Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Hili nalo neno
Ndo maan lazma asitishe unyumba,kulala chumba kimoja na chakula km akil ale alichopakuliwa mtoto
Vya kutengewa sumu nje njeee

Ila kwa ajili ya watoto sio kosa lao
Aendelee kuwepo kwny huo mji
Mahitaji ya kiutu uzima atafte mchepuko ampime wakielewana amuoe

Nasisitiza asitoe talaka
Ili Wasigawane mali lakini
Mali Mali Mali........kugawana!?.usikute demu mwenyewe ni goal keeper 🔥🔥🔥🔥.
 
Hiyo ndoa kwa nini anataka Kuingangania...???? Yeye ndo analelewa na mwanamke au??? Hapo ni atafute mwanamke wa kulelea mwanae tu ni BORA MARA 100 AOE SINGLE MAZA MWINGINE AMBAE JAMAA AKE ALIFARIKI[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kiukweli huyo dada kazingua sana, siyo tu kuchepuka kaamua kuzaa nje kabisa na kumletea mtoto mume wake aibu, Kama walikua wanapendana na huyo ex wa utotoni, why wasingehakikisha wanaoana. Kuliko hivo unaolewa na mtu mwingine ikiwa akili yako ipo kwa mwingine, si vizuri na unamtesa mume uliyemkubalia akuoe na watoto pia ikiwa mtaachana.

Ushauri wangu ni uzinzi ni kosa ambalo linaweza kutenganisha wanandoa, so busara itumike kama wataamua kulinda maslahi ya watoto. Ila kama mioyo yao ni mizito kuendelea watengane tu.

Wanandoa jiheshimuni bana hadi umeamua kuoa/kuolewa means umeamua kutulia na kuachana na mambo yote ili kujenga familia,tulieni kwenye ndoa zenu.
 
Updates Ya Kikao

Ndugu wamekusanyika nyumbani kwa mzee
Ndugu wa mwanaume;
Baba na mama
Wajomba wote
Shangazi wote
Msimamizi wa ndoa
Mume (Kaka)
Mimi na ndugu zetu wengine

Ndugu wa mwanamke
Baba na mama
Wajomba wake
Shangazi zake
Msimamizi wa ndoa
Mke (shemeji) na dada yake

Mwenyekiti wa kikao ni mjomba wetu (Kaka wa mama)

Mume ameanza kutoa maelezo yake...
Anaelezea namna alivyothibitisha na alivyothibitishiwa na mkewe kuhusu baba halisi wa mtoto, Moses

Kuna utulivu wa wastani, kila familia imekaa upande wake..

Kwakuwa siwezi kuandika kila kitu, tarudi badae kwa ajili ya kutoa hitimisho litakalofikiwa..
 
Okay....safi
 
Akilinda ndoa , je baba halisi hatawahi kuja kudai mtoto wake ? Mtoto ataitwa ubini wa nani kati ya hao wawili? Huyo mwanaume abebe nguo zake atokomee gizani kwani anaweza kufanya jambo baya sana.Na akifika huko asimuhadithie mtu tukio hilo.Pole sana mfikisha madam ambaye pia ni mhanga.Hata ukifunga na kuomba Mungu hatoi jibu hapo.
 
mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.
Dhambi pekee isiyosameheka ni uasharati. Pole kwa Bro, pole kwa watoto ambao wanaenda kuingia kwenye mateso wasiyostahili!
 
Sababu za kupima DNA na kutaka kujua zitumike kuamua kifuatacho.
 
Hakuna swala gumu hapo. Ni talaka tu. Sababu za kufanya hivyo zipo wazi na hakuna atakayelaumu. Mambo mengine yanapangiliwa.
 
Habarini!!!
Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga
Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.
Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.
Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yake...pia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.
Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda.
Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake..

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)
Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake..
Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.
Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.
Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni...na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa..
Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!

Pole sana kwa mwanaume aliyekutwa na hili

Yeye na mke wake tuu ndio wanaweza kuamua nini kifanyike. Sisi tumesikia ya upande mmoja ila hatujui kama kuchepuka huko kulikua ajali au alidhamiria? Hatujui wachepukaji walichokua wamepanga baada ya mtoto kuzaliwa.

Hii inauma sana lakini sasa Mwanaume ajiulize nafsini mwake na amuombe Mungu ampe maamuzi sahihi anaweza kuamua kumuacha huyu aliyechepuka akazaa akakutana na asiyechepuka, au anayechupuka asipate mimba, au anayechepuka akapata mimba asizae badala yake akaitoa au akakutana na asiyechepuka kabisaa
 
Habarini!!!
Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga
Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.
Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.
Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yake...pia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.
Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda.
Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake..

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)
Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake..
Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.
Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.
Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni...na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa..
Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
Pole sana....ameoa mke wa mtu.
 
Amtafute mtu anaitwa Joka jeusi atamshauri vizuri mimi nimeshindwa
 
Back
Top Bottom