Ndoa imenizawadia kiharusi

Pole sana mkuu...
Naamini utapona majeraha ya moyo na maumivu ya mwili...
Unatakiwa ujihurumie wewe kwanza kwa kupambania afya yako, na kama vipi mtengane tu.. japokuwa tumesikiliza upande mmoja lakini ushauri wa jumla ni kuepuka maumivu!
Shkamoo mapenzi... ..kuna mtu alifungwa, na kupoteza kila kitu.. na akapewa masharti kwamba ili atike jela anatakiwa kufata wanachotaka hao .. waliomtia kimiani!
 
Mkuu umeongea kiuchungu sana.
Kuwa kivyako tu.
Ni nao wa3 ila kila siku kero tu.
Sasa maamuzi ni kupiga kimya tu.
Sina kiharusi ila sitaki kero.
Mtu aende Kwa mama maisha yakimshinda mjini.
 
Pole sana mkuu inshallah utakaa sawa mie mzee wangu ana miezi 6 Toka amepata stroke ila kwa sasa anaweza kutembea na kufanya Kila kitu ni muhimu ndugu yangu uwe unawaona physiotherapist watakusaidia stroke inapona epuka kuwaza sana na hiyo ni presha ndio imepelekea ukapata kiharusi usiache dawa za presha ndugu yangu Inshallah utakaa sawa
 
Ukweli mchungu ni kwamba Wanaume wengi hawafi kwa ajali wala magonjwa wala vita. Wanaume wengi wanakufa kwa msongo wa mawazo, ukimya, na presha ya maisha.

Mwanaume haambiwi pole, haambiwi utashinda, haambiwi jipumzishe kwanza badala yake, kila mtu anamuangalia kama kiwanda cha miujiza – cha kutoa pesa, upendo, msaada, faraja, na subira bila kuchoka.

Anapoamka asubuhi, anawaza:
“Leo watoto wale nini, Leo watoto watatibiwa vipi, Niwapelekee nini wazazi, Kodi ya nyumba imeisha, umeme umeisha, nina kiatu kimoja nacho kimechakaa

Lakini bado atavaa tabasamu.
Ataandika "good morning" status.
Ataambia watu, “tuko vizuri tunaendelea vizuri "

Hawajui kwamba mwanaume huyu usiku analala kitandani lakini hapati usingizi, akiwaza kesho itakuwaje. Anaota ndoto ambazo hazitimii. Anavuta pumzi nzito lakini hakuna anayemsikiliza. Ataomba ushauri, atadharauliwa. Ataomba msaada, ataambiwa “we si mwanaume wa kweli, jikaze mwanaume, mwanaume ni kupambana.

Na mbaya zaidi...
Wanaume wengi wanajitahidi sana kwa wanawake ambao hata hawathamini wala kutambua mchango wao. Wanatoa kila walichonacho kwa mtu ambaye hayuko tayari hata kumshika mkono wakati anadidimia.

Mwanaume anapokata tamaa, halii. Ananyamaza. Akinyamaza – anaumia. Akiumia sana –anapata msongo wa mawazo, anaanza kufa kidogo kidogo tena anakufa kimya kimya.

Hebu leo hata kama bado mwanaume wako hajafanikiwa, msalimie mwanaume kwa upendo. Muambie unathamini sana juhudi zake na unautambua mchango wake. Mtie moyo, msaidie hata kwa neno. Usingoje afe ndio umwite “shujaa”.

Mwenyekiti nasisitiza tena, Mheshimu sana mwanaume wako, wanaume wanapitia magumu mengi sana katika maisha. Tunaelewana lakini?
 
Na bado Mungu atazidi kukutendea mambo chanya na mazuri zaidi.
Mwamini Mungu zaidi, mfanye awe namba moja.
 
Na ukiumwa,unaweza kosa wa kukutawaza.

Too bad mda mwingine unaweza kuwa na mtu na akashindwa kukutawaza vile vile.

Kua single ni raha, shida inakuja mtu ukizeeka.

Ni kweli lakin pia unaweza zeeka na mtu yupo na ukakosa matunzo vile vile tena mda mwingine ukiwa na mtu ambaye sio sahihi anaweza kuwapa sumu mpaka watoto mliowazaa wenyewe nao wakakutenga kwasabab wanazozijua wao wenyewe bila kujali umri wako. Na hapa naongelea familia uliyoelea mwenyewe mpaka hapo kwenye uzee wako.

Hapa ndo utajua hii Dunia Haina formula, hapa ndo utajua kumbe point ni kuwa na mtu sahihi tu lakin sio ili mradi uwe na mtu ili likitokea akusaidie, No! anaweza kuwepo na asikusaidie vile vile.

Bora ukose wakukuangalia unapokua single au uzeeni kuliko awepo halafu akukimbie au asikusaidie, haloo hii inauma zaidi kuliko ujue umekosa kwasabab ya u single wako lakin sio ile yupo lakin ndo hivyo kazingua, huwa inauma zaidi.
 
Kuna mzee pia alipata stroke kwa matatizo kama hayo.

Mkewe alikua anakitembeza kwa serengeti boy waziwazi na wana watoto wakubwa kabisa.
Ile dharau mzee ilimletea shida sana, pamoja na kua anaumwa bado mke anamletea majengeka.

Kuiolea jamii nako ni changamoto sana.
 
Mkuu, mkandamizaji ni mchungaji kabisa lakini alikandamiziwa mkewe
 
Upo sahihi.
Lakini sio wewe muhuni huna hofu ya mungu utafute mke mwenye hofu ya Mungu, ni kwenda kumtesa tu dada wa watu. Hofu ya Mungu muwe nayo wote wawili ndo mambo yataenda vizuri.
Mwanaume anapendeza akiwa muhuni hata kama ni kidogo tu. Sasa mwanaume awe amepooza tu, hana udikteta hata kidogo, hana circle ya wanawake wa kumpa wasiwasi kidogo wife. Hiyo ndoa si itakua bored.
 
Ni wengi wanapitia hiyo hali. Lakini wanaofaidi ndoa ni wale never mind kwenye ndoa yaani ameyaweka maisha ya ndoa kama hana cha kupoteza. Huyu anaweza kuacha mke muda wowote.
Cha muhimu kujua kwenye ndoa za siku hizi ni kujijali kwanza wewe. Usione shida kuachana nae hata ikibidi kumuachia kila kitu ili kuokoa nafsi yako.
Ndoa inahitaji akili sana kama unahitaji kudumu kwenye ndoa. Mimi baada ya kuona tomuch,chap nikaamua kufungua biashara wilaya nyingine mbali na tulipo. Kwa hiyo muda mwingi naumalizia huko,ndio kupumzika kwangu. Hapo ndio nikamuachia mtihani yeye na ujuaji wake sana. Nakuambia mpaka nina amani sana. Home naenda siku za weekend tu. Watoto wote nimewaweka boarding. Sijali kama wahuni wanapiga. Japo ni ile aina ya wanawake wanaomjua MUNGU sana ila ndani ya nyumba wa moto sana. Hakupi nafasi ya kuongea. Yeye kila anajiona yuko right (sijui nikutumbukiaje?} Kwa hiyo mimi ni vitendo tu.

Bado nawaasa vijana kuoa au kuolewa sio lazima wala sio kitu muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…