidi.
Nakubaliana na wewe mkuu. Kwa kweli nimesema tu katika harakati za kupapasa wapi kwa kuanzia. Lakini kusema ukweli nyumba ndogo na yenyewe ni balaa nyingine. Kwenye UKIMWI anaweza kuwa na tahadhari tu. ILa sema changamoto zingine za nyumba ndogo na zenyewe ni balaa. Lakini pia ukijaribu kuangalia huyu bwana anasema tayari ameshashirikisha hadi wanafamilia kulijadili hili lakini hawajapata majibu. Inawezekana kuendelea kumchunguza lakini wakati mwingine kumuignore linaweza kuwa ni jibu lingine. So inaweza isiwe lazima sana kwamba awe na nyumba ndogo lakini akaamua kumuignore tu mke wake.
 
Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
61,279
66,111
Kaa na mkeo na ndugu wa pande zote mbili, ikiwezekana na kiongozi wa kiroho(Hawa ni kama mashaidi).
Mueleze mke wako jinsi unavyompenda na jinsi unavyojisikia juu yake na kumuhitaji.
Mpe nafasi ya kujieleza na aeleze kinagaubaga wapi anaona tatizo lipo na nini sababu ya kufanya abadilike.
Onesha ukali kama mwanaume pale inapobidi, onesha kila kitu kilichokukera juu yake pia.
 
Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,729
4,581
usauri wangu ni huu .

1. chugnuza asira zako kwake zinatokana na nini kwa nini unahasira..

2. achana na wazo la kutafuta nyumba ndogo hili litakuharibia kabisa

3. kama mmefunga ndoa a kanisani nendeni mkawaone mapadre/wachungaji wawasaidie juu ya hili ili kiini kijulikane

4. baadhi ya wanawake wanaposhika pesa pengine nyingi kuliko mume wake hata kama mtaji na mambo yote mume ndio kawezesha huwa wanaota mnara wa kiburi na dharau ya hali ya juu sana nani ngumu kujinasua toka katika mnara huo wa kiburi ...cha msingi anglia njia mpaya ya usimamizi wa miradi yako na kazi zako ..mpunguzie kazi na usimamizi wa mali

5. kwa nini anakusema kwa ndugu zake kuwa unamnyanyasa? ni kweli unamnanyanyasa? ...hebu jichunguxe katika hasira zako..wewe hapo ulipo una wasilina na ndugu zake/wako vizuri?

6. hizo pesa anazokusanya huwa anapeleka wapi kama wewe hujui lolote juu ya pesa hizo? ....kuwa makini sana juu ya hili lazima ujue anaingiza kiasi gani na anatuna wapi na status ikoje huko ziliko(benk)

7.hakikisha ugomvi wenu hauathiri ukuaji wa watoto na watoto waepushwe ni mgogoro wenu..kuwa nao karibu

8. hakikisha una take-control ya mali zote kuanzia usimamizi hadi utunzaji wa pes

9. tuliza akili yako il hakikisha unayatawala mazingira na si mazingira yakutawale hasa mambo ya unyumba uliyoyakosa kwa mda sasa

10. wakai unafanya jitihada zote hizi hakiisha unasali na kuomba Mungu .....kikubwa zingatia kumpunguzia kazi na usimamizi wa mali..
 
gongolamboto

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
1,152
539
Kuna uwezekano mkeo akawa limbukeni au amejiona sasa anaweza kuwa kila kitu bila wewe. Ingawa stori yako ni upande mmoja, uwezekano wa kukudhuru ni mkubwa hasa kama anatoka kwenye makabila yanayojulikana kwa tabia hiyo. Muhimu kaa ufikiri na umuite umpe ukweli wa moyoni bila vitisho wala kugusia kuwa unataka kuachana naye. Akijua kuwa una mpango huo atakuwahi na kukuharibia maisha. Ningekuwa wewe ningebadili usimamizi wa mali kiasi cha kupunguza kipato chake. Ningeweza hata kujaribu kumpunguzia hiyo biashara nikimpa somo kuwa kukaa nyumbani ni jambo muhimu. Kama anakunyima chakula cha bwana basi kuna kidudu mtu ambaye ameishamuingia. Fanya utafiti ujue kiburi chake kinatoka wapi ili ujue jinsi ya kupambana naye. Waweza kuanza ku-diversify miradi yako ili kuanza kukusanya nguvu mpya in case if anything happened. Nadhani kwa leo haya yanatosha mwanangu. POLE SANA KWA YANAYOKUKUTA.

Umenena. Sasa hivi wanawake wameingiliwa na haka kaugonjwa. Hauko peke yako kaka. Dhibiti pesa tu atanyooka
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,376
22,818
mweh!mweh!here we are again!
sasa kama haya ni kwa miaka 21 wengine inakuwaje?
naogopa sana mimi!
ni busara ipi yatatikana kuepuka haya !?hizi ndoa huwa tunamfungia nani?
hvi kama kweli mwenzi wako wa ndoa ni ubavu wako na mwili ndani ya mwili wako tunaruhusu vipi ndoa zetu zinafika hapa!
mi nakosa lakusema to be frank!
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,078
17,743
Jamani pamoja na ndoa kuwa na miaka 21 bado kuna madudu ya namna hii Aisee naitaji miaka ya kama mitano mingine ya kutafakari ndoa nione kama nitashawishika kuingia la sivyo wacha nizeeke tu kha.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,771
23,031
kwanza keti na mkeo mwambie akupe solution, kama mwanamke zinamtosha atakupa akigoma fanya maamuzi magumu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom