Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Ndoa imeingia doa. Msaada wa mawazo unahitajika sana

Habarini!!!
Ndoa ya ndugu yangu wa damu (kaka) imeingiliwa na kirusi hatarishi, maji yamezidi unga
Alimuoa binti (mke wake) kigori kabisa, na kwa utamaduni wetu, hili huwa tukio la heshima kwa muaji na waozeshaji (familia ya binti) pia.
Baada ya miaka sita ya furaha na huzuni, ndoa ya ndugu yangu imesimama wima, ikiwa na jumla ya watoto watatu, wakiume wawili na kabinti.
Kati ya watoto hao, mtoto mmoja (wa tatu) hafanani kabisa na watoto wengine, na hafanani na baba yake wala mama yake...pia hafanani na yeyote katika familia yetu wala ya mwanamke.
Jambo hili lilimpa shaka bro, alijipa moyo lakini uafrika wetu ukamshinda.
Maswali ya "mbona hafanani na sisi?" yalikuwa mengi, jambo lililomfanya bro aamue kutafuta suluhu ya nafsi yake..

Alianza kwa kupima DNA kwa Siri bila yeyote ndani ya familia kujua...majibu yakaonesha si wake (Tz)
Akaenda nae Nairobi, huko akampima tena, ikaonesha si damu yake..
Kwa maelezo yake, anadai alienda kwa gwiji fulani huko Mombasa, nako akaambiwa si damu yake... Zaidi tena huko Mombasa, huyo mama (mganga) alimuonesha baba halisi wa mtoto yule

Bro alirudi kwake, akamkalisha kitako mke, akatumia maarifa na ujuzi wake wooote aliojaaaliwa kumshawishi mke amwambie chochote juu ya mtoto yule.
Japo lilikuwa jaribio gumu, lakini mke alikiri kuwa Moses, mtoto wa mwisho, si mtoto wa kaka. Na akamtaja baba yake halisi.

Picha iko hivi;
Shem katika makuzi yake, alikuwa na rafiki yake (mtoto mwenzake) ambaye walitengana baada ya familia ya huyo kijana kuhamia mkoa mwingine. Walipokua, walitafutana na wakaendelea kuwasiliana km wapenzi hadi shem alipoolewa.
Lakini licha ya kuolewa, mawasiliano yao yaliendelea na ahadi yao ilikuwa wazae mtoto mmoja ili iwe kumbukumbu ya mapenzi yao tangu utotoni...na walipokuwa wakipata nafasi ya kukutana, basi walikuwa wananyanduana hadi mtoto huyo akapatikana..

Bro anataka kufanya maamuzi; ni moja tu kati ya mawili
1. Avunje ndoa au
2. Alinde ndoa

Binafsi km mshauri wa karibu, nimemshauri alinde ndoa..
Kaniuliza KWANINI? Nimekosa jibu!
Watoto wengine wanabadiliswa hospitali kwa makosa au kwa kujua hivyo mtoto akija kwako ni wako mengine ni kujutafutia rahana
 
1
Alinde ndoa ya 1
Kwa ajili ya wanae wale 2

2
Aoe mke wa pili kupooza nafsi.,ya kiserikali..siku akiona kampenda mtu wakubaliane amuoe mke wa 2 ht km ye ni mkristo

3
Asimtaliki wa mke kwanza kuepuka kuvunja familia na kugawana mali nk...
Akioa atakuwa ametoa adhabu
Akimuacha atakuwa amempa nafasi ya kwenda kwa mpenzi wake wa utotoni[emoji1787]
Watoto nao ndio wanampa msongo zaidi
 
Analinda ndoa kwa ushahidi wote alionao! Mimi namshauri atengane nae tu hakuna jinsi hili ni kosa la kudhamalia na likimkakati. Ni ngumu sana kumpenda huyo mtoto. Sasa anaishi vipi na msaliti ama anataka awekewe mafuta ya moto puani wakati kalala.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
mbona mwanamke hajapambana kuilinda yeye ndo apambane hamna kitu kama hicho yani mke umeoa anadhamiria kabisa kuzaa na mtu wa nje unasema alinde ndoa??
Apige chini atakuja kufa siku si zake huu ujinga ndo unaua wanaume wengi ni upumbavu ingekua hiyo mimba iliingia bahati mbaya kwenye kuchepuka unaweza kuwaza ila kadhamiria kutoka moyoni kuzaa na mwanaume mwingine huku kaolewa hapana asee.

Kama kaweza kuzaa kwa hiari means anampenda mshkaji sana next step ni akiambiwa muekee sumu tu tulee mtoto wetu ndo atajua alipambania ndoa au mauti.
Hili nalo neno
Ndo maan lazma asitishe unyumba,kulala chumba kimoja na chakula km akil ale alichopakuliwa mtoto
Vya kutengewa sumu nje njeee

Ila kwa ajili ya watoto sio kosa lao
Aendelee kuwepo kwny huo mji
Mahitaji ya kiutu uzima atafte mchepuko ampime wakielewana amuoe

Nasisitiza asitoe talaka
Ili Wasigawane mali lakini
 
Kama bado wanapendana na kuishi kwa amani, yaani mwanamke bado ana upendo na wanaishi vema, nashauri wayamalize tu kwa kusameheana na waendelee kulea familia! nina amini walichokijenga ndani ya miaka 6 sio kidogo, hivyo kukivunja ni kujirudisha nyuma!
Zaidi ya yote tukio hilo nina hakika limeshampa mwanamke funzo kubwa, hakika hatokaa tena azae nje maana alifanya siri kubwa lakini ameumbuka!
 
Hofu iko hapo kwenye kuendelea na jamaa
Kurudiana hawezi zuia wether wametengana ama wako wote

Ila kuendelea kuishi nae kama mke inachochea ye kumrudia jamaa kuliko wakiacha kulala km mke na mume...

Watoto wana umri gani?
Na ana jeuri ya kumuacha kweli huyo mke?.!
Mana usijitie kusema tuachana na umemfia mwenzako
 
mbona mwanamke hajapambana kuilinda yeye ndo apambane hamna kitu kama hicho yani mke umeoa anadhamiria kabisa kuzaa na mtu wa nje unasema alinde ndoa??
Apige chini atakuja kufa siku si zake huu ujinga ndo unaua wanaume wengi ni upumbavu ingekua hiyo mimba iliingia bahati mbaya kwenye kuchepuka unaweza kuwaza ila kadhamiria kutoka moyoni kuzaa na mwanaume mwingine huku kaolewa hapana asee.

Kama kaweza kuzaa kwa hiari means anampenda mshkaji sana next step ni akiambiwa muekee sumu tu tulee mtoto wetu ndo atajua alipambania ndoa au mauti.
Sasa ujinga wa mmoja usiwafanye nyote kuua familia. Kama mwanamke kashindwa kuilinda haina maana kuwa na mwanaume nae ashindwe
Asiache mke ila labda watengane vyumba hapo ndani..wasishiriki tena unyumba..

Aendelee kukaa ili watoto waone wako pamoja..
Wakikua wataelewa

Kupooza nafsi atafte nyumba ndogo..aanze maisha mengine huko..awe na miji 2...

Hataweza tenganisha maisha yake 100% na huyo mke cz of watoto..
Whatever happens afikirie watoto huyo ni mama yao..
Nahis huyo👆👆 kaelezea sawa na nilichokuwa namaanisha
 
mbona mwanamke hajapambana kuilinda yeye ndo apambane hamna kitu kama hicho yani mke umeoa anadhamiria kabisa kuzaa na mtu wa nje unasema alinde ndoa??
Apige chini atakuja kufa siku si zake huu ujinga ndo unaua wanaume wengi ni upumbavu ingekua hiyo mimba iliingia bahati mbaya kwenye kuchepuka unaweza kuwaza ila kadhamiria kutoka moyoni kuzaa na mwanaume mwingine huku kaolewa hapana asee.

Kama kaweza kuzaa kwa hiari means anampenda mshkaji sana next step ni akiambiwa muekee sumu tu tulee mtoto wetu ndo atajua alipambania ndoa au mauti.
Hapa ndipo bro anaposimamia...
Kuzaa kwa kukusudia ni ujasiri usiopimika
Yaan hata yey anasema inaweza kufikia wakaamua wamuue, na mke akakubali
 
aloo hapo kama ni Mimi ndoa imeishia hapo, yani mke azae nje na mtu mwingine alafu Mimi nikaushe tu aloo hapo pangumu sana.
 
Dunia sio fair jamaa anakosa raha kabisa Mungu ampe upeo,[emoji36][emoji36][emoji36]ndoa izi usaliti unauma sana

Ila zile mambo unamuacha then anaenda kuoa mke aliyeachwa ndo yale yale
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] utaona na yey anaerud kwa aliyemwacha
 
Akioa atakuwa ametoa adhabu
Akimuacha atakuwa amempa nafasi ya kwenda kwa mpenzi wake wa utotoni[emoji1787]
Watoto nao ndio wanampa msongo zaidi
Aoe tu atulize nafsi

Ila huyu pia asimtaliki rasmi mana kuna watoto ..nani atawalea?
Ht km akidai talaka aseme bado anampenda mkewe talaka haitoki hapo
Atabaki analea wanae
 
Uyo kaka Ako amtafute uyo jamaa wakae
Ampige hata 2-3 za baridi na amshukuru kwa kumlindia mkee

Unaweza Kuta jamaa alikua mvumilivu aombi papuchi ovyoo na anafanya Binti asitongozwe ovyo kwa kumpa kampani

Uyo mtoto amlee kama mtoto wa mke wake na ampe heshima zote kama mtoto wake unaweza Kuta ndo baraka katika familia iyo
 
Mhhh

Umesema alikua bikra,huku mbele alikua na mpenzi wa utotoni!!!
Kama alikua bikra huyu mpenzi wa utotoni kiasi cha kutosahauliana walikua wana t****na kwa macho kiasi cha bro ako kukuta bikra????
Utoto ulikuwa urafiki (watoto wanaokuwa pamoja)
Baadae walipokuwa vijana ndio wakawa wapenzi ila kwa kipindi chote hadi mke anaolewa alikuwa hajawahi kukutana na mwanaume, hata huyo wa utotoni.
 
Mwanaume una advantage ya kuoa fasta tu..unakua na miji 2..nyumba kubwa kwa ajili ya watoto
Nyumba ndogo mapenzi baasi

Ila nani ataoa mke ana watoto 3?!

Talaka ni maumivu makali asijaribu

Shida hapa nahisi bado anampenda mkewe!
 
Analinda ndoa kwa ushahidi wote alionao! Mimi namshauri atengane nae tu hakuna jinsi hili ni kosa la kudhamalia na likimkakati. Ni ngumu sana kumpenda huyo mtoto. Sasa anaishi vipi na msaliti ama anataka awekewe mafuta ya moto puani wakati kalala.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Kwa hakika kila nikijaribu kumshauri kutomuacha mkewe, maswali anayoniuliza yanakosa majibu
Wakati mwingine hata mm najiuliza what if ningekuwa mim...
 
Mkioa mjue Kuna kuchapiwa... Mlivoambiwa kua myaone mlizani nn [emoji23][emoji23]
 
Kama bado wanapendana na kuishi kwa amani, yaani mwanamke bado ana upendo na wanaishi vema, nashauri wayamalize tu kwa kusameheana na waendelee kulea familia! nina amini walichokijenga ndani ya miaka 6 sio kidogo, hivyo kukivunja ni kujirudisha nyuma!
Zaidi ya yote tukio hilo nina hakika limeshampa mwanamke funzo kubwa, hakika hatokaa tena azae nje maana alifanya siri kubwa lakini ameumbuka!
Uko sawa, lkn kumbuka machozi sio kipimo cha majuto[emoji1787]
 
Back
Top Bottom